Changamoto za kuoa ukiwa “Senior Bachelor”

Changamoto za kuoa ukiwa “Senior Bachelor”

Sasa unakuta mwanaume hana mashine anafua mwenyewe, anapika mwenyewe, anapasi mwenyewe, chakula chake kitamu kuliko cha wanawake wengi, anaosha vyombo mwenyewe, akienda shopping anajua viungo vyote hadi tenderriser na hasahau kutokununua hata kimoja.
Sufuria zake saafi anazisugua na steelware kuchwao, anapata wageni wa kike na wa kiume kila weekend, akienda kazini ana pack chakula alichopika yeye, Wanawake wake hawapiki anawapikia wanasubiria chakula chake huku wanaangalia +EVA. Anaalikwa kwenye sherehe anahudhuria hasahau.
Sasa huyu aoe ili iweje? Anachokosa nisex tu.
Bila kurahau Anakaa hadi kwenye mbuyi anakuna nazi, anaonja chumvi !!
 
Ma sinior bachelor waki oa ndoa zao zinakuwa stable kwa sababu hawana mambo mengi na focus yao ni kujenga familia.
Wanajua na wanaweza kuzikabili Changamoto za maisha.
Wana uvumilivu wa hali ya juu hususani kwenye kashikashi za mahusiano kwa sababu wameshapitia mengi huko nyuma.
Nawakumbusha vijana kwamba wasiowe kwa mihemko kwa sababu "ninge" huja mwisho wa safari
 
Mi changamoto kubwa niliyoipata ilikuwa ni kupenda, senior bacheloz always wanakuwa wamepita kwenye mahusiano mengi sana. Kwahiyo kupenda moyo ulishakufa kitambo hii inasababisha kigugumizi kwenye maamuzi yupi atakufaa kwa matumizi ya nyumban.
Ila changamoto nyingine ni kuacha makoloni yote na kuwa na mmoja kama njiwa. Hili ni tatizo kwakweli. Kwa wanaotaka kuoa au kuolewa fanyeni maamuzi mapema mtakuwa sugu kwenye mapenzi iwaletee shida kwenye maamuzi. Na kama unadate na senior bachelor ujue kuwa peke yako ni 2-10%tu
This is very true.
Thank you for sharing mkuu.
 
Ma sinior bachelor waki oa ndoa zao zinakuwa stable kwa sababu hawana mambo mengi na focus yao ni kujenga familia.
Wanajua na wanaweza kuzikabili Changamoto za maisha.
Wana uvumilivu wa hali ya juu hususani kwenye kashikashi za mahusiano kwa sababu wameshapitia mengi huko nyuma.
Nawakumbusha vijana kwamba wasiowe kwa mihemko kwa sababu "ninge" huja mwisho wa safari
Kinyume chake wengi wanasema mpaka umri huu hujaoa kuna tatizo mahali
 
changamoto kubwa kwangu mimi nimezoea kuishi mwenyewe, akija manzi tu gettoh akikaa week namchoka sababu kwanza nikipanga ratiba zangu muhimu nimzingatie na yeye, yaan mfano mda wa kurudi home, pia mara nyingi nikiwa home nahitaji kupumzika zaidi kuliko kuongea hii ni changamoto zaidi maana ukiwepo nyumban anataka story zaidi, Mungu anisaidie anibadilishe, maana pia nimekua mkosoaji mkubwa
Tena unakuta ule mda unaitaka kupumzika ndio anakuchokonoachokonoa. Ilisha nikuta sana hii
 
4. Senior bachelor's tumeshazoea that privacy, na vitu ndani ya nyumba viko katika sehemu sahihi, sasa baadhi ya wanawake wanakuja na issue Za kuosha vyombo vya breakfast pamoja na vya lunch, naona kama mwanamke kaja kusaidia mende kuzaliana
Kwa zaidi ya miaka 6 sasa sijawahi kupija. Ndani kwangu utakuta kikombe kimoja na kijiko kimoja tu. Tena kikombe chenyewe kimevunjika juzi. Hii no dawa tosha ya hao wanaojidai wanakuja kuosha vyombo. Ama wale wanaosema we nenda kazini utanikuta
 
Mimi nadhani mdada akigonga 30 tayari tumuite "senior spinster"!! Manake kama kidume kikigonga 36 ni senior, basi 6yrs difference mi sawa kabisa kumuita mdada senior
 
Back
Top Bottom