Kaka
RRONDO, acha kuleta Habari za kishabiki bila kuwa na data, Nimeshakuonya mara nyingi humu, unajishushia hadhi yako kaka, Hiyo kauli yako kusema Timu zote ni mbovu ni Uongo Mkubwa, usiniaminishe kuwa MAN U wote ndio Mlivyo
Kinachotokea sasa ni mabadiriko makubwa ndani ya CHELSEA, Wakati nyie (MAn U, Man City, Arsenal na Liver) bado mko kwenye dunia ileile ya Kawaida CHELSEA YUpo kwenye Sayari Nyingine Kabisa. Hivyo Viwango vyenu bado viko palepale kwa kawaida, ila Chelsea ndio wamebadirika Sana sana sana,
sasa Mnapojaribu kujiringanisha na CHELSEA mnajiona kuwa mmeshuka kiwango BIG NO, Kiwango chenu kipo vilevile ila BLUES ndio wamepanda Sabini mara Saba
Hebu angalia table ya msimu wa mwaka jana 2013-2014 kwenye mwezi wa November kama huu
1
. Arsenal P13 Pts 31
2.
Liverpool P12 Pts 24
3. Chelsea P12 Pts 24
4. Everton P13 Pts 24
5.New Castle P13 Pts 23
6. Man City P12 Pts 22
7. Soton P12 Pts 22
8. Man U P12 Pts 21
Kwa Msimu huu mpaka sasa msimamo huko hivi
1.
Chelsea P12 Pts 322. Soton P11 Pts 25
3.
Man City P12 Pts 24
4.
Man U P12 Pts 19
5. New Castle P12 Pts 19
6. Westham P12 Pts 18
7. Swansea P12 Pts 18
8. Arsenal P12 Pts 17
Ukiangalia Vizuri Points za Man City na Man U kwa mwezi wa November Msimu uliopita (2013-2014) ni sawa kabisa na Point za msimu huu (2014-2015) za mwezi ule ule wa November, sasa sijuhi kwa nini unasema kiwango cha mwaka huu cha NYIE wapinzani ni kibovu? UKWELI NI KWAMBA WAKATI BADO MPO LEVEL ILEILE YA MSIMU ULIOPITA,
maana msimu ulipita wakati kama huu CHELSEA alikuwa na points 24 tu sawa na NYIE, Leo ChELSEA kawaacha hapo hapo
Ndio hali halisi bwana
RRONDO, tulia dawa inaingia polepole, Japo inauma lakini ndio Dawa
CC:
Mentor,
agosti 8,
Tony Gwanco,
Ntuzu,
Manumbu