Mtazamo wangu juu ya mechi:
- Playing too defensive kwa kuendelea kumuweka Azpilicueta kama right wing kulisababisha tukafungwa goli mbili leo. Shida ya hii system inampunguzia nguvu ya kushambulia maana anakuwa too defensive na inampunguzia nguvu ya kudefend maana anajua kuna Rudiger nyuma yake.
- Kocha alifanya vyema kumtoa Morata maana aidha bado ana majeruhi hivyo anacheza kwa uoga ama hana nguvu bado za kuhimili mikiki ya Premier League (hapa ndipo wapenzi wa Lukaku wanapopata point kwa nini wanadhani ni bora kuliko Morata). Hata hivyo bado naamini Morata ni chaguo sahihi kama ataweza kubadilika kuendana na physical demands za game za EPL.
- Baada ya kumtoa Morata, kulibaki pengo la kati - kuzuia mipira isivuke kati na ndipo alipomtoa Alonso ambaye alikuwa anazidiwa defensively upande ule. Akamuingiza Willian ambaye Alikuja kucheza nafasi ya Pedro zaidi. Azpilicueta akaenda kushoto.
- Pedro na Willian walicheza wote kama wing back na attacking kwa kupokezana ingawa Pedro alionesha kurudi nyuma zaidi na kumuacha Willian atambae mbele. Hii iliwachanganya Watford kutokujua yupi hasa ni wing back na nani atapanda.
- Kuna moves kadhaa pia zilionesha kama Willian alikuja kati alipokuwa akicheza Fabregas kisha Fabregas akapanda juu. Yote hii iliamsha sana nguvu ya midfield na kuanzia dakika ya 70 hadi mpira unaisha, tuliweza kudominate midfield.
- Kwa kutambua kuwa Willian, Pedro na Fabregas sasa wanaingiliana nafasi na kutaka kusogeza mashambulizi mbele, akaingia Zappacosta kudhibiti ulinzi na Willian akapanda mbele nafasi ya Pedro. Na goli la nne ndivyo lilivyopatikana.
- Kwa kuangalia tu jinsi tulivyocheza dakika 25 za mwisho ni dhahiri kuwa mechi nyingi tulizonazo kocha akiweza kukpanga kikosi hikihiki chembamba vizuri tuna uwezo wa kushinda. Nadhani msimu huu kutokana na kununua wachezaji wengi wageni na kutafuta hasa wapi wanacheza kocha anajikuta anabadili kikosi mara kwa mara lakini akibahatisha chemistry nzuri bado naamini tuna kikosi kizuri sana kulinganisha na timu nyingine kwenye ligi.