Chelsea FC (The Blues) | Special Thread

Chelsea FC (The Blues) | Special Thread

26E5BFA700000578-3006614-image-a-43_1427046482984.jpg
 
Kusema ukweli naona Chelsea ifungwe mechi zote na tusichukue kombe ili huyu Babu atimuliwe.
Huu mfumo wake wa kudefend ushagoma

Kadifendi wapi mkuu, ivi ktk hayo magoli mawili waliopata Hull City bado tu utamlaumu Jose Mourinho kwa makosa gani?
 
Afu Chelsea fans wanajipa matumaini kuwa watachukua kombe. Kwa huu mchezo hatufiki popote pale.
Stoke, Liver, Arsenal, United ,QPR ni mechi ngumu sana


Tunapenda kucheza michezo migumu na kuonesha ubora wetu kua sisi ni bora na tumedhamiria kua mabingwa huo ndio ukweli...BTW magoli yote ya Hull City yalikua ni zawadi kutoka kwa wachezaji wa chelsea....
 
Tumepata point tatu muhimu sana japo mechi ilionekana ngumu kiasi

bado Blues kuna yumba kidogo kwenye ulinzi, Chelsea haina historia ya kufungwa fungwa magoli ya hovyo namna hii, hope Mou na wachezaji wake wameona hizo weaknesses na watazifanyia kazi kwa mechi tisa zilizobaki

Hongereni wana Blues wote


Mkuu Kituko habari za masiku kaka?

Chelsea walifanya marekebisho ya makosa ya ktk mechi hiyohiyo ya jana, unaweza kuniambia Hull City walitushambulia wapi tena ukiondoa zile shuti tatu mfululizo alizookoa kipa wetu? Kwa kifupi magoli waliopata Hull City wachezaji wa chelsea walifanya makosa wao na ndio maana ata Mou kabla ya ngwe ya kwanza kuisha aliinuka na kutangulia ndali....hakupendezwa na upuuzi wa wachezaji wake....sasa kipindi cha pili waliporudi nafikiri wewe mwenyewe uliwaona hao chelsea.
 
Last edited by a moderator:
Hongereni sana humu akina Ntuzu, kalou, Mentor na wengineo wote wa jukwaa hili kwa ushindi mnono.

Asante sn kaka BAK ingawa wachezaji wetu walitaka kukitia kitumbua mchanga lol.....

Nashukuru pia kwa picha mkuu BAK.....

Today he had a bad day...


Hakufanya makosa peke yake mkuu...goli la kwanza kulikua na Willian na Iva wote hao wawili wakakubali kupigwa chenga na mchezaji akadrive kuingia ndani kina Terry nao kati wakafanya makosa pia goli la pili kipa hakua makini ktk kudrible mpira pamoja kua Iva alimrudishia kipa ata km adui alikua karibu kwanini asidribla kuelekea pembeni ya goli upande wa kulia na akacheza kuupeleka mpira katikati na kufungwa?

Hongereni kwa ushindi....ni heri Rentboys wachukue EPL, lakini si Goons ama Shitty...

Nzi asante sn mkuu Hongereni sn na nyie kwa kuwafunga wale jamaa wenye roho mbaya....
 
Last edited by a moderator:
  • Thanks
Reactions: BAK
Mkuu Kituko habari za masiku kaka?

Chelsea walifanya marekebisho ya makosa ya ktk mechi hiyohiyo ya jana, unaweza kuniambia Hull City walitushambulia wapi tena ukiondoa zile shuti tatu mfululizo alizookoa kipa wetu? Kwa kifupi magoli waliopata Hull City wachezaji wa chelsea walifanya makosa wao na ndio maana ata Mou kabla ya ngwe ya kwanza kuisha aliinuka na kutangulia ndali....hakupendezwa na upuuzi wa wachezaji wake....sasa kipindi cha pili waliporudi nafikiri wewe mwenyewe uliwaona hao chelsea.

Nipo Mkuu Ntuzu,

ni kweli half ya kwanza tulifanya makosa ambayo ni adimu sana kufanyika kwenye timu ikiwa chini ya MOU, hayo makosa ya ulinzi naona yanendelea tangu ile siku na PSG tulipofungwa magoli ya vichwa huku wafungaji wakiwa hawajakabwa kabisa, kwenye kona tatu vilipgwa vichwa vitatu na viwili vikawa ni goli, Mechi ya So'ton pia kuna kauzembe ka kujilinda tena kalifanyika

all in all tumeshinda na kweli timu ilibadirika kipindi cha pili, lakini ilikuwa ni risk kubwa kuwaachia Hull warudishe hizo goli mbili
 
Last edited by a moderator:
Mkuu BAK asante kwa picha. Mimi nilirudi kwangu half time sikuendelea kuangalia game. I was so mad at those kids yani...that was a game to kill...reminded me of Bradford
 
Last edited by a moderator:
Mkuu nakubaliana na wewe lkn binafsi nasema wazi kabisa kua mchezo wa jana ilikua lazima tushinde kwa hali yoyote ile hii inatokana na kwamba sasa tunashikilia ile nafasi ya kuchukua ubingwa na kamwe hatutakiwi kufanya makosa km tuliofanya kwa PSG na Soton lkn hayo magoli waliopata Hull ni maksoa ya wacheza wa chelsea wao uwanjani...na wanapaswa kulaumiwa ktk hilo kwa kuwazawadia hull magoli mawili tena kwa harakaraka na kufanya mchezo kua mgumu....Hull walikua hawawezi kutengeneza move za kuzaa magoli zaidi ya mbili au tatu hivi walizotengeneza na kipa wetu akokoa hiyo ndio ilikua mpira amabayo waliweza kuipitisha lkn zaidi ya hapo chelsea iliwashika Hull na ndio maana tukashinda....

Mi tayari nimeshaanza kusheherekea ubingwa mkuuu

Nipo Mkuu Ntuzu,

ni kweli half ya kwanza tulifanya makosa ambayo ni adimu sana kufanyika kwenye timu ikiwa chini ya MOU, hayo makosa ya ulinzi naona yanendelea tangu ile siku na PSG tulipofungwa magoli ya vichwa huku wafungaji wakiwa hawajakabwa kabisa, kwenye kona tatu vilipgwa vichwa vitatu na viwili vikawa ni goli, Mechi ya So'ton pia kuna kauzembe ka kujilinda tena kalifanyika

all in all tumeshinda na kweli timu ilibadirika kipindi cha pili, lakini ilikuwa ni risk kubwa kuwaachia Hull warudishe hizo goli mbili
 
Last edited by a moderator:
Ubingwa kwa tmu gan wakat beki yenu inamababu weng na kuna uwezekano wa kupoteza point zaid y Tisa SSA ubingwa mnatoa wapi😀
 
Yaani wapenzi na washabiki wenzangu wa chelsea hii ni game ya nne na mimi sioni sababu hasa ya kupata ushindi kiduchu ni dalili kwamba mda wowote hili kombe tunalikosa na itakuwa aibu kubwa kwetu kukaa juu msimu mzima halafu tunaondolewa kileleni dakika za mwisho tena kizembe zembe . Wakati timu nyingine zinarudi kwenye fomu game hizi za mwisho wao chelsea wanapoteana wanacheza mpira below standard na hii ni risk kwetu . FABRIGAS amekuwa mzigo na mwenzake osca ipo haja ya kusajiri viungo wengine wenye majina na beki na mshambuliaji . hata tukipata viungo kama modrich, reus, khedira , kroos au de brune sio mbaya kwenye nafasi ya ushambuliaji tuongeze mmoja kama cavani au laccazett drogba aondoke .na beki mmoja kama varane au venatia . Lakini vinginevyo kwa kikosi hiki mwakani tusitegemee lolote na hata msimu huu sina uhakika sana na huu ubibgwa mda na saa yoyote tunanyanganywa ubingwa
 
Ubingwa kwa tmu gan wakat beki yenu inamababu weng na kuna uwezekano wa kupoteza point zaid y Tisa SSA ubingwa mnatoa wapi😀

Hiyo timu yako yenye beki vijana ishapigwa goli ngapi msimu huu?
 
Kuna mechi nyingine zinastahili pole tu,iwe mmeshinda au mmefungwa.Poleni kwa ushindi wa jana.cc Ntuzu
 
Last edited by a moderator:
Kuna mechi nyingine zinastahili pole tu,iwe mmeshinda au mmefungwa.Poleni kwa ushindi wa jana.cc Ntuzu



juve2012 asante Sn Mkuu. Ngoma ilitaka Kuchanika jana lol......


Anyway. Kuna makosa Wachezaji wamekua Wanafanya na Yanafanyiwa Kz mkuu.
 
Last edited by a moderator:
HADI SASA NINACHOKIONA HAPA KWA BAADHI YA MASHABIKI WENGI WA CHELSEA, WAMEKUBALI KUSHIKWA MASIKIO NA KUAMINI MANENO YA WAPINZANI WETU NA KUAMINI KABISA KWAMBA 'ETI KOMBE SIO LA CHELSEA!!!!!' HUU NI ZAIDI YA UPUMBAVU NA UJINGA. JIULIZENI KAMA HAO WAPINZANI WANGESHIKA NAFASI YETU NA WANGEKUWA NA NGUVU KAMA YA TIMU YETU CHELSEA FC, INGEKUWAJE??? NI WAZI KABISA KWAMBA CHELSEA FC NI TIMU PEKEE YENYE NGUVU KUBWA EPL KULIKO TIMU ZOTE, SASA KAMA NI HIVYO KWANINI MUOGOPE HOVYO HOVYO BILA KUTUMIA AKILI ZENU NA KUKUBALI KUSHIKWA MASIKIO NA HAO MALOOOSERZZZ:A S-cry:. NI AIBU SANA KUONA KAMANDA MZIMA WA CHAMA KUBWA KAMA CHELSEA UNATAMKA WAZI WAZI KAULI ZA KIUWOGA-WOGA KUWA CHELSEA HAITAPATA UBINGWA. ACHENI HUU UPUUZI CHELSEA IPO CHINI YA MTU MAKINI SANA 'MOURINHO' NA LAZIMA TUFANYE SHEREHE YA UBINGWA WA EPL. TENA HILI SIJAOLIONA HAPA TU BALI HATA HUKO MAJUU MISHABIKI WENZETU INAYOTUWAKILISHA PALE IMEKUWA KAMA MAZOBA:A S confused:, HASA KWENYE MECHI KUBWA HUWA HAWASHANGILII IPASAVYO MWANZO MWISHO ILA HUWA WANAPENDA KWENDA NA MATUKIO MAZURI YANAYOFANYWA NA WACHEZAJI WETU TU. HII NI HATARI SANA NA NDIO MAANA WAPINZANI WANAPATA NAFASI KUWAVURUGA WACHEZAJI WETU WAWAPO UWANJANI. TUIGE TIMU KAMA JUVE NA NYINGINEZO HUWA WANATUMIA VIZURI UWANJA KWA KUSHANGILIA MUDA WOTE WAWAPO UWANJANI ILI KUWAPA NGUVU WACHEZAJI WAO LAKINI UKIRUDI KWETU UTAFIKIRI TUMEKULA GUNDI:shut-mouth:. KWA MTAZAMO WA HARAKA NI KWAMBA TIMU IPO TAYARI KWA UBINGWA LAKINI MASHABI NA WAPENZI HAWAPO TAYARI KWA MATAJI NA HATUNA HABARI:lalala::whistle: KABISA NA MASUALA HAYO. DIZAINI KAMA TUMEROGWA VILE:A S-confused1: NA WAPINZANI. ILA NATAKA KUWAHAKIKISHIA KOMBE LA EPL NI LA CHELSEA FC TU.:wink2:
 
Hongereni sana kwa point 3 muhimu sana,mengine yaachwe tu kama yalivyo. Ntuzu niliwaambia mdharau mwiba ...
lakini Mungu mkubwa maombi yangu yalikuwa nanyi daima hata ile dakika ya mwisho.

Cc Viol Mentor kalou
 
Last edited by a moderator:
binafsi nadhani tuko pazurina tuko vizuri. ushindi ni ushindi tu hata kama tumeuhangaikia.

in any case tusisahau pia kuwa kila timu tutakayocheza nayo lazima itakamia kuliko kawaida. so tukifanikiwa kushinda tusisikitike sana.

bado hizi mechi ni ngumu sana. hatuko vibaya kabisa ndugu zanguni. na wala hatuna haja ya kujaa pressure, ingawa pia hatuhitaji kubweteka kama Liverpool this time last season mpaka kombe likawatoka. tukaze buti, tujue tunahitaji point 3 kila game hata kama tutashinda kwa tofauti ya goli moja, huo ni ushindi tayari!!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom