Chelsea FC (The Blues) | Special Thread

Chelsea FC (The Blues) | Special Thread

Sijui kama uliitazama match kipindi cha kwanza
Hadi kipindi cha pili alipoingia wilian na zappa ndio team ilibadilika
Jitathmini kwanza kwasababu hata kauli zako zinakinzana mara useme akianza Cahill lazima tufungwe mara unabadilisha hoja hueleweki nikutakie usiku mwema.
 
Jitathmini kwanza kwasababu hata kauli zako zinakinzana mara useme akianza Cahill lazima tufungwe mara unabadilisha hoja hueleweki nikutakie usiku mwema.
Kiukweli cahill ni tatizo huwa sifichi sijawahi kumkubali
Sifa zote kwa batshuay wakati wa shida tu
 
Na Matic je siyo tatizo huko? naskia timu iliyopanda daraja imekutoa bikra *****

Punguza hasira na Belo mkuu.

Kwa kweli Belo ni man utd lakini ni kati ya mashabiki ambao kama hafanyi mzaha anatoaga mchanganuo unbiased.

Ni kweli MPAKA SASA Matic ameonesha ni bora kuliko Bakayoko. Haimaanishi Bakayoko ni mbovu. Waliomnunua Bakayoko nadhani waliangalia zaidi future kwa maana ya umri wao na potential aliyonayo Bakayoko. Huenda Matic hakutaka kugombania namba ndiyo akashinikiza kuondoka lakini wangekuwa pamoja msimu huu angemfundisha Bakayoko a thing or two.
 
Sijui kama uliitazama match kipindi cha kwanza
Hadi kipindi cha pili alipoingia wilian na zappa ndio team ilibadilika


Naelewa unachokisema. Namkubali sana Azpilicueta lakini huwa sifurahii akipangwa wing maana inapunguza nguvu yetu ya kukaba.

Kwa MTAZAMO WANGU game ya leo, Azpilicueta, Zappacosta na Pedro wangekaa upande huo wa kulia mambo yangekuwa tofauti sana.

Na kwa kukujibu kuhusu Cahill (dah leo nimemuona anavyodefend kwa kurudi nyuma..ila simpondi hahah) nadhani umeona kazi yake inavyokuwa ngumu kutokana pia na weakness ya Alonso kukaba. Anajikuta anatakiwa kukaba watu wawili - wa kwake, na huyu aliyempita Alonso). Kwa mtazamo wangu, hiyo ni nafasi ya kuanza kumjaribisha zaidi Kenedy kama atafaa au kutafuta mchezaji mwingine bora zaidi.

Kwa msimu huu, walau kwenye EPL, bado tuna kikosi cha kutosha kushinda ligi ninaamini. Ni kocha kucheza vizuri karata zake. Asiwe too defensive.
 
Mtazamo wangu juu ya mechi:

- Playing too defensive kwa kuendelea kumuweka Azpilicueta kama right wing kulisababisha tukafungwa goli mbili leo. Shida ya hii system inampunguzia nguvu ya kushambulia maana anakuwa too defensive na inampunguzia nguvu ya kudefend maana anajua kuna Rudiger nyuma yake.

- Kocha alifanya vyema kumtoa Morata maana aidha bado ana majeruhi hivyo anacheza kwa uoga ama hana nguvu bado za kuhimili mikiki ya Premier League (hapa ndipo wapenzi wa Lukaku wanapopata point kwa nini wanadhani ni bora kuliko Morata). Hata hivyo bado naamini Morata ni chaguo sahihi kama ataweza kubadilika kuendana na physical demands za game za EPL.

- Baada ya kumtoa Morata, kulibaki pengo la kati - kuzuia mipira isivuke kati na ndipo alipomtoa Alonso ambaye alikuwa anazidiwa defensively upande ule. Akamuingiza Willian ambaye Alikuja kucheza nafasi ya Pedro zaidi. Azpilicueta akaenda kushoto.

- Pedro na Willian walicheza wote kama wing back na attacking kwa kupokezana ingawa Pedro alionesha kurudi nyuma zaidi na kumuacha Willian atambae mbele. Hii iliwachanganya Watford kutokujua yupi hasa ni wing back na nani atapanda.

- Kuna moves kadhaa pia zilionesha kama Willian alikuja kati alipokuwa akicheza Fabregas kisha Fabregas akapanda juu. Yote hii iliamsha sana nguvu ya midfield na kuanzia dakika ya 70 hadi mpira unaisha, tuliweza kudominate midfield.

- Kwa kutambua kuwa Willian, Pedro na Fabregas sasa wanaingiliana nafasi na kutaka kusogeza mashambulizi mbele, akaingia Zappacosta kudhibiti ulinzi na Willian akapanda mbele nafasi ya Pedro. Na goli la nne ndivyo lilivyopatikana.

- Kwa kuangalia tu jinsi tulivyocheza dakika 25 za mwisho ni dhahiri kuwa mechi nyingi tulizonazo kocha akiweza kukpanga kikosi hikihiki chembamba vizuri tuna uwezo wa kushinda. Nadhani msimu huu kutokana na kununua wachezaji wengi wageni na kutafuta hasa wapi wanacheza kocha anajikuta anabadili kikosi mara kwa mara lakini akibahatisha chemistry nzuri bado naamini tuna kikosi kizuri sana kulinganisha na timu nyingine kwenye ligi.
 
458AE23300000578-5003497-image-a-181_1508593375067.jpg


Hawa walitusaidia sana kubadili matokeo!
 
Quna tetesi qwamba hichi qipindi cha qiangazi qocha anataqa qumtoa Batsman ..ila qazuiliwa; ni qweli waquu..??
 
458ACCB300000578-5003497-image-a-174_1508592775094.jpg


The All Season Man of the Match for Chelsea...We call him DAVE!

458ACE6E00000578-5003497-image-a-177_1508592872930.jpg


Sina lengo la kumponda Cahill, ila huyu alistahili kuwa Captain wa timu yetu..mbele ya Hazard na Luiz!
yaani goli ni tamu hadi masteward wote badala ya kuwalinda washabiki wote waligeuka kuangalia goli la azplicueta,kweli mpira unaumiza sana
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom