I hope ulimbwaga kwa sababu nyingine na siyo hii ya kukwambia "universal truth". Sasa baada ya kuwa msomi, una kazi, probably gari na nyumba na UKAONESHA KUMPENDA ni kwa nini binti asiseme "this is love"? Kuwa na vitu na upendo ni package kamili kila mwanamke anaitaka. Mwanamke akikwambia "nimekupenda wewe na si vitu vyako" muulize "mimi yupi?" Akishakutajia sijui ucheshi, ustaarabu, werevu, kipaji cha utunzi na macho mazuri muulize ungekuwa kapuku pamoja na traits zote hizo angekupenda? Akikwambia ndiyo muulize mngekutana wapi kwanza! Hata hayawani hachagui mwenzi dhaifu labda akose namna kabisa. Bibie akikukuta huna kitu na akakupenda basi ujue ana macho ya rohoni, ameona potential ndani yako na ana uwezo wa kusubiri izae. Sasa usisubiri kukutana na mwanamke mnafiki. Ukikutana na "ideal she" wako wewe songesha. Kwamba amekupenda kwanza ulivyo navyo kisha wewe au kinyume chake itakuwa siri yake na usalama wako.