Chelsea FC (The Blues) | Special Thread

Chelsea FC (The Blues) | Special Thread

Shida ilikuwa kwa midfield brother...kaangalie tena replays.

Halafu pia ndiyo maana nimependekeza Morata - kwa msimu huu tu lakini - atokee benchi.
Hakukuwa na shida kwenye midfield katika ile game labda tunatofautiana katika kuusoma mchezo.
Back to the point,Morata atokee bench 19 games zilizobaki hivi mkuu are you serious na unachozungumza kweli?
Kweli Chelsea itamaliza nafasi ya 2/3 kwa kuanza na Willian Hazard Pedro?
Nadhani hutaki kumuona Conte akiwa Chelsea msimu ujao
 
Hakukuwa na shida kwenye midfield katika ile game labda tunatofautiana katika kuusoma mchezo.
Back to the point,Morata atokee bench 19 games zilizobaki hivi mkuu are you serious na unachozungumza kweli?
Kweli Chelsea itamaliza nafasi ya 2/3 kwa kuanza na Willian Hazard Pedro?
Nadhani hutaki kumuona Conte akiwa Chelsea msimu ujao
Definitely haitakuwa mechi zote.
 
Tatizo Chelsea always kuna Head Coach ambae ndio Conte kwa sasa hakuna Team Manager.Tofauti ya Head Coach na Manager ni kwamba Manager anakuwa na authority kubwa zaidi katika timu.Katika suala la usajili Conte anaweza kupendekeza wachezaji anaowataka lakini sio mara zote Club itakubaliana nae sometimes anaweza kumtaka huyu akaletewa yule kwasababu yeye hana authority kubwa katika swala hilo ndio maana wachezaji wengi ambao anawataka huwa hawapati au anachelewa kuwapata.Kuna mama mmoja anaitwa Marina Granovskaia na Michael Emenalo kabla hajaondoka hawa ndo wana deal na biashara zote za timu zinazohusu mikataba kwahiyo ukipendekeza mchezaji wasipompitisha wao hatokuja ng'o.
Conte alipendekeza majina ya washambuliaji anaowataka majira ya joto lakini matokeo yake walimletea Morata tu.
Kiukweli hii ni changamoto sana, nakumbuka msimu huu kipindi cha usajili.. Mapenndekezo mengi ya konte yalitupiliwa nje
 
Mimi nafikiri ni muda muafaka WA kumrudisha kocha Carlo Ancelote, ni kocha mzoefu amewahi kufundisha klabu kubwa ulaya kama Bayern Munich, Real Madrid. Tukiendelee na huyu kocha Conte hatuzi, ameishiwa mbinu, nina wasiwasi kama tutaweza kuizuia Barcelona.
SASA, mbio za ubingwa EPL, hatumo KBS
 
Unajua kwamba ukianza hivyo unakosa quality ya no 9? refer game ya City alipotoka Morata akaingia Willian kilichotokea mabeki wa kati wa City wakapata likizo ya muda uwanjani.Hio formation ya kuanza hivyo ina work tunapocheza na timu ambazo ni under dogs lakini huwezi kucheza msimu mzima hivyo it won't work out.
Morata yuko fit, probably ataanza game ya leo
 
tulifanya kosa kubwa kumruhusu kosta aende morata alitakiwa ajifunze nyuma ya kosta
Halikuwa kosa kumuondoa Costa kama ulifatilia scenario nzima Costa kaondolewa kwasababu za kinidhamu ikumbukwe hakuna mchezaji mkubwa kuliko klabu.
Morata asingekuja kama Costa angekuwepo msimu huu kwasababu Madrid alikuwa mshambuliaji chaguo la pili nyuma ya Benzema inawezekana vipi aje huku tena awe chaguo la pili nyuma ya Costa?
Labda kama Conte angemuhakikishia nafasi kwa kuwatumia wote wawili.
NB:NI KWELI TUNAMISS FIGHTING SPIRIT YAKE PALE MBELE
 
Nimeona mtu anapendekeza kutumia false no. 9 Hazard. Duuuuh mnachekesha. Hivi mmecheki game ya Everton na ile ya man city baada ya morata kutoka na Willian akaingia. Hazard mda mwngi anakuja kuchukua mpira kati kupandisha mbele. Namba 9 ni muhimu hata batshuayi lakini awepo ndan. Kuna timu zna defense nzur bila no 9 ni uongo. Nafasi ya pili tunaipata lakini c ubigwa wa EPL. Kama unataka uwe bingwa unatakiwa usipoteze game zaidi ya 2 before chrismas by Conte
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom