Hivi uongo ni ugonjwa au tabia tu mbaya ?

Manyanza

Platinum Member
Joined
Nov 4, 2010
Posts
20,346
Reaction score
49,161
Wakuu nimekuwa nikijiuliza bila hata kupata majibu .

Uongo unaweza kuwa ni ugonjwa au moja ya tabia tu mbaya ?

Kimsingi kila binadamu ana madhaifu yake anaweza akadanganya ili kuepuka aibu na wakati mwingine kutaka kujilinda, au kutafuta faida hasa kwenye ishu za pesa, na wakati mwingine mtu huongea uongo ili kuepuka adhabu, au mbaya zaidi mtu huongea uongo aonekanekana ni mtu mwenye sifa nzuri kwenye jamii.

Kuna wale ambao huongea uongo wa kulazimisha (pathological lying) Hasa ndugu zetu Wanasiasa na Machawa ambao hongea uongo wa waziwazi tena usio na faida yoyote na happ ndipo huwa nawaona wana matatizo fulani ya afya ya akili au kukosa utu kwa hali fulani

Nini mtazamo au mawazo yenu kuhusu ''UONGO " Je ni tabia mbàya au ni ugonjwa ?
 
Screenshot_2026-07-18_192650.jpg
 
Uongo ni sehemu ya maisha

Kuna viunzi huwezi kuviruka bila kutumia uongo yaani ni uache usiendelee au uendelee kwa kutumia uongo ndiyo maana hata kwenye masimulizi nabii Ibrahim au Abraham aliongopa nae

Kwahiyo uongo Upo ila vizuri usipitilize sana nataman kuendelea ila Mercedes yangu ishajazwa mafuta acha niondoke hapa
 
Hata ungesema ist sawa tuu mkuu!
 
Huna baya Tajiri
 
Kuna wakati ili upate jambo la muhimu ni lazima uongee uongo! Mfano ukimpenda demu lazima ujaze uongo zaidi ya ukweli ili umpate vinginevyo hutaweza kumvua chupi.
 
Uongo ni tabia mbaya... Imetoka kwa baba wa uongo ibilis na anatutoto twingi sasa hivi.
 
Nina rafiki yangu wa kike ni Muongo balaa,yaani anadanganya hata pasipo na sababu ya kudanganya...nimewahi muuliza hivi kwa nini huwa unadanganya?anasema basi tu hata sina sababu najikuta tu nimeshasema uongo....ni Tabia mbaya
 
Ni tabia mbaya kama utatumika kuharibu na nzuri kama utatumika kujenga
 
Uongo si ugonjwa ila unasababisha ugonjwa na uaribifu mkubwa katika familia jamii taifa hata ulimwengu kwa ujumla.
Ila uongo umesaidia sana watu wengi hapa duniani.
 
Wakuu nimekuwa nikijiuliza bila hata kupata majibu .

Uongo unaweza kuwa ni ugonjwa au moja ya tabia tu mbaya ?

Kimsingi kila binadamu ana madhaifu yake anaweza akadanganya ili kuepuka aibu na wakati mwingine kutaka kujilinda, au kutafuta faida hasa kwenye ishu za pesa, na wakati mwingine mtu huongea uongo ili kuepuka adhabu, au mbaya zaidi mtu huongea uongo aonekanekana ni mtu mwenye sifa nzuri kwenye jamii.

Kuna wale ambao huongea uongo wa kulazimisha (pathological lying) Hasa ndugu zetu Wanasiasa na Machawa ambao hongea uongo wa waziwazi tena usio na faida yoyote na happ ndipo huwa nawaona wana matatizo fulani ya afya ya akili au kukosa utu kwa hali fulani

Nini mtazamo au mawazo yenu kuhusu ''UONGO " Je ni tabia mbàya au ni ugonjwa ?
Uongo ni njia mbadala ya mlengwa kujitahidi kuufanyia mazingaombwe ubongo wako ukubaliane na mawazo hitajika kwa wakati husika.
 
Back
Top Bottom