Chelsea FC (The Blues) | Special Thread

Chelsea FC (The Blues) | Special Thread

hii game itakuwa ngumu sana ... au unaweza shangaa ikawa nyepesi sana. it all depends on the perfection ya strategy za kila timu. nakumbuka mwaka uleeee, chelsea ilimpiga Barcelona (ya akina Ronaldinho) bao 3 ndani ya dkk 15 za kwanza...enzi za akina Damien Dunn, Arjen Robben na wengineo chini ya huyu huyu Maurinho. Nna gut feelings kuwa Maurinho atataka kuirudia ile strategy ya kupata mabao walau mawili ndani ya 30 minutes za mchezo wa kasi sana ili kuwatibua PSG. na kwa kasi hiyo nadhani atahitajika kucheza 4 - 3 - 3 au 4 - 1 - 2 - 2 -1 wakiwemo Hazard, Willian na Ramires ili waweze kukimbiza sana. of course Costa atakuwa kule mbele kabisa. kwa mawazo yangu timu itakayoanza kwa formation zote hizo mbili itakuwa:

golini: Courtois (urefu wake ni advantage against urefu wa Ibra

Mabeki wanne ni:

1. Ivanovic
2. Azp
3. Zouma (nguvu na kasi ili amdhibiti Ibra)
4. Terry

Midfield mkabaki libero mbele ya mabeki

1. Matic (atakuwa pekee immediately mbele ya mabeki kuzuia buoyancy ya midfield ya PSG

Midfield wakabaji na watawanyaji mipira:

2 midfields:

Faby na

Ramires watakuwa katikati ya dimba (mbele ya Matic) ili kutawanya mipira kushoto na kulia kwa attacking midfields wakimbizaji yani

2. attackers: Hazard na Willian

1. Stricker wa mwisho, Costa.

kwa formation hii ambayo itakuwa ikibadilika kuwa 4-3-3 kwa Ramires kuongezeka kwenye kukimbiza huku Fabrigas akisogea mbele kukaribia D ya PSG tutakapokuwa tunashambulia itamfanya Ramires aweze kupanda na kushuka kwa kasi na mapafu yake ya mbwa.

sitegemei mchezo kuanza kwa taratibu au sisi kupack basi tukisubiri counter attacks. nategemea kuwarudisha nyuma PSG ili akina Cavani warudi kusaidia ulinzi. defensively tukishambuliwa tutaanza kukaba tokea kwenye 18 ya PSG. Hazard na Willian na hata Costa wataanza kukaba immediately tukipoteza mpira. na kama willian atakuwa akikaba akiwa kwenye position ya 18 ya PSG upande wa kulia, basi tegemea Hazard atakuwa ameanza kushuka kurudi kwa Azp upande wa kushoto, same as Fab. hii itaongeza watu 2 mpaka 3 katikati ya uwanja in addition to uwepo wa Ramires na Matic. hivyo tukishambuliwa tayari tutakuwa kwenye 4 - 5 - 2 mode immediatey ili kupunguza nguvu za midfield ya PSG kupeleka mipira pembeni au kukata chenga. tutakuwa makini sana na set pieces manake uwepo wa Ibra na Cavani hewani unaweza sumbua.

Binafsi nadhani tutafurahi kuwa mashabiki wa Chelsea kesho manake level ya elevation ya uchezaji itakuwa juu sana. nadhani baada ya kesho ndipo ubingwa utakuwa de facto stamped kwetu kwa kiwango cha juu sana cha uchezaji na precision tutakachokionesha. nawaonea raha na gere mashabiki watakaokuwa uwanjani, manake viti havitakalika kwa sehemu kubwa sana ya mchezo wa kesho!!! na Mungu atubariki Chelsea kesho!!
 
Manumbu yani nimejikuta nafurahi tu kwa kusoma post yako iliyojaa uchambuzi mzuri na vionjo vya manjonjo mengi na furaha ya ushindi hapo kesho.

Naikumbuka vzr ile game yetu pale darajani na Fc barcelona, wakati huo barc walikua kwenye kiwango cha juu sn kwa ulaya 'unstopable team' chini ya kocha wao raia wa Uholanzi Frenky Rijkard. nakumbuka tulitoka Camp Nou tukiwa tumelala kwa goli 2 kwa 1 na Barc walitushinda baada ya Big man wetu DD kutolewa kwa kadi nyekundu kwa makusudi maamuzi yalifanya huyo refa na kupokea vitisho sn va kuuwawa na kuamua kuachana kabisa na kz ya uamuzi wa mipira. na mchezo uliofata hapo darajani mwamuzi alitundika kipenga chake kabatini babu Upara Corina akaombwa na Special One kkupuliza kipenga huo mchezo.

Nakumbuka magoli yalipatikana kwa haraka sn, Kina Duff,Edu Gudjenson, Joe Colly walifanya kz sn huku Barc wakipata kigoli kimoja kilichopatikana kwa mkwaju wa penati baada ya Recardo Calvalo kuupangusa mpira kichwani ulikokua unatua kichwani mwa Samuel Eto'o. Na baadae Terry kuzima ndoto za Barc kwa kichwa safi baada ya kona safi iliyopigwa na Lampard.

Ni kweli mkuu tunahitaji kucheza mpira wa kasi sn kesho ili kuwachanganya kabisa hawa PSG kila idara...maana km tutaanza taratibu tutawafanya wajiamini sn kuwapa uwezo wa kutushambulia.

Mkuu tunahitaji mawazo mbadala kutoka kwa wadau mbalimbali ngoja tuone watakapokuja tuone wanasema nini.
 
Last edited by a moderator:
Mkuu mi nimekualika utoa maoni yako yoyote yale kwa uhuru kabisa ndio maana nimekuita. Lkn km isingelikua hivo ningewaita mashabiki wa chelsea tu maana nawafahamu vzr. Lkn kwasababu tunahitaji mawazo kutoka pande zingine au kwa wakosoaji wetu ndio maana nikakuita....

Nikuombe tena km utapenda ulete utoe maoni yako......

Umeangalia mechi ya jana Arsenal vs Man (dis)United. Ingawaje haikuwa na mvuto sana kimpira nilivyouona mimi lakini matokea yalienda kwa timu pinzani.
Umechambua vya kutosha kuhusu vikosi vya Chelsea na PSG kuwa havina majeruhi. Mmeshamwadhibu PSG mara kadhaa kwa hiyo tegemeeni kuwa PSG anakuja kwenu akiwa kama faru/ kiboko/nyati aliyejeruhiwa.

Chelsea atacheza kwa tahadhari sana ili kuepusha PSG asifunge bao la ugenini. Kama ilivyo kawaida ya Mou atatumia ku-pack basi lake ili hilo lisitokee.

Mechi itakuwa na msisimko kuliko ile ya Arsenal na Man. United jana.

Kwa maoni yangu naona Chelsea atapigwa mtama leo. Kwa hiyo wacha nikupe "pole" kabisa. Nikirudi hapa ni kwa kumsalimia Kalou tu na kumwomba aniazime ile kamusi ya "maneno nzito nzito"
 
Ntuzu ahsante kwa mualiko
Naona wewe na Mentor mnapendekeza a more defensive approach Vs PSG, wakati kalou anataka muende all guns blazing, kila la kheri
Nimemuelewa sana Manumbu na nadhani approach yake iko well balanced, kama mkicheza kwa formation ya 4-1-2-3, golini 'Kotwaa' 4 (JT, Zouma, Azplicueta, Brana) - 1 (Matic) - 2 (Ramires & Fabregas) - 3 (Hazard, Costa, Willian)
Ni game ya akili mingi sana, ukishambulia sana na kuacha mlango wazi utafungwa, mkipark bus mtaalika mashambulizi mengi na kuongeza chances za kufungwa, busara ni kucheza a balanced game.
Match itaamuliwa kwenye midfield, mkiwaacha Motta, Matuidi na dogo Veratti wacheze kwa uhuru then mtaaga mashindano, mkiweza kuwacontain hawa then hamtapata usumbufu wa Ibra na Cavani.
Lakini pia ni muhimu kwa Zouma kuanza badala ya Cahill, bwana Cahill alishindwa kabisa kumdhibiti Ibra kwenye game 1 na hata goal la kusawazisha lilitokana na makosa yake, Zouma ana wajua vizuri PSG, ana nguvu na mwepesi kuliko Cahill

PSG wameshuka kiwango kidogo tofauti na msimu uliopita, lakini kwa kiasi kikubwa ni team ileile, wakati Chelsea imeimprove tofauti na msimu jana, the game is yours to lose.
 
Nonda umeona sasa, umetoa uchambuzi mzuri amabao ata mimi nimependa.....nachukua nafasi hii kuipokea hiyo pole ila nikukumbushe tu pole siku zote hutolewa na chochote pia.

Asante sn mkuu.
 
Ntuzu ahsante kwa mualiko
Naona wewe na Mentor mnapendekeza a more defensive approach Vs PSG, wakati kalou anataka muende all guns blazing, kila la kheri
Nimemuelewa sana Manumbu na nadhani approach yake iko well balanced, kama mkicheza kwa formation ya 4-1-2-3, golini 'Kotwaa' 4 (JT, Zouma, Azplicueta, Brana) - 1 (Matic) - 2 (Ramires & Fabregas) - 3 (Hazard, Costa, Willian)
Ni game ya akili mingi sana, ukishambulia sana na kuacha mlango wazi utafungwa, mkipark bus mtaalika mashambulizi mengi na kuongeza chances za kufungwa, busara ni kucheza a balanced game.
Match itaamuliwa kwenye midfield, mkiwaacha Motta, Matuidi na dogo Veratti wacheze kwa uhuru then mtaaga mashindano, mkiweza kuwacontain hawa then hamtapata usumbufu wa Ibra na Cavani.
Lakini pia ni muhimu kwa Zouma kuanza badala ya Cahill, bwana Cahill alishindwa kabisa kumdhibiti Ibra kwenye game 1 na hata goal la kusawazisha lilitokana na makosa yake, Zouma ana wajua vizuri PSG, ana nguvu na mwepesi kuliko Cahill

PSG wameshuka kiwango kidogo tofauti na msimu uliopita, lakini kwa kiasi kikubwa ni team ileile, wakati Chelsea imeimprove tofauti na msimu jana, the game is yours to lose.

Asante sn mkuu,

Unaonaje uwezo wa makocha sasa ktk upande wa mbinu, kwamba Laurant Blanc anaweza akawa bingwa wa mbinu ktk huo mchezo au bwana Happy One ndo atakua kidedea ktk huo upande? Au tunaweza kusema Buruda Ancelotti km angekua bado yupo PSG ndo angeweza kumsumbua Mou?
 
Last edited by a moderator:
Umeangalia mechi ya jana Arsenal vs Man (dis)United. Ingawaje haikuwa na mvuto sana kimpira nilivyouona mimi lakini matokea yalienda kwa timu pinzani.
Umechambua vya kutosha kuhusu vikosi vya Chelsea na PSG kuwa havina majeruhi. Mmeshamwadhibu PSG mara kadhaa kwa hiyo tegemeeni kuwa PSG anakuja kwenu akiwa kama faru/ kiboko/nyati aliyejeruhiwa.

Chelsea atacheza kwa tahadhari sana ili kuepusha PSG asifunge bao la ugenini. Kama ilivyo kawaida ya Mou atatumia ku-pack basi lake ili hilo lisitokee.

Mechi itakuwa na msisimko kuliko ile ya Arsenal na Man. United jana.

Kwa maoni yangu naona Chelsea atapigwa mtama leo. Kwa hiyo wacha nikupe "pole" kabisa. Nikirudi hapa ni kwa kumsalimia Kalou tu na kumwomba aniazime ile kamusi ya "maneno nzito nzito"

kumbe una akili hata ya kuchambua soka!' ......... ulisemaga chelsea ni timu ya divers!'

Grand PA
 
Binafsi Nonda kanifurahisha sn, na nimatumaini yangu tutapata uchambuzi mzuri sn toka kwake.
 
Asante sn mkuu,

Unaonaje uwezo wa makocha sasa ktk upande wa mbinu, kwamba Laurant Blanc anaweza akawa bingwa wa mbinu ktk huo mchezo au bwana Happy One ndo atakua kidedea ktk huo upande? Au tunaweza kusema Buruda Ancelotti km angekua bado yupo PSG ndo angeweza kumsumbua Mou?

Hakuna ubishi Jose Mourinho ni master tactician, bwana Laurent Blanc bado mchanga sana kwa JM. Lakini LB ana kikosi imara zaidi kilichokaa pamoja kwa muda mrefu na wachezaji wengi ni matured.
Kama JM ataachwa achezeshe team namna anavyotaka yeye na si namna vibosile wa Chelsea wanavyotaka, simuoni Blanc akimsumbua JM, lakini kwa sababu ana pressure za Club kucheza a more expansive and attractive brand of football (unfamiliar territory for Jose) match inaweza kuamuliwa na discipline ya wachezaji uwanjani katika kujituma na kufuata maelekezo ya kocha
 
kumbe una akili hata ya kuchambua soka!' ......... ulisemaga chelsea ni timu ya divers!'

Grand PA
Siwezi kusema nnazo akili au nnazo akili za kuchambua soka. Hilo ni juu ya yako kuamua. Kusema kuwa Chelsea ni timu ya rugby/mieleka na divers ni kutokana na replays za fouls na jinsi ambavyo wachezaji wa Chelsea huwa wanawabamiza wachezaji wa timu pinzani.
Kwa hiyo, mnao wachezaji ambao wanadive...kama uliangalia mechi FA cup baina ya Man United na Arsenal umeona wazi kuwa kwa nyakati tofauti, at least, twice, Di Maria, Rooney na kijana mmoja walitaka kum-fool mwamuzi kwa dives.

Kwa mtu anaependa kuona mpira mpira, sio vita au faking playing football..inaudhi kuangalia mechi zinazotawaliwa na ujanja wa kijinga kama kufanya substitutions mbili za wachezaji kama Chelsea walifanya katika mechi moja ya EPL hivi karibuni ili kuua muda tu dakika za mwisho ili kuhakikisha anaondoka na points. Kwa mtu kama wewe utaona ni sawa , unataka timu yako ishinde ikicheza mpira au ikicheza mieleka, iki-pack basi, ikicheza boring game.

Inapotokea wewe kupenda nnapoandika yanayosikikana kwa ladha masikio yako yanapenda kusikia, uwe na uvumilivu nnapoandika yanayoudhi macho yako na yanaleta hisia ya mzuka katika kichwa chako.

Diversity ya mawazo, michango ndio inayoleta "utani wa simba na yanga" kimpira.

Bahati mbaya, Nonda si mpenzi wala shabiki wa Simba au Yanga ..hapo unapata tabu kunielewa.
Mimi ni mpenzi wa mpira, kandanda, kabumbu, kitale, soka....sijipi nafasi ya kujiudhi au kusononeka kwa kujifunga na timu fulani.

Kapime pressure kabisa ili uweze kuangalia game ya kesho kwa raha.
 
“No. If somebody puts on the table €250,000 to win a certain match it’s nice but I think professionalism goes beyond that. Don’t take this the wrong way but, for me, what’s more important is the happiness and pride of success, more than the money.
“Football is about our passion for the game, the happiness and the pride of victories. They have no price.”
 
Mourinho noma sana, jamaa ana akili nyingi.
 
hii game itakuwa ngumu sana ... au unaweza shangaa ikawa nyepesi sana. it all depends on the perfection ya strategy za kila timu. nakumbuka mwaka uleeee, chelsea ilimpiga Barcelona (ya akina Ronaldinho) bao 3 ndani ya dkk 15 za kwanza...enzi za akina Damien Dunn, Arjen Robben na wengineo chini ya huyu huyu Maurinho. Nna gut feelings kuwa Maurinho atataka kuirudia ile strategy ya kupata mabao walau mawili ndani ya 30 minutes za mchezo wa kasi sana ili kuwatibua PSG. na kwa kasi hiyo nadhani atahitajika kucheza 4 - 3 - 3 au 4 - 1 - 2 - 2 -1 wakiwemo Hazard, Willian na Ramires ili waweze kukimbiza sana. of course Costa atakuwa kule mbele kabisa. kwa mawazo yangu timu itakayoanza kwa formation zote hizo mbili itakuwa:

golini: Courtois (urefu wake ni advantage against urefu wa Ibra

Mabeki wanne ni:

1. Ivanovic
2. Azp
3. Zouma (nguvu na kasi ili amdhibiti Ibra)
4. Terry

Midfield mkabaki libero mbele ya mabeki

1. Matic (atakuwa pekee immediately mbele ya mabeki kuzuia buoyancy ya midfield ya PSG

Midfield wakabaji na watawanyaji mipira:

2 midfields:

Faby na

Ramires watakuwa katikati ya dimba (mbele ya Matic) ili kutawanya mipira kushoto na kulia kwa attacking midfields wakimbizaji yani

2. attackers: Hazard na Willian

1. Stricker wa mwisho, Costa.

kwa formation hii ambayo itakuwa ikibadilika kuwa 4-3-3 kwa Ramires kuongezeka kwenye kukimbiza huku Fabrigas akisogea mbele kukaribia D ya PSG tutakapokuwa tunashambulia itamfanya Ramires aweze kupanda na kushuka kwa kasi na mapafu yake ya mbwa.

sitegemei mchezo kuanza kwa taratibu au sisi kupack basi tukisubiri counter attacks. nategemea kuwarudisha nyuma PSG ili akina Cavani warudi kusaidia ulinzi. defensively tukishambuliwa tutaanza kukaba tokea kwenye 18 ya PSG. Hazard na Willian na hata Costa wataanza kukaba immediately tukipoteza mpira. na kama willian atakuwa akikaba akiwa kwenye position ya 18 ya PSG upande wa kulia, basi tegemea Hazard atakuwa ameanza kushuka kurudi kwa Azp upande wa kushoto, same as Fab. hii itaongeza watu 2 mpaka 3 katikati ya uwanja in addition to uwepo wa Ramires na Matic. hivyo tukishambuliwa tayari tutakuwa kwenye 4 - 5 - 2 mode immediatey ili kupunguza nguvu za midfield ya PSG kupeleka mipira pembeni au kukata chenga. tutakuwa makini sana na set pieces manake uwepo wa Ibra na Cavani hewani unaweza sumbua.

Binafsi nadhani tutafurahi kuwa mashabiki wa Chelsea kesho manake level ya elevation ya uchezaji itakuwa juu sana. nadhani baada ya kesho ndipo ubingwa utakuwa de facto stamped kwetu kwa kiwango cha juu sana cha uchezaji na precision tutakachokionesha. nawaonea raha na gere mashabiki watakaokuwa uwanjani, manake viti havitakalika kwa sehemu kubwa sana ya mchezo wa kesho!!! na Mungu atubariki Chelsea kesho!!
Asante sana manumbu
 
"We have tougher games than PSG in training " Mourinho said.

Wakuu nimekuwa naitafakari hii kauli ya Mourinho nabaki nacheka Tu. Huyu jamaa amewashusha kiasi gani hawa PSG? Au lengo lake ni nini hasa? Au kuna vitu gani kawaelekeza hawa vijana wake?

Cc Mentor Manumbu Mourinho kalou Nonda etc

Kwa upande wangu Hakuna chochote mpendwa ila ni power of speech, maneno yana nguvu sana na yanabadilisha mambo,halafu ukiwa unashindana na adui yako ambaye naye anakuhofia kiasi fulani ukimwambia maneno ya kumshusha sometime huwa yana muondolea confidence na kumpoteza uelekeo kabisa, hii ndo siri ya Mo anajua nguvu ya maneno....... Na kiukweli inamsaidia sana.
 
Last edited by a moderator:
Mamito unataka kuniambia ni mikwara Tu ya Mou na hakuna lilote? Au ni kweli yawezekana Chelsea wametrain an kiasi kwamba mchezo wa Leo utakua ni rahisi kwao?

Kwa upande wangu Hakuna chochote mpendwa ila ni power of speech, maneno yana nguvu sana na yanabadilisha mambo,halafu ukiwa unashindana na adui yako ambaye naye anakuhofia kiasi fulani ukimwambia maneno ya kumshusha sometime huwa yana muondolea confidence na kumpoteza uelekeo kabisa, hii ndo siri ya Mo anajua nguvu ya maneno....... Na kiukweli inamsaidia sana.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom