Chatanda azua tena mvutano CCM, Chadema Arusha | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Chatanda azua tena mvutano CCM, Chadema Arusha

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by kilimasera, Jan 10, 2011.

 1. kilimasera

  kilimasera JF-Expert Member

  #1
  Jan 10, 2011
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 3,073
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  [​IMG]
  Mary Chatanda

  WABUNGE na madiwani wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), jana walisusa kushiriki uchaguzi wa Jumuiya za Serikali za Mitaa Tanzania (ALAT) katika Mkoa wa Arusha.

  Walifikia hatua hiyo wakipinga uwepo wa Mbunge wa Viti maalumu kupitia Jumuiya ya Wanawake (UWT) wa Mkoa wa Tanga, Mery Chatanda katika mkutano huo.


  Mbunge wa Jimbo la Karatu, Mchungaji Israel Natse ambaye alitaka ufafanuzi wa Chatanda kuwepo katika kikao hicho, kwa kuwa kanuni za Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi) wabunge wanaopaswa kuhudhuria kikao hicho, ni wa Mkoa wa Arusha tu na sio vinginevyo.


  Hata hivyo, Mwenyekiti wa muda wa mkutano huo, Ismail Katamboi ambaye ni Diwani wa kata ya Kisongo, katika Halmashauri ya Arusha, alisema Chatanda ni mjumbe halali wa kikao hicho na kutaka shughuli za kikao hicho kuendelea.


  Naye Mwenyekiti wa Halmashauri ya Karatu, Lazaro Massay alisimama na kumtaka Katamboi kueleza kama Chatanda ni Mbunge wa Arusha ama Tanga.


  Lakini Katamboi hakutaka kujibu swali hilo kama alivyotaka Massay bali alisisitiza kuwa Chatanga ni mjumbe halali wa mkutano huo wa Alat na hakutoa ufafanuzi zaidi.


  Baada ya jibu hilo, Diwani Julius ole Sekayane (CCM) ambaye alimwakilisha Meya wa Jiji la Arusha, alisimama na kuwataka wajumbe kuendelea mkutano kwa kuwa Chatanda ni mjumbe halali katika mkutano huo na anayedai kuwa sio halali amekosea.


  Baada ya malumbano hayo, wabunge wa Chadema, Natse wa Karatu na Mbunge wa Arusha mjini, Godbless Lema na madiwani wote wa Chadema waliondoka ndani ya ukumbi wakisema hawako tayari kushiriki uchaguzi huo.


  Natse akizungumza nje ya ukumbi, alisema Chatanda sio mjumbe halali na pili wao wanaungana na wenzao kusema kuwa hawamtambui Meya wa Jiji la Arusha Gaudence Lyimo kwani hakuchaguliwa kufuata kanuni za Tamisemi.


  Mkutano huo wa Alat Mkoa wa Arusha hushirikisha wabunge wote wa mkoa, wenyeviti wa halmashauri za wilaya, wakurugenzi wa halmashauri zote na madiwani wawili waliochaguliwa na baraza la madiwani la wilaya husika.


  Mkutano huo ulikuwa wa kumchagua Mwenyekiti wa Alat mkoa wa Arusha, mweka hazina, kamati ya utendaji na mbunge mwakilishi wa mkoa katika mkutano mkuu wa Alat Taifa.
   
 2. Mpogoro

  Mpogoro JF-Expert Member

  #2
  Jan 11, 2011
  Joined: Dec 7, 2008
  Messages: 361
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Huyu Mery Chatanda ana matatizo gani au ndo cheap popularity!?Yaani inauzunisha kama taratibu na sheria hazifuatwi na hivyo kusababisha matatizo kwenye chaguzi hasa hizi za madiwani.Mambo haya ya uchaguzi yalitakiwa kukamilika mara moja ili viongozi waende wakatumie wananchi!Inasikitisha sana!
   
 3. P

  Percival Salama Senior Member

  #3
  Jan 11, 2011
  Joined: Feb 3, 2010
  Messages: 118
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0

  Watanzania wanapotaka katiba mpya kwa sababu ya mambo kama haya. Mbona hamtupi ufafanuzi wa kutosha watanzania wajue huyu chatanda kama anastahili au hastahili kwa mujibu wa sheria. Tujuzeni tupate kujua na hasa kujua tunaanzia wapi kurusha mijadala mizito ya umuhimu kutenda haki ili amani iweze kudumu. MAANA PASIPO HAKI HAKUNA AMANI na AMANI ya mabavu si ya KUDUMU. Wahenga wana masemo "AMANI NI TUNDA LA HAKI"
   
 4. U

  Unstoppable JF-Expert Member

  #4
  Jan 11, 2011
  Joined: Jan 7, 2011
  Messages: 1,049
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Huyu mama anaudhi kwakweli yuko kama wale wadudu wa mahindi weusi wanaitwa "Tribolium Confuser" ukimbinya unafikiri amekufa anakaa muda anaibuka upya aah! Naona amepewa hiyo kazi maalumu "kuvuruga taratibu za vikao"


   
 5. Quinine

  Quinine JF-Expert Member

  #5
  Jan 11, 2011
  Joined: Jul 26, 2010
  Messages: 10,915
  Likes Received: 12,086
  Trophy Points: 280
  WABUNGE na madiwani wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), jana walisusa kushiriki uchaguzi wa Jumuiya za Serikali za Mitaa Tanzania (ALAT) katika Mkoa wa Arusha wakipinga uwepo wa Mbunge wa Viti maalumu kupitia Jumuiya ya Wanawake (UWT) wa Mkoa wa Tanga, Mery Chatanda katika mkutano huo.

  Walidai Chatanda si mbunge wa Mkoa wa Arusha hivyo hastahili kuwepo pale.

  Baada ya malumbano ya muda murefu, wabunge wa Chadema, Natse wa Karatu na Mbunge wa Arusha mjini, Godbless Lema na madiwani wote wa Chadema waliondoka ndani ya ukumbi wakisema hawako tayari kushiriki uchaguzi huo.
   
 6. The Hunter

  The Hunter JF-Expert Member

  #6
  Jan 11, 2011
  Joined: Dec 25, 2010
  Messages: 1,049
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 145
  Dawa ya wanafki ni kujitenga nao.
   
 7. M

  Malila JF-Expert Member

  #7
  Jan 11, 2011
  Joined: Dec 22, 2007
  Messages: 4,410
  Likes Received: 734
  Trophy Points: 280
  Ili apelekwe Uholansi anatakiwa kuwa na makosa gani? Maana mama huyu anakaribia kupata sifa za kwenda huko.
   
 8. S

  Shiefl Senior Member

  #8
  Jan 11, 2011
  Joined: Oct 31, 2010
  Messages: 145
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mwenda wazimu huyu. Si anatoka kule kwa mzee Makwambe. Tanga shehh. Unatamani umfungulie maji ya baridi ili akaamke usingizini. Si umesikia tena na wale SSM walikwambia ni mjumbe halali wa Arusha. Hapa ni utoto na mzee Pinda kazi ishamshinda piii. Hii ndo wizara yake. Akina Mwanri machachari na falsafa za kiuchumi wapi hawasikii kisa mzee wa chama kasema. Upuuzi tu
   
 9. TATIANA

  TATIANA JF-Expert Member

  #9
  Jan 11, 2011
  Joined: Dec 8, 2010
  Messages: 4,103
  Likes Received: 472
  Trophy Points: 180
  una maanisha akili yake imesinzia eeh! Haaa, thx
   
 10. Humphnicky

  Humphnicky JF-Expert Member

  #10
  Jan 11, 2011
  Joined: Dec 1, 2010
  Messages: 1,808
  Likes Received: 526
  Trophy Points: 280
  HUYU NDO MARY CHATANDA


  [​IMG]
   
 11. taffu69

  taffu69 JF-Expert Member

  #11
  Jan 11, 2011
  Joined: Feb 26, 2007
  Messages: 2,089
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 135
  Huyu mama anatiwa kiburi na Makamba, CCM inabidi wawe makini sana na watu wenye tabia kama ya Makamba. Makamba anazeeka vibaya na amekosa hata chembe ndogo ya busara, viongozi wa CCM wasipokuwa makini kuna hatari ya taifa letu kutumbukia kwenye janga kubwa kwa sababu ya watu wachache wasiokuwa na busara. Kwa nini huyu mama ateuliwe kupitia mkoa wa Tanga halafu akasababishe tafrani huko Arusha na viongozi wakae kimya?
   
 12. Kamakabuzi

  Kamakabuzi JF-Expert Member

  #12
  Jan 11, 2011
  Joined: Dec 3, 2007
  Messages: 1,499
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  Tusipokuwa makini iko siku rais wa nchi ya nje atakuwa pia rais wa tanzania! au kwa mfano askari mkenya atakuwa pia askari wa tanzania, na vita kati ya tz na kenya ikitokea tunamfanya kuwa kamanda wa vikosi vya tanzania (halafu tunategemea kushinda). Ukiuliza sababu utaambiwa kenya ilimteua huyu kufanya kazi tanzania hivyo hakuna kikwazo kwake kuipigania tanzania anakofanyia kazi!!
   
 13. Kamakabuzi

  Kamakabuzi JF-Expert Member

  #13
  Jan 11, 2011
  Joined: Dec 3, 2007
  Messages: 1,499
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  Makamba siyo mwamuzi wa mwisho katika ccm; juu yake kuna mwenyekiti, huyu nae lazima awe anamuunga mkono makamba. Kwa hiyo JK anaunga mkono suala hili.
  Hakuna pa kukimbilia ila kwenye nguvu ya umma.
   
 14. f

  fundimchundo Senior Member

  #14
  Jan 11, 2011
  Joined: Jul 23, 2010
  Messages: 150
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 35
  Wataalamu wa Serikali za Mitaa tufafanulieni tafadhali.
  Mawazir na manaibu wao wote ni Wabunge wanaofanya kazi jijini Dar es Salaam na hawahudhurii vikao vya Jiji la Dar na Manispaa zake.
  Kwa nini hili la Mary Chatanda linaruhusiwa kuleta tafrani hadi kusababisha Mauaji ya Watanzania wenzetu?
  What are the Rules and Regulations relating to this matter?
  Au Mawaziri na ma-Naibu wao wanakosea kutohudhuria vikao vya Jiji la Dar?
   
 15. M

  Mwikimbi JF-Expert Member

  #15
  Jan 11, 2011
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 1,745
  Likes Received: 109
  Trophy Points: 160
  Amen
   
 16. Wabogojo

  Wabogojo JF-Expert Member

  #16
  Jan 11, 2011
  Joined: Nov 5, 2010
  Messages: 355
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Ole wao CHADEMA kama wangekubali uwepo wa Chatanda hapo kikaoni basi wangekuwa wamemhalalisha hata uwepo wake wa kwenye kikao cha uchaguzi wa kumchagua Mtahiki Meya wa Jiji la Arusha.

  Hongereni sana wajumbe wa CHADEMA kwa kuutegua huo mtego.
   
 17. kinya

  kinya JF-Expert Member

  #17
  Jan 11, 2011
  Joined: Feb 20, 2009
  Messages: 483
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 35
  safi sana hakuna kuchangamana na hao wanaosabisha mauaji ya wengine kwa uroho.
  vp lakini huo mkutana/uchaguzi uliendelea au uliahirishwa.
   
 18. STEIN

  STEIN JF-Expert Member

  #18
  Jan 11, 2011
  Joined: Aug 29, 2010
  Messages: 1,764
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Huu ndio uzuri wa CDM wana misimamo hadi utapenda. Hakuna kufunika kikombe mwanaharamu apite.

  Peoples power!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
   
 19. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #19
  Jan 11, 2011
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,334
  Likes Received: 22,184
  Trophy Points: 280
  Ana laana binti huyu
   
 20. Polisi

  Polisi JF-Expert Member

  #20
  Jan 11, 2011
  Joined: Nov 22, 2010
  Messages: 2,087
  Likes Received: 39
  Trophy Points: 145
  Mimi naomba mwenye data za kutosha kuhusu maeneo ya uwakilishi wa wabunge wa viti maalum atumwagie hapa. inanipa shida sana. Assubuhi tambo hizo, sorry tambwe hiza amesema sheria ya uchaguzi inazungumzia uwakilishi wa mbunge wa viti maalum sehemu anayoishi siyo anayofanyia kazi. mfano wabunge wetu wa CDM wanawakilisha mikoa au majimbo? mimi napenda tulumbane kwa hoja. mbona mza, hai, kgm, moshi, huu utata haujajitokeza, huko hakuna wabunge wa viti maalum?
   
Loading...