Character Never Lies! Utamtambuaje Mtu Mwema au Mbaya?

Character Never Lies! Utamtambuaje Mtu Mwema au Mbaya?

Vyote viwili, Universe haitambui mtu mwema au mbaya, yenyewe ina respond kutokana na vibration unayo provide baada ya tukio kufanyiwa.

Ukiwa mwema hata kidogo then ukawa disappointed na matokeo ya wema huo najua utalalamika sana,

Hapa kuna mfanya na mfanyiwa, aliekufanyia ubaya universe haiwezi muhukumu coz he/she doesn’t give a f*ck so no vibration there

Kwa wewe mfanyiwa kule kulalamika kwako kutapelekea universe ione you deserve kile kitu hence matukio ya aina hiyo ya kufanyiwa ubaya hayataisha maishani mwako mpaka uanze na wewe roho ngumu.
Okay karibu tena
 
Interesting…. Wanasema hakuna mtu mbaya/mwema entirely.
Mimi naamini kila mtu ana ile tabia yake isiyoweza kubadilika kwa mazingira yaani tabia kuu
Bali mtu anakuwa mwema/mbaya kulingana na vile anavyojisikia kuhusu wewe.
Kuna watu ni wabaya kwa sababu tu umewazidi kitu fulani na hii haiwezi kuhalalisha tabia yake mbaya et imetokana na mazingira ya wewe kumzidi labda kama sielewi
Ndio maana mtu akikuonesha ubaya kwa mara ya kwanza, muamini…. kwasababu kwanini amejisikia kuwa mbaya kwako kwa mara ya kwanza tu? Hajataka kukupa hata grace period…..
Exactly
 
kuwa mtu mwema hiyo ni weakness tayar na watu wata take advantage na mwisho hautafika mbali,

Hakuna rewards ukiwa mtu mwema zaid ya disappointment.

Cheers kwa wenye roho mbaya wote🍻
Ni sahihi.

Lakini kuwa mtu mwema ni faida kwako na si kwa wengine . Kuna level fulani ya amani mtu unakuwa nayo ukiwa unafahamu haujamfanyia mtu ubaya.

Kuwa mwema, usiwe naive, imarisha mipaka.
 
Kwenye hii dunia vitu vingi vimeumbwa viwili viwili: binadamu, wanyama, wadudu

Hata kwenye tabia zipo nzuri na zipo mbaya
Watu wapo wema na wapo wabaya

Hapa sina maana ya muonekano wa mtu, I'm talking about character, kwa sababu tabia yako ndiyo itatuambia wewe ni nani, na tabia yangu ndiyo itawaambia mimi ni nani

Sasa je, tabia za nje zinatosha kumjua mtu kuwa ni mbaya au mwema?

Kwa mtazamo wangu jibu ni ndiyo, ila si mara zote tabia ya nje huonyesha kilichopo ndani

Kuna watu wanaonekana wema sana, lakini ndani wamejaa hila

Na kuna watu wanaonekana wakali au wagumu, lakini ndani wana mioyo safi sana

Lakini ukweli ni kwamba, actions speak louder than words

Mwisho wa siku tutakutambua kwa matendo yako

Sasa ni matendo gani ukiyaona kwa mtu unahitimisha kuwa huyu ni mtu mwema?

Kwangu mimi, mtu mwema nampima kwanza kwa upendo alionao kwa wengine

Mtu mwema mara nyingi habebi chuki wala roho mbaya kwa wengine

Mara nyingi watu wema huwa watulivu wanapoamua mambo, kwa sababu wanaamini wakifanya haraka wanaweza kusababisha matatizo au hasara kwa wengine

Watu wema hujali hisia za wengine Kama hawezi kukusaidia, mara nyingi hayupo tayari kukuumiza au kukupa matatizo

Mtu mwema hufurahia kuona wengine wakifanikiwa

Akiona mwenzake amepiga hatua hasemi
(Kwa nini yeye?)Badala yake anasema, Hongera🤗
Anaamini mafanikio ya mwingine hayapunguzi nafasi yake

Mtu mwema akimkosea mtu huwa yupo tayari kuomba msamaha

Na akikosolewa hasikii vibaya kila wakati, kwa sababu anajua hakuna binadamu mkamilifu

Kwa hiyo ukipata mtu wa aina hii kwenye maisha yako, usimchukulie poa

Watu wema ni wachache kuliko tunavyofikiri

Mara nyingi huwa ndiyo watu wanaokupa amani ya moyo wanakushauri kwa faida yako hata kama ukweli unauma wanakuombea mema hata ukiwa haupo nao, na wanabaki upande wako hata pale ambapo hawapati faida yoyote kutoka kwako

Ukiwa na mtu mwema karibu yako, mara nyingi unajikuta hata wewe unabadilika na kuwa mtu bora zaidi Positive people create positive lives
👇

Sasa twende kwa mtu mbaya...

Mtu mbaya mara nyingi hubeba chuki dhidi ya wengine

Moyo wake huwa kama umekufa ganzi, hana anachojali kuhusu wengine

Hata kama hana cha kukusaidia, atafanya juu chini akupe maumivu

Mtu mbaya marafiki zake ni unafiki, uchonganishi, umbeya, ubinafsi, chuki na husda

Mtu mbaya hataki kuona wenzake wakifanya vizuri

Anataka yeye ndiye awe top kwenye kila kitu

Akiona wenzie wanasifiwa, roho inamnyonga akiamini hawastahili

Hufurahia maanguko ya watu

Yule alikuwa anajidai, sasa amekuwa kama sisi kiko wapi🤣

Mtu mbaya hubeba chuki ambayo mwisho wa siku hummaliza yeye mwenyewe kidogo kidogo

Lakini pia ni hatari kua karibu yake maana chuki aliyoificha ndani akiitoa njee ni majanga

Anaweza kutabasamu mbele yako, lakini ndani anateseka kwa sababu tu huwezi kuanguka kama anavyotamani

Na kitu kingine nilichokiona, mtu mbaya huwa ni mgumu sana kufurahia mafanikio ya wengine

Kila zuri analigeuza baya kila mafanikio anaona kuna mchezo umefanyika utasikia
(hapa si bure kuna kitu)

Shida ya kuwa karibu na mtu wa aina hii ni kwamba taratibu utaanza kupoteza amani yako bila kujua

Atakuvuruga kisaikolojia, atakufanya uwaone wengine wabaya kama yeye, atakukatisha tamaa kila unapopiga hatua na wakati mwingine anaweza kuwa sababu ya wewe kuharibu mahusiano yako na watu wasiokuwa na kosa

Watu wabaya hua pia wanapenda wakikosana na watu na wewe eti ukosane nao pia hua wanapenda kurithisha uadui🤣🤣

Watu wa aina hii wakishindwa kukutumia, wanaanza kukuchafua Ndiyo maana kuna msemo unasema, show me your friends and I'll tell you who you are

Mara nyingi tabia huambukiza, hivyo ukikaa sana na mtu mwenye roho mbaya bila kuwa makini, unaweza kujikuta unaanza kufanana naye bila hata kugundua

Sasa hapo tumeona baadhi ya tabia za watu wema na watu wabaya na huo ni mtazamo wangu


Wewe ongezea...

Ni tabia gani ukiiona kwa mtu unaamini kabisa huyu ni mtu mwema?

Na ni tabia gani ukiiona unaona huyu ana roho mbaya?

Halafu ukijipima wewe mwenyewe, kwa tabia zako za ndani na nje unajiona upo upande gani?

Happy Tuesday 😊
ShesRise_1 ✋️
Kumjua mtu mwema au mbaya inabidi ufatilie tabia zake Kwa wengine
&
Vinginevyo inabidi akupige tukio Ili ujue kuwa ni mbaya au akutendee wema ujue kua ni mwema
Asante.
 
Ni sahihi.

Lakini kuwa mtu mwema ni faida kwako na si kwa wengine . Kuna level fulani ya amani mtu unakuwa nayo ukiwa unafahamu haujamfanyia mtu ubaya.

Kuwa mwema, usiwe naive, imarisha mipaka.
♥️♥️
 
Kumjua mtu mwema au mbaya inabidi ufatilie tabia zake Kwa wengine
&
Vinginevyo inabidi akupige tukio Ili ujue kuwa ni mbaya au akutendee wema ujue kua ni mwema
Asante.
Sahihi.


Kwangu mimi hata mtu akinifanyia wema siwezi kuconclude kuwa huyu ni mtu mwema, kuna performative kindness…. hii ni kindness yenye lengo fulani.

Kipimo changu cha tabia ya mtu ni ubaya anaowafanyia wengine walioko kwenye situation moja na mimi.
 
Sahihi.


Kwangu mimi hata mtu akinifanyia wema siwezi kuconclude kuwa huyu ni mtu mwema, kuna performative kindness…. hii ni kindness yenye lengo fulani.

Kipimo changu cha tabia ya mtu ni ubaya anaowafanyia wengine walioko kwenye situation moja na mimi.
My sister 🥰
 
ShesRise_1

Kuna watu wanaamini aliyewatuma watu kuua watu 29 October ni mtu mwema.
🤔🤔🤔🤔🤔🤔
What’s your take babes

😜
Kuna watu wamesema kua ni mbaya

Kuna watu wanasema et ni mwema

Unajua huyo inaedaiwa alituma watu kuua anaweza kusema aliona tishio kwa usalama wake na nchi

Akaamua kuchukua maamzi magumu utamuamini?

Waliouwawa/ kujeruhiwa nao watasema waliona tishio la huyo mtu kwa nchi na uchumi na sababu zingine telee

so wakaona ngoja waingie front
Ndio yakatokea yaliyotokea

In fact kila mtu upande utajihesabia haki na kuona uliamua sahihi

Sasa kinachobaki ni wewe unaetazama unatazama kwa jicho gani?

Hapo nimekujibu tayari 😊
Tafadhari usiniombe jibu lingine babie 💋
 
binafsi kitu kinachoanza kunistua kwamba huenda inawezekana kwa asilimia kubwa mtu niliyekutana nae eidha ana intensions mbaya na mimi ama inaweza isiwe intensions mbaya ila anataka kunitumia kwa hila ( taking advantage ) mapema sana nikiona mtu ananiiga hasa character yangu ama namna ninavyoyatizama mambo umakini unaongezeka juu ya mtu huyo. hiyo huwa ni sign yangu ya awali kabisa.
 
binafsi kitu kinachoanza kunistua kwamba huenda inawezekana kwa asilimia kubwa mtu niliyekutana nae eidha ana intensions mbaya na mimi ama inaweza isiwe intensions mbaya ila anataka kunitumia kwa hila ( taking advantage ) mapema sana nikiona mtu ananiiga hasa character yangu ama namna ninavyoyatizama mambo umakini unaongezeka juu ya mtu huyo. hiyo huwa ni sign yangu ya awali kabisa.
Ilikuaje mpka hiyo ikawa ndio signal yako?
Kuna story?
 
Back
Top Bottom