The _Analyst
JF-Expert Member
- May 26, 2017
- 466
- 564
Mkuu kwangu mimi nimemuona Bakayoko kama usajili mzuri hata kama hajafanya sawa na mategemeo yetu mashabiki. Ila nakuhakikishia msimu ujao kila mtu atamkubali japo tunapungukiwa midfield mmoja, Alonso anahitaji msaidizi ili apate mtu wa kumsaidia, central midfield. Ampandu ajengewe uwezo maana yeye na Christensen wanatosha pale kati.Am not totally against Morata. Ila kwa sasa anahitaji ushindani na kwa kuwa Batshuayi ameshindwa kutoa hiyo changamoto ni vyema tukawatumia hawa washambuliaji wetu watatu vyema na Morata wakati anaendelea kuzoea ligi na kutafuta stamina atokee benchi wakati mabeki wameshachoka.
Akiwa fit msimu ujao wala sioni haja ya kuongeza striker. Tunahitaji tu kuboresha midfield yetu maana Fabregas muda umemtupa mkono. Mtu tunayemhitaji kucheza na Kante ni mix ya Matic na Fabregas yaani anajua defence na ni mzuri wa kushambulia.
Na huu ni mtazamo wangu.