Chelsea FC (The Blues) | Special Thread

Chelsea FC (The Blues) | Special Thread

We hujielewi kabisa, liver kakufunga kwako isitoshe kakuzidi point sasa unataka afanye nini kwa sasa uamini ni bora zaidi yako? yuko robo fainali ligi cup wewe ushatolewa, narudia tena liver ni timu bora kwa sasa kuliko timu yoyote epl
Endelea kuamin kuwa liver ni bora ..
Napia kufungwa na liver uwanja wa nyumbani sio jambo la ajabu sana kwan hakuna bingwa ambaye hawezi kupoteza mechi yoyote mkuu..
 
Tukija ktk swala Alonso anachofanya Conte ni kucheza na akili za watu. Kweli tunacheza mfumo Wa 3-4-3 lkn timu inapokua inashambuliwa ni kweli tunakua ktk hii back line ya wachezaji Wa 3 na ni aina gani hao ya hao wachezaji alionao ktk hii back line ya 3?

Conte mjanja sn tena sn. Anatumia uwezo Wa wachezaji binafsi kutengeneza huu mfumo na hii ndio inayowapa tabu sn timu pinzani tunapokutana nazo.

Kwa mfano Alonso ni beki Wa kushoto kwa asili lkn huyu beki amepewa Uhuru Wa kuweza kupanda mbele sn na kurudi nyuma km alivyo Moses ktk upande wake. Na pia huyu Alonso anachezeshwa huu upande km timu ikiwa inashambuliwa Basi huku nyuma kuna kua na wachezaji watano wanaosimama km mabeki akiwemo Alonso Cahill Luiz na Azp na Moses. Hii inafanya ngome ya chelsea kua ngumu sn. Na wakati huo huo huyu Azp amekua akitulia nyuma na hapandi mbele hovyo hovyo km ilivyokua zamani na ukiomuona mbele ni Mara moja moja sn sema huyu jamaa amekua huru pia kuingilia mipira ktk maeneo ya kati na kutibua mipira Mara kadhaa na ata ktk eneo LA kati pia. Kwahiyo unakuta Luiz anakua huru sn na kupunguziwa kz sn kitu ambacho Terry km anasimama hapo kati ataweza kucheza vzr tu. Na ata Ivanovic maana huu mfumo unawapunguzia baadhi ya wachezaji majukumu sn.

Bado hatujakubaliana kwa Alonso (especially kama uliona game dakika za mwanzo tukicheza na Everton).

Sanasana umenichanganyia maneno mengi halafu ukarukia point nyingine...ila poa tu. Kwa kuwa nyuma yake kuna Cahill aliyebadilika ndiyo maana hatuoni madhara sana ila kiukweli upande wake ndiyo upo weak hasa pia kwa kuwa Hazard harudi sana nyuma kukaba.
 
Endelea kuamin kuwa liver ni bora ..
Napia kufungwa na liver uwanja wa nyumbani sio jambo la ajabu sana kwan hakuna bingwa ambaye hawezi kupoteza mechi yoyote mkuu..
Mkuu sijatoa sababu moja kuonyesha liver ni bora kuliko chelsea
 
Bado hatujakubaliana kwa Alonso (especially kama uliona game dakika za mwanzo tukicheza na Everton).

Sanasana umenichanganyia maneno mengi halafu ukarukia point nyingine...ila poa tu. Kwa kuwa nyuma yake kuna Cahill aliyebadilika ndiyo maana hatuoni madhara sana ila kiukweli upande wake ndiyo upo weak hasa pia kwa kuwa Hazard harudi sana nyuma kukaba.
Mentor mi naona Chelsea haina upande ambao uko weak sema wewe unaiona tofauti kwasababu huyu Alonso sio km Moses kwasababu huyu Alonso ni beki sasa anajaribu kupandisha mipira mbele na drive kitu ambacho kinampa shida sio km Moses. Moses ktk kupandisha mipira mbele yuko vzr na pia anajituma sn ktk kukaba na uzuri ni kwamba ktk upande wake yuko Azp ambae ni mbishi na ana uwezo Wa kupandisha mipira mbele vzr tu.

Nachoweza kusema taratibu Alonso atakaa vzr tu. Na uzuri km ulivyosema huo upande Wa Cahill, Cahill katulia na hapandi mbele sn....
 
Tena ata km wakigundua watakua na kz ya kupambana na uwezo Wa mchezaji mmoja mmoja maana tunakoendea Matic au Kante mmoja wao hapo atapewa acheze na Willian. Sasa Willian akiwa kati hapo akawa ana tiririka na mipira kuja nayo mbele timu pinzani lazima ziumie.
mkuu ulikuwa wapi mbona ulipotea sana
 
mkuu ulikuwa wapi mbona ulipotea sana
Mkuu mi nipo sema last season timu yetu haikua vzr inafikia hatua unashindwa ata kucomment kitu kwasababu timu haiendi vzr.... Inabaki kua msomaji tu.
 
Tena ata km wakigundua watakua na kz ya kupambana na uwezo Wa mchezaji mmoja mmoja maana tunakoendea Matic au Kante mmoja wao hapo atapewa acheze na Willian. Sasa Willian akiwa kati hapo akawa ana tiririka na mipira kuja nayo mbele timu pinzani lazima ziumie.
ninachofurahia hii chelsea yangu ni namna hazard alivyorudi kwenye form yake ya zamani ktk kufunga magoli ufungaji wa magoli ulikuwa tatizo na hasa huyu hazard anapokuwa butu pamoja na kuwa na costa ambaye siyo mnyumbufu ambaye akikutana na beki tight anapata tabu sana kuscore unamhitaji hazard akufungulie njia jaribu kucheki goli la pili la hazard dhidi ya everton utaamini ninachosema yaani beki wakati bado inashangaa pamoja na golikipa wanashangaa mpira uko nyavuni huo ndiyo unyumbufu ninaomaanisha
 
Tena ata km wakigundua watakua na kz ya kupambana na uwezo Wa mchezaji mmoja mmoja maana tunakoendea Matic au Kante mmoja wao hapo atapewa acheze na Willian. Sasa Willian akiwa kati hapo akawa ana tiririka na mipira kuja nayo mbele timu pinzani lazima ziumie.

Kaka mi nilikuwa ni miongoni mwa waliompokea Conte kwa shingo upande sababu ya mazoea ya Mou, na zile mechi za mwanzo timu ilikuwa mbovu sana
Lakini kwa sasa kwa mfumo huu ni balaa maana Chelsea wanaonekana wako 15 Kiwanjani, kipa mmoja, mabeki saba na Foward saba, maana wale watatu wa nyuma wakishambuliwa wale wane wa kati wanakuja kuwa mabeki na wale watatu wakishambulia wanne wa kati wanakuja kuongeza idadi, kwa hiyo nyuma hakufungiki na mbele tunatupia tu kwenye nyavu,

Timu sasa imesimama, ila kocha anapaswa kuwa na sub ya ukweli kwa Victor, Kante na matic maana wakiumia au wakiwa na kadi ni balaa
 
Mkuu mi nipo sema last season timu yetu haikua vzr inafikia hatua unashindwa ata kucomment kitu kwasababu timu haiendi vzr.... Inabaki kua msomaji tu.
pole sana ni kweli unachosema hadi wakati mwingine unajuta ni kwa nini unashabikia mpira?
 
We hujielewi kabisa, liver kakufunga kwako isitoshe kakuzidi point sasa unataka afanye nini kwa sasa uamini ni bora zaidi yako? yuko robo fainali ligi cup wewe ushatolewa, narudia tena liver ni timu bora kwa sasa kuliko timu yoyote epl

We hujui mpira, maana wala hujui kwa nini Chelsea walifungwa na Liver, pia hujui pamoja na kufungwa huko kamzidi Chelsea point moja tu zingine zimeenda wapi?
 
Asante mrs. Mcharo wangu.

Hofu yangu tu ni wiki ijayo, mtaweza kuninyamazishia hao washinda gobole wa London kweli!??? Mna wiki mbili nzima za kujiandaa. Niahidini Hamutaniangusha ili niwaombee!!!
Hatutakuangusha Mcharo wangu wale wetu ni nyie na Man city safari ya kwanza tu mlituotea.....big four hatupotezi tena, Hata nyie mjiandae mkija kwetu
 
We hujielewi kabisa, liver kakufunga kwako isitoshe kakuzidi point sasa unataka afanye nini kwa sasa uamini ni bora zaidi yako? yuko robo fainali ligi cup wewe ushatolewa, narudia tena liver ni timu bora kwa sasa kuliko timu yoyote epl
Nafikir moja ya watu ambao kazi yao nikuangalia mpira lakin hawaujui wewe ni moja wapo....tuache na jukwaa letu ...
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom