Chelsea FC (The Blues) | Special Thread

Chelsea FC (The Blues) | Special Thread

David Luiz ameamua kumaliza utata baada ya kumfuata kocha wake huko Chelsea, Antonio Conte kumaliza bifu na kuweka hadharani matakwa yake.

Beki huyo Mbrazili amemwambia kocha huyo kwamba anataka nafasi yake kwenye kikosi cha kwanza kama itashindikana basi hatakuwa na kitu cha kuendelea kukifanya hapo Stamford Bridge, ataondoka!

Luiz na Conte wamekuwa kwenye bifu kubwa siku za karibuni ambapo Mbrazili huyo alipigwa chini kwenye kikosi cha kwanza baada ya kumkosoa kocha wake juu ya mbinu zake katika mechi ya kipigo kutoka kwa AS Roma katika Ligi ya Mabingwa Ulaya Oktoba mwaka huu. Luiz alionyesha kutofurahishwa pia wakati alipofanyiwa sub katika mechi ya nyumbani dhidi ya Wataliano hao.

Tangu sakata hilo kuibuka, Luiz sasa amekuwa gumzo akiwindwa na klabu kibao ikiwamo Real Madrid na Bayern Munich, huku kocha Jose Mourinho akimtaka pia beki huyo wa kati aende akaongeze nguvu huko Old Trafford.

Mtu wa karibu na Luiz alisema: "David ni kama mchezaji mwingine yeyote yule anataka kucheza. Hivyo kwa sasa anasubiri tu kuona nini kitatokea."
Mungu anakuona Numbisa
 
Vipi gemu la leo, tutachomoka kwa Southampton?, napendelea conte atumie mfumo wa 3-4-3, mbele wakae pedro, willian na hazard
 
Ktk vitu ambavyo mnapaswa kumuangalia Conte ni approach zake za Big game akiwa darajani na ugenini... Niseme tu kwa kifupi ni kwamba Conte anatambua nafasi yake ya kuifunga Barcelona iko darajani tu so Chelsea itacheza zaidi ya uifikiriavyo kuhakikisha inaisukuma nje Barça na wakienda camp nou hapo ndo watawekewa 3+5+2

Hapo Kati lazima umuone Kante, Drinkwater na Bakayoko. Moses na Alonso. Warahi Barça watasaza
Changia hivyo tu hapa jukwaani, ukibet vile pesa yako mhindi anakula asubuhi kabisa!
 
PG azisifia Chelsea na Spurs huku akiiponda ManU
Asema hizi mbili zinacheza mpira tena kwa mfumo watakao
b3e7fe368049e4ef7568bc10820f9008.jpg
Hapa anamchota tottenham akili kwa game yao leo
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom