Kunguru Mjanja
JF-Expert Member
- Aug 22, 2012
- 2,047
- 3,978
- Thread starter
- #33,781
Pedro na Fab wanacheza nafasi mbili tofauti, Fab anatakiwa akabe sana na kupeleka mipira mbele. Pedro yeye kwa mfumo huu ni kufunga tu kukaba ni kidogo sana. Sema Conte anamjaribisha mchezaji mara moja tu asipodeliver anaachana nae. Kumuweka Bench Batshuay inanikera sana
Sio kwamba anajaribu mara moja Mkuu, yule anakupanga ukizingua mpaka ufanye vizuri mazoezini ndo anakupanga maana anasema "uwe mdogo uwe mkubwa ukikidhi vigezo vyangu unaanza".
Kumuweka Batchuayi nje kweli inaweza ikaonekana mbaya, ila sasa shida mpinzani wake ni D. Costa ambaye ana tabia Conte anazozipenda mtu mwenye hasira ya ushindi, anaependa mpira. Pia kama umeona ikifika dk ya 80 lazima afanye sub kuingiza wachezaji wengine.