Chatanda azua tena mvutano CCM, Chadema Arusha

Chatanda azua tena mvutano CCM, Chadema Arusha

Kutokana na Makamba na Chatanda kufanikiwa kuonesha dunia hali halisi ya ccm kuhusu uozo wake, na umahiri wa chadema, kwa matamshi yao mbalimbali, kuna uwezekano mkubwa uongozi wa cdm kuwazawadia tuzo ya mwaka, ya wanasiasa bora.

Nashauri wanajf muwarahisishie viongozi wa cdm kazi ya kuorodhesha kauli murua za Makamba na M. Chatanda. Ya kwanza labda ni ile aliyotoa wakati wa mchakato wa kura ya maoni kuwa "kila mgombea wa ccm ametoa rushwa, tofauti ni kiwango tu." Endelea na listi tafadhali.
 
I think it's better to tell that the difference between stupidity and genius is that genius has its limits.
Makamba and company should understand this.
 
Kutokana na Makamba na Chatanda kufanikiwa kuonesha dunia hali halisi ya ccm kuhusu uozo wake, na umahiri wa chadema, kwa matamshi yao mbalimbali, kuna uwezekano mkubwa uongozi wa cdm kuwazawadia tuzo ya mwaka, ya wanasiasa bora.

Nashauri wanajf muwarahisishie viongozi wa cdm kazi ya kuorodhesha kauli murua za Makamba na M. Chatanda. Ya kwanza labda ni ile aliyotoa wakati wa mchakato wa kura ya maoni kuwa "kila mgombea wa ccm ametoa rushwa, tofauti ni kiwango tu." Endelea na listi tafadhali.

Iran, Pakistan na Afghanistan Watapokea Ushujaa wa CCM. Chadema Itapokelewa na Dunia Nzima...
 
Katibu wa CCM agoma kuomba radhi maaskofu Tuesday, 11 January 2011 20:43

Mussa Juma, Arusha

KATIBU wa CCM Mkoa wa Arusha, Mary Chatanda, amesema anaheshimu maoni ya aliyekuwa Makamu Mwenyeki wa CCM, John Malecela, lakini anaamini alichokisema kuhusu maaskofu kuvua majoho kama wanataka kuingilia siasa ni sahihi.

Akizungumza jijini hapa jana, Chatanda alisema kauli aliyotoa kuhusu maaskofu kuwa wavue majoho na kuingia siasa, kutokana na kutoa kauli ya kutomtambua Meya wa Arusha, Gaudence Lyimo, inabaki imesimama haina makosa.

Chatanda alisema kabla ya maaskofu kutoa maoni yao, walipaswa kuwaita viongozi wa vyama vya siasa na kujua ukweli badala ya kutoa maamuzi yao.

"Namheshimu sana mzee Malecela, lakini yale ni maoni yake... mimi nilichokizungumza kinabki kimesimama," alisema Chatanda.
Hata hivyo, Chatanda alilaumu vyombo vya habari kwa kulikuza suala la kuwataka maaskofu kuvua majoho, hali ya kuwa alizungumza mengi kuhusiana na mgogoro wa Arusha.

“Niliwaita kutoa tamko la Kamati ya Siasa ya Mkoa, tulipongeza polisi kwa kudhibiti maandamano na pia kuelezea hasara ambayo tumeipata CCM na kutoa pole kwa wafiwa," alisema Chatanda.

Wakati huohuo, Waandishi wa habari mkoani Arusha, wamelalamikia lugha za kejeli na dharau kwa baadhi ya wanahabari mkoani hapa, ambazo zimekuwa zikitolewa na Chatanda.

Chatanda anadaiwa kuwa chanzo cha vurugu hizo ambazo zilisababisha mauaji ya watu watatu na kujeruhi zaidi ya 29, baada ya kuruhusiwa kupiga kura ya kumchagua meya wa Arusha, ilhali amepata ubunge wa viti maalum kupitia Mkoa wa Tanga.

Kutokana na Mkurugenzi wa Jiji la Arusha, kumruhusu kupiga kura, madiwani wa Chadema walisusa kikao na kuondoka, huku uchaguzi huo ukiendelea.
 
KATIBU wa CCM Mkoa wa Arusha, Mary Chatanda, amesema anaheshimu maoni ya aliyekuwa Makamu Mwenyeki wa CCM, John Malecela, lakini anaamini alichokisema kuhusu maaskofu kuvua majoho kama wanataka kuingilia siasa ni sahihi.

Akizungumza jijini hapa jana, Chatanda alisema kauli aliyotoa kuhusu maaskofu kuwa wavue majoho na kuingia siasa, kutokana na kutoa kauli ya kutomtambua Meya wa Arusha, Gaudence Lyimo, inabaki imesimama haina makosa.

Chatanda alisema kabla ya maaskofu kutoa maoni yao, walipaswa kuwaita viongozi wa vyama vya siasa na kujua ukweli badala ya kutoa maamuzi yao.

"Namheshimu sana mzee Malecela, lakini yale ni maoni yake... mimi nilichokizungumza kinabki kimesimama," alisema Chatanda.
Hata hivyo, Chatanda alilaumu vyombo vya habari kwa kulikuza suala la kuwataka maaskofu kuvua majoho, hali ya kuwa alizungumza mengi kuhusiana na mgogoro wa Arusha.

Kama kweli Chatanda anamheshimu sana mheshimiwa Mzee wetu Malecela basi si afuate ushauri wake wenye nasaha kibao...............kuomba msamaha ni kuonyesha umahiri na utashi wa kisiasa dada yangu........................................
 
Bahati yake Zuhura Chatanda ni kwamba Ukristoni hakuna kuombewa kifo bali nikuombewa tu msamaha juu mbinguni laa sivyo ingelikua ni kwa dini yake mpaka sasa albadiri jua kuzama tu na azame na yeye mwenyewe kuzimuni.

Ila mama mwisho huenda ukagoma kuwa mzuri saaanna katika uhai huu huu, ogopa sana sauti ya wengi kuna sauti ya Mwenyezi Mungu mle!!
 
Kama kweli Chatanda anamheshimu sana mheshimiwa Mzee wetu Malecela basi si afuate ushauri wake wenye nasaha kibao...............kuomba msamaha ni kuonyesha umahiri na utashi wa kisiasa dada yangu........................................

mkuu unapigia mbuzi gitaa?
 
Animals have these advantages over man: they die without any idea of death, their funerals cost them nothing, and no one starts lawsuits over their wills. - Voltaire
 
Huya mama hana kitu, afadhari tuachane naye! Ni tunda la mafisadi!
 
Naomba nikupeushauri kidigo Dadangu Maria Chatanda, wewe kweli ni Mwanamke mwenye nguvu lakini kumbuka kuliwahitoke wanawake wenye nguvu kuliko wewe wakakitetea Chama hicho hicho leo hii ukiwaona hutaamini. Unamkumbuka Hawa Ngurume? alikuwa nguvu kama simba dume leo hii huko wapi? Chunga sana dadangu kama kweli unataka kuishi kwa raha Duniani kuwa Mwangalifu na kauli zako CCM sio kila kitu na kila kitu sio CCM.
 
Baba Junjo kuna mjumbe katutahadharisha kwamba huyu mama ni wale wa kujitolea mhanga hivyo tayari keshakata shauri tusijisumbue naye. Kwa tahadhari hiyo, yangu macho na huyo meya wa CCM wa kuchonga.

Jiandaeni twenzetuni mazikoni kwa wafu wetu mashujaa wa mabadiliko tunayoitaka nchini. Natamani Mungu amlinde huyu Chatanda aje aone demokrasia ya kweli inavyofanya kazi utamu bila misuguano isiyo ya lazima pindi wananchi tutakapojiandikia katiba yetu moja kwa moja bila udalali.

Kwa kweli hata Chatanda naye atafurahi sana kuliko hivi sasa ambapo bastola muda wote kwenye maziwa na risasi sita ndani.
 
Na waandishi nao wanampa huyu mama muda asiostahili. For Heaven's sake who the hell is she? Katibu wa CCM anapewa ujiko utadhani ni mtendaji wa serikali ambaye maoni yake yangetusumbua. Mnampa ujiko ambao hajaufanyia kazi. Sikuwahi kumsikia huyu mama hadi hivi majuzi. But I like her style though..
 
Achaneni na huyo mwanamke, mwoneni kama kichaa tu akikunyang'anya nguo chuchumaa wala usimkimbize!
 
Nahisi sophia simba na hawa ghasia wamepata mrithi hebu wadau mwageni elimu ya huyu mary chatanda maana ananichefua baada ya hapo ndo tutaanza kumjadili
 
Mkuu achaneni na huyu vuvuzela msimfanye main topic hapa jf atajiona celeb,
 
Nahisi sophia simba na hawa ghasia wamepata mrithi hebu wadau mwageni elimu ya huyu mary chatanda maana ananichefua baada ya hapo ndo tutaanza kumjadili
majanikv naomba issue isiwe elimu yake bali ni hulka binafsi. Wako ma graduate wanatema pumba huku kuna mababu zetu hata darasa hawalijui lakini busara.
 
majanikv naomba issue isiwe elimu yake bali ni hulka binafsi. Wako ma graduate wanatema pumba huku kuna mababu zetu hata darasa hawalijui lakini busara.

nilitaka kujua sehemu alizopitia mpaka kufika hapo
 
BA (Ulopokaji)
MA (umalaya)
PhD (unafiki na uchonganishi-specialization:-mauaji)
Prof.... bado haja publish vya kutosha!!!!
 
Back
Top Bottom