Character Never Lies! Utamtambuaje Mtu Mwema au Mbaya?

🤔🤔🤔🤔🤔🤔

Kuna watu wamesema kua ni mbaya

Kuna watu wanasema et ni mwema

Unajua huyo inaedaiwa alituma watu kuua anaweza kusema aliona tishio kwa usalama wake na nchi

Akaamua kuchukua maamzi magumu utamuamini?

Waliouwawa/ kujeruhiwa nao watasema waliona tishio la huyo mtu kwa nchi na uchumi na sababu zingine telee

so wakaona ngoja waingie front
Ndio yakatokea yaliyotokea

In fact kila mtu upande utajihesabia haki na kuona uliamua sahihi

Sasa kinachobaki ni wewe unaetazama unatazama kwa jicho gani?

Hapo nimekujibu tayari 😊
Tafadhari usiniombe jibu lingine babie 💋
Uko sahihi, ilikuwa ni challenge ili tupanue mjadala.

Na kwa majibu yako ndio maana tunapata kipimo cha wema au ubaya according to….
1.Culture
2.Dini
3.Sheria za nchi
4.sheria za kimataifa.
5. Individual (msingi wa mada yetu ya leo)

Watu karibu wote wamejibu vizuri, mada nzuri.
 
Kwenye hii dunia vitu vingi vimeumbwa viwili viwili: binadamu, wanyama, wadudu

Hata kwenye tabia zipo nzuri na zipo mbaya
Watu wapo wema na wapo wabaya

Hapa sina maana ya muonekano wa mtu, I'm talking about character, kwa sababu tabia yako ndiyo itatuambia wewe ni nani, na tabia yangu ndiyo itawaambia mimi ni nani

Sasa je, tabia za nje zinatosha kumjua mtu kuwa ni mbaya au mwema?

Kwa mtazamo wangu jibu ni ndiyo, ila si mara zote tabia ya nje huonyesha kilichopo ndani

Kuna watu wanaonekana wema sana, lakini ndani wamejaa hila

Na kuna watu wanaonekana wakali au wagumu, lakini ndani wana mioyo safi sana

Lakini ukweli ni kwamba, actions speak louder than words

Mwisho wa siku tutakutambua kwa matendo yako

Sasa ni matendo gani ukiyaona kwa mtu unahitimisha kuwa huyu ni mtu mwema?

Kwangu mimi, mtu mwema nampima kwanza kwa upendo alionao kwa wengine

Mtu mwema mara nyingi habebi chuki wala roho mbaya kwa wengine

Mara nyingi watu wema huwa watulivu wanapoamua mambo, kwa sababu wanaamini wakifanya haraka wanaweza kusababisha matatizo au hasara kwa wengine

Watu wema hujali hisia za wengine Kama hawezi kukusaidia, mara nyingi hayupo tayari kukuumiza au kukupa matatizo

Mtu mwema hufurahia kuona wengine wakifanikiwa

Akiona mwenzake amepiga hatua hasemi
(Kwa nini yeye?)Badala yake anasema, Hongera🤗
Anaamini mafanikio ya mwingine hayapunguzi nafasi yake

Mtu mwema akimkosea mtu huwa yupo tayari kuomba msamaha

Na akikosolewa hasikii vibaya kila wakati, kwa sababu anajua hakuna binadamu mkamilifu

Kwa hiyo ukipata mtu wa aina hii kwenye maisha yako, usimchukulie poa

Watu wema ni wachache kuliko tunavyofikiri

Mara nyingi huwa ndiyo watu wanaokupa amani ya moyo wanakushauri kwa faida yako hata kama ukweli unauma wanakuombea mema hata ukiwa haupo nao, na wanabaki upande wako hata pale ambapo hawapati faida yoyote kutoka kwako

Ukiwa na mtu mwema karibu yako, mara nyingi unajikuta hata wewe unabadilika na kuwa mtu bora zaidi Positive people create positive lives
👇

Sasa twende kwa mtu mbaya...

Mtu mbaya mara nyingi hubeba chuki dhidi ya wengine

Moyo wake huwa kama umekufa ganzi, hana anachojali kuhusu wengine

Hata kama hana cha kukusaidia, atafanya juu chini akupe maumivu

Mtu mbaya marafiki zake ni unafiki, uchonganishi, umbeya, ubinafsi, chuki na husda

Mtu mbaya hataki kuona wenzake wakifanya vizuri

Anataka yeye ndiye awe top kwenye kila kitu

Akiona wenzie wanasifiwa, roho inamnyonga akiamini hawastahili

Hufurahia maanguko ya watu

Yule alikuwa anajidai, sasa amekuwa kama sisi kiko wapi🤣

Mtu mbaya hubeba chuki ambayo mwisho wa siku hummaliza yeye mwenyewe kidogo kidogo

Lakini pia ni hatari kua karibu yake maana chuki aliyoificha ndani akiitoa njee ni majanga

Anaweza kutabasamu mbele yako, lakini ndani anateseka kwa sababu tu huwezi kuanguka kama anavyotamani

Na kitu kingine nilichokiona, mtu mbaya huwa ni mgumu sana kufurahia mafanikio ya wengine

Kila zuri analigeuza baya kila mafanikio anaona kuna mchezo umefanyika utasikia
(hapa si bure kuna kitu)

Shida ya kuwa karibu na mtu wa aina hii ni kwamba taratibu utaanza kupoteza amani yako bila kujua

Atakuvuruga kisaikolojia, atakufanya uwaone wengine wabaya kama yeye, atakukatisha tamaa kila unapopiga hatua na wakati mwingine anaweza kuwa sababu ya wewe kuharibu mahusiano yako na watu wasiokuwa na kosa

Watu wabaya hua pia wanapenda wakikosana na watu na wewe eti ukosane nao pia hua wanapenda kurithisha uadui🤣🤣

Watu wa aina hii wakishindwa kukutumia, wanaanza kukuchafua Ndiyo maana kuna msemo unasema, show me your friends and I'll tell you who you are

Mara nyingi tabia huambukiza, hivyo ukikaa sana na mtu mwenye roho mbaya bila kuwa makini, unaweza kujikuta unaanza kufanana naye bila hata kugundua

Sasa hapo tumeona baadhi ya tabia za watu wema na watu wabaya na huo ni mtazamo wangu

Wewe ongezea...

Ni tabia gani ukiiona kwa mtu unaamini kabisa huyu ni mtu mwema?

Na ni tabia gani ukiiona unaona huyu ana roho mbaya?

Halafu ukijipima wewe mwenyewe, kwa tabia zako za ndani na nje unajiona upo upande gani?

Happy Tuesday 😊
ShesRise_1 ✋️
Ukitumia nadharia/falsafa ya Johari Window utaweza kupambanua binadamu tulivyo. Hatutabiriki yan au ni vigumu sana mtu kujifunua/kujiweka wazzi hadi wenzake wamfahamu kwa kiundani wake i.e ni mwema au ni mbaya. Itategemea yule mtu anayefanya Tathmini juu ya mhusika. Wewe unayemwona Mbaya kwako ni Mwema kwa wenzio.& vice versa. Yule anayeonekana Leo ni mwema Kesho anaweza akaonekana ni Mbaya hadi waliosema ni Mwema wakashangaa n.k.n.k.
 
Nje ya mada!
Hivi kuna utafiti wowote uliowahi kufanyika juu ya uwezo wa wabongo kuelewa na kulijibu swali? Kama upo naombeni link.
We acha tu maswali ni mengine
Majibu nimengine

Uzuri bado tupo ndani ya mada

Anyway twende hivyo hivyo😊
 
Uko sahihi, ilikuwa ni challenge ili tupanue mjadala.

Na kwa majibu yako ndio maana tunapata kipimo cha wema au ubaya according to….
1.Culture
2.Dini
3.Sheria za nchi
4.sheria za kimataifa.
5. Individual (msingi wa mada yetu ya leo)

Watu karibu wote wamejibu vizuri, mada nzuri.
Love you 😍
 
Ukitumia nadharia/falsafa ya Johari Window utaweza kupambanua binadamu tulivyo. Hatutabiriki yan au ni vigumu sana mtu kujifunua/kujiweka wazzi hadi wenzake wamfahamu kwa kiundani wake i.e ni mwema au ni mbaya. Itategemea yule mtu anayefanya Tathmini juu ya mhusika. Wewe unayemwona Mbaya kwako ni Mwema kwa wenzio.& vice versa. Yule anayeonekana Leo ni mwema Kesho anaweza akaonekana ni Mbaya hadi waliosema ni Mwema wakashangaa n.k.n.k.
Upo sahihi si katai kumfanyia utafiti mtu tena ule wa kina kama unavyosema ni kweli ndio utaweza kumfahamu zaidi

Japo pia ni ngumu kumjua in deep
Ila mazingira yanaweza kumfanye uhalisia wake wa ndani anaouficha au oneshe njee

Hat

Pia usisahu kila mtu ana tabia yake kuu inayomtambulisha
 
Kwenye hii dunia vitu vingi vimeumbwa viwili viwili: binadamu, wanyama, wadudu

Hata kwenye tabia zipo nzuri na zipo mbaya
Watu wapo wema na wapo wabaya

Hapa sina maana ya muonekano wa mtu, I'm talking about character, kwa sababu tabia yako ndiyo itatuambia wewe ni nani, na tabia yangu ndiyo itawaambia mimi ni nani

Sasa je, tabia za nje zinatosha kumjua mtu kuwa ni mbaya au mwema?

Kwa mtazamo wangu jibu ni ndiyo, ila si mara zote tabia ya nje huonyesha kilichopo ndani

Kuna watu wanaonekana wema sana, lakini ndani wamejaa hila

Na kuna watu wanaonekana wakali au wagumu, lakini ndani wana mioyo safi sana

Lakini ukweli ni kwamba, actions speak louder than words

Mwisho wa siku tutakutambua kwa matendo yako

Sasa ni matendo gani ukiyaona kwa mtu unahitimisha kuwa huyu ni mtu mwema?

Kwangu mimi, mtu mwema nampima kwanza kwa upendo alionao kwa wengine

Mtu mwema mara nyingi habebi chuki wala roho mbaya kwa wengine

Mara nyingi watu wema huwa watulivu wanapoamua mambo, kwa sababu wanaamini wakifanya haraka wanaweza kusababisha matatizo au hasara kwa wengine

Watu wema hujali hisia za wengine Kama hawezi kukusaidia, mara nyingi hayupo tayari kukuumiza au kukupa matatizo

Mtu mwema hufurahia kuona wengine wakifanikiwa

Akiona mwenzake amepiga hatua hasemi
(Kwa nini yeye?)Badala yake anasema, Hongera🤗
Anaamini mafanikio ya mwingine hayapunguzi nafasi yake

Mtu mwema akimkosea mtu huwa yupo tayari kuomba msamaha

Na akikosolewa hasikii vibaya kila wakati, kwa sababu anajua hakuna binadamu mkamilifu

Kwa hiyo ukipata mtu wa aina hii kwenye maisha yako, usimchukulie poa

Watu wema ni wachache kuliko tunavyofikiri

Mara nyingi huwa ndiyo watu wanaokupa amani ya moyo wanakushauri kwa faida yako hata kama ukweli unauma wanakuombea mema hata ukiwa haupo nao, na wanabaki upande wako hata pale ambapo hawapati faida yoyote kutoka kwako

Ukiwa na mtu mwema karibu yako, mara nyingi unajikuta hata wewe unabadilika na kuwa mtu bora zaidi Positive people create positive lives
👇

Sasa twende kwa mtu mbaya...

Mtu mbaya mara nyingi hubeba chuki dhidi ya wengine

Moyo wake huwa kama umekufa ganzi, hana anachojali kuhusu wengine

Hata kama hana cha kukusaidia, atafanya juu chini akupe maumivu

Mtu mbaya marafiki zake ni unafiki, uchonganishi, umbeya, ubinafsi, chuki na husda

Mtu mbaya hataki kuona wenzake wakifanya vizuri

Anataka yeye ndiye awe top kwenye kila kitu

Akiona wenzie wanasifiwa, roho inamnyonga akiamini hawastahili

Hufurahia maanguko ya watu

Yule alikuwa anajidai, sasa amekuwa kama sisi kiko wapi🤣

Mtu mbaya hubeba chuki ambayo mwisho wa siku hummaliza yeye mwenyewe kidogo kidogo

Lakini pia ni hatari kua karibu yake maana chuki aliyoificha ndani akiitoa njee ni majanga

Anaweza kutabasamu mbele yako, lakini ndani anateseka kwa sababu tu huwezi kuanguka kama anavyotamani

Na kitu kingine nilichokiona, mtu mbaya huwa ni mgumu sana kufurahia mafanikio ya wengine

Kila zuri analigeuza baya kila mafanikio anaona kuna mchezo umefanyika utasikia
(hapa si bure kuna kitu)

Shida ya kuwa karibu na mtu wa aina hii ni kwamba taratibu utaanza kupoteza amani yako bila kujua

Atakuvuruga kisaikolojia, atakufanya uwaone wengine wabaya kama yeye, atakukatisha tamaa kila unapopiga hatua na wakati mwingine anaweza kuwa sababu ya wewe kuharibu mahusiano yako na watu wasiokuwa na kosa

Watu wabaya hua pia wanapenda wakikosana na watu na wewe eti ukosane nao pia hua wanapenda kurithisha uadui🤣🤣

Watu wa aina hii wakishindwa kukutumia, wanaanza kukuchafua Ndiyo maana kuna msemo unasema, show me your friends and I'll tell you who you are

Mara nyingi tabia huambukiza, hivyo ukikaa sana na mtu mwenye roho mbaya bila kuwa makini, unaweza kujikuta unaanza kufanana naye bila hata kugundua

Sasa hapo tumeona baadhi ya tabia za watu wema na watu wabaya na huo ni mtazamo wangu

Wewe ongezea...

Ni tabia gani ukiiona kwa mtu unaamini kabisa huyu ni mtu mwema?

Na ni tabia gani ukiiona unaona huyu ana roho mbaya?

Halafu ukijipima wewe mwenyewe, kwa tabia zako za ndani na nje unajiona upo upande gani?

Happy Tuesday 😊
ShesRise_1 ✋️
In fact,
mambo yamebadilika sana nyakati hizi,
na uovu mwingi umejificha kwenye wema, na kwahivyo ni vigumu mno kuditect ubaya wa muovu unless kuna Neema na Baraka za Mungu za kipekee na za kutosha ndani yako.

hata hivyo,
ukigusa strengths yake muovu mapema,
kwa kujua au kutokujua, ni wazi unaweza kugundua haraka aina ya ukali wake ambao unaweza kukuwezesha kuhisi, kujua au kutambua nia yake ovu dhidi yako.

May the blood of Jesus Christ protect you and your family from every form of evil planned against you. :HAhaa:
 
Vyote viwili, Universe haitambui mtu mwema au mbaya, yenyewe ina respond kutokana na vibration unayo provide baada ya tukio kufanyiwa.

Ukiwa mwema hata kidogo then ukawa disappointed na matokeo ya wema huo najua utalalamika sana,

Hapa kuna mfanya na mfanyiwa, aliekufanyia ubaya universe haiwezi muhukumu coz he/she doesn’t give a f*ck so no vibration there

Kwa wewe mfanyiwa kule kulalamika kwako kutapelekea universe ione you deserve kile kitu hence matukio ya aina hiyo ya kufanyiwa ubaya hayataisha maishani mwako mpaka uanze na wewe roho ngumu.
Maelezo haya mtu akiyafata anapotea

Energy ya mtenda na mtendwa zote ziko sawa. Yaani ukifanya ubaya na ukipokea ubaya wote ni level moja tu..

It comes from the same thing.... FEAR.
 
Binadamu ni mbaya pia ni mwema ana darkside na right side

Kinachotokea Kuna ambao Wana balance hizo pande mbili na ambao wanashindwa na kuegemea upande Mmoja pekee .

Binadamu ni pande mbili kwa wakati mmoja

1. DARK SIDE
Hii ni sehemu ya wivu, hasira, tamaa, ubinafsi, kulipiza kisasi.
Ni ile sauti inayosema "chukua yako kwanza", "watalia wao".
Haitoweki. Iko ndani ya kila mtu.

2. RIGHT SIDE / LIGHT SIDE
Hii ni huruma, upendo, uaminifu, kutoa, kusamehe.
Ni ile sauti inayosema "msaidie", "fanya kilicho sahihi hata kama hakuna anayeona".

Kwa nini wengine wanapotea?

Kama ulivyosema kuna watu 2:

Aina 1: WENYE BALANCE
Wanajua wana darkside, lakini hawaiachii iwaongoze.
Wanaitumia hasira yao kujitetea, sio kuwadhuru.
Wanaitumia tamaa yao kujenga, sio kuiba.
Hawa ndio tunasema "ana moyo mzuri lakini si mjinga"

Aina 2: WENYE KUEGEMEZA UPANDE MOJA
1. Wale wa Light tu → Wanakuwa wajinga. Watu wanawatumia. Mwishoni wanachoka na kuwa wachoyo zaidi ya wengine
2. Wale wa Dark tu → Wanakuwa wakatili. Wanapata vitu haraka lakini wanakufa wakiwa peke yao

Siri ya Balance ni nini?
Sio kufuta darkside. Sio kujifanya malaika 24/7.

Balance = Kujua lini kutumia upande gani

Mfano:
Ukimya = Right side. Lakini wakati mwingine lazima useme "Hapana" = Dark side yenye mipaka.
Kutoa = Right side. Lakini wakati mwingine lazima ujilinde = Dark side yenye hekima.

Watu wenye balance wanaamani ndani. Hawajipingi wenyewe.

---

Carl Jung alisema: "Huwezi kufika nuru bila kwenda ndani ya giza lako kwanza"
 
Interesting…. Wanasema hakuna mtu mbaya/mwema entirely.

Bali mtu anakuwa mwema/mbaya kulingana na vile anavyojisikia kuhusu wewe.

Ndio maana mtu akikuonesha ubaya kwa mara ya kwanza, muamini…. kwasababu kwanini amejisikia kuwa mbaya kwako kwa mara ya kwanza tu? Hajataka kukupa hata grace period…..
Hiyo ni illusion uliyo iongelea hapo

Hakuna aliye mbaya... Na usimwamini.

Amini kilicho tokea ila mtu si mbaya wala mzuri.

That's why watu hatuendelei kwa sababu tu naweka watu kwenye mafungu kama nyanya.
 
In fact,
mambo yamebadilika sana nyakati hizi,
na uovu mwingi umejificha kwenye wema, na kwahivyo ni vigumu mno kuditect ubaya wa muovu unless kuna Neema na Baraka za Mungu za kipekee na za kutosha ndani yako.
Ndio ni kweli kwa wale wenye imani wanaelewa sana hii
hata hivyo,
ukigusa strengths yake muovu mapema,
kwa kujua au kutokujua, ni wazi unaweza kugundua haraka aina ya ukali wake ambao unaweza kukuwezesha kuhisi, kujua au kutambua nia yake ovu dhidi yako.
Ni kweli
May the blood of Jesus Christ protect you and your family from every form of evil planned against you. :HAhaa:
Amen ♥️
 
Binadamu ni pande mbili kwa wakati mmoja

1. DARK SIDE

Hii ni sehemu ya wivu, hasira, tamaa, ubinafsi, kulipiza kisasi.
Ni ile sauti inayosema "chukua yako kwanza", "watalia wao".
Haitoweki. Iko ndani ya kila mtu.

2. RIGHT SIDE / LIGHT SIDE
Hii ni huruma, upendo, uaminifu, kutoa, kusamehe.
Ni ile sauti inayosema "msaidie", "fanya kilicho sahihi hata kama hakuna anayeona".

Kwa nini wengine wanapotea?

Kama ulivyosema kuna watu 2:

Aina 1: WENYE BALANCE
Wanajua wana darkside, lakini hawaiachii iwaongoze.
Wanaitumia hasira yao kujitetea, sio kuwadhuru.
Wanaitumia tamaa yao kujenga, sio kuiba.
Hawa ndio tunasema "ana moyo mzuri lakini si mjinga"

Aina 2: WENYE KUEGEMEZA UPANDE MOJA
1. Wale wa Light tu → Wanakuwa wajinga. Watu wanawatumia. Mwishoni wanachoka na kuwa wachoyo zaidi ya wengine
2. Wale wa Dark tu → Wanakuwa wakatili. Wanapata vitu haraka lakini wanakufa wakiwa peke yao

Siri ya Balance ni nini?
Sio kufuta darkside. Sio kujifanya malaika 24/7.

Balance = Kujua lini kutumia upande gani

Mfano:
Ukimya = Right side. Lakini wakati mwingine lazima useme "Hapana" = Dark side yenye mipaka.
Kutoa = Right side. Lakini wakati mwingine lazima ujilinde = Dark side yenye hekima.

Watu wenye balance wanaamani ndani. Hawajipingi wenyewe.

---

Carl Jung alisema: "Huwezi kufika nuru bila kwenda ndani ya giza lako kwanza"
Shukran mkuu hakika umeongea jambo nadhani kila mmoja atafaidika na hii comment

Asante na karibu tena 🙏
 
Binadamu ni pande mbili kwa wakati mmoja

1. DARK SIDE

Hii ni sehemu ya wivu, hasira, tamaa, ubinafsi, kulipiza kisasi.
Ni ile sauti inayosema "chukua yako kwanza", "watalia wao".
Haitoweki. Iko ndani ya kila mtu.

2. RIGHT SIDE / LIGHT SIDE
Hii ni huruma, upendo, uaminifu, kutoa, kusamehe.
Ni ile sauti inayosema "msaidie", "fanya kilicho sahihi hata kama hakuna anayeona".

Kwa nini wengine wanapotea?

Kama ulivyosema kuna watu 2:

Carl Jung alisema: "Huwezi kufika nuru bila kwenda ndani ya giza lako kwanza"

Darkside navyoielewa, haimaanishi tu ubaya wa mtu anaotamani kuufanya kwa wengine ila Dark side yawezekana ikawa ni siri ya mtu alivyo ndani tofauti na anavyojionesha nje. Ni sawa na mtu ambaye kwa nje anayachukia mahusiano na kuyapinga ila punyeto kwake ni kama dozi

Hajamdhuru mtu, hajamkera mtu ila kuna sehemu yupo weak tofauti na watu nje wanavyomchukulia.

Back to the mada, watu wema ambao bado ni wema ni wachache sana sana sanaaa kwa sababu wengine hubadilishwa na dissapointments au maumivu baada ya watu kuuchukulia wema wake kama gap la kumtumia.

Ila kuna ambao hayo yote hayawabadilishi na kukutana na mtu wa aina hii. Kwa life time si ajabu ukakutana na mmoja, wawili, watatu na ukibahatika sana labda wanne.

Wengi wanafake kuwa wema ili wapate maslahi au wawatumie watu. Ila siku maslahi yasipopatikana, wanajivua gamba. Na hii yawezekana ikawa ndio idadi kubwa ya watu. Arifu watu wana roho mbaya sana
 
binafsi kitu kinachoanza kunistua kwamba huenda inawezekana kwa asilimia kubwa mtu niliyekutana nae eidha ana intensions mbaya na mimi ama inaweza isiwe intensions mbaya ila anataka kunitumia kwa hila ( taking advantage ) mapema sana nikiona mtu ananiiga hasa character yangu ama namna ninavyoyatizama mambo umakini unaongezeka juu ya mtu huyo. hiyo huwa ni sign yangu ya awali kabisa.
Ndio wale watu wanaojifanya wema sana kwako ila muhudumu wa bar au restaurant anamfokea ama kumtukana.

Mtu helpless na ambaye hajamfanyia chochote.

Watu wenye roho mbaya na wanaigiza wema huwa hawajifichi uhalisia wao pale wanaposema au wanapowatendea watu ambao hawana msaada kwao.

Na hiyo alert yako muhimu, nimeichukua pia maana ni dalili kuu ya manipulators
 
Back
Top Bottom