Consultant_Silwano
Member
- May 22, 2017
- 74
- 33
Changamoto kubwa kwenye eneo la uhasibu na kodi kwa wanafanyabiashara wengi hasa wanaotumia mtindo kuagizisha mizigo mbalimbali kutoka nje ya nchi kwa kutumia Fedha za wateja kufanikisha au ku-facilitate biashara husika ,changamoto hizi hupelekea biashara au wafanyabiashara wengi wa mtindo tajwa hapo juu kupata madeni makubwa baada ya ukaguzi TRA ambao kisheria lazima ufanyike hivyo basi kama washauri wa kodi tumeona ni vema tuzibainishe na kuwasilisha ili kutoa uelewa au kukuwakumbusha wafanyabiashara wa eneo hili changamoto zao:
✅Kutotambua umuhimu uhasibu kwenye biashara, hii ni changamoto kubwa sana kwa wafanyabiashara wengi sana hasa kwa wafanyabiashara wanaotumia mtindo kuagizisha mizigo kutoka nje nchi kuja Tanzania, kutokana na kutojua au kutokua na elimu ya Uhasibu wafanyabiashara wengi sana wa kuagizisha mizigo Mara zote nimeona kwenye mitandao wanatumia namna mbalimbali kupokea malipo kutoka kwa wateja wao Kama vile namba za simu, lipa namba za mitandao ya simu, benki akaunti ambazo hawatofautishi kati akaunti za kupokea Fedha za wateja(Customers trust accounts), akaunti za Biashara (Business accounts). Kutokana na hili kosa la kutotofautisha malipo Fedha ya yanayopokewa kwenye akaunti mbalimbali za wafanyabiashara hivyo kusababisha biashara hizi zikifanyiwa ukaguzi na TRA na Mara nyingi wanafanyiwa ukaguzi wa lazima kitaalamu unaitwa Jeopard assessment ambao hupelekea kupewa assessment ya kodi kubwa sana kwani TRA huona Fedha zote walizopokea ni Kama mauzo ya biashara(Business sales or revenue).
✅Changamoto ya kutotunza rekodi za biashara(Business record keeping),hii pia ni changamoto kubwa sana kwa wafanyabiashara wengi sana wa mtindo wa kuagizisha,changamoto hii pia hupelekea changamoto nyingine kikodi ambayo huwafilisi au kuwaondolea utilivu katika biashara na ukizingatia kwa mujibu wa sheria nchini mfanya biashara binafsi mwenye mauzo yanayoanzia 100M (Non presumptive taxpayer) anatakiwa kufunga hesabu kila mwaka wa kodi na kwa biashara inayofanyika kwa mtindo wa kampuni ni lazima kufunga hesabu bila kuazingatia kigezo cha mauzo. Kwa sura ya biashara za kuagizisha TRA na kwa akili ya kawaida wote wanatakiwa kufunga hesabu kila mwaka na wengi hawana kumbukumbu za biashara na wala hawatambui wajibu huu hali inayopelekea kulipa kodi kubwa sana baada ya ukaguzi kutoka TRA.
✅Changamoto ya kutofuata na kutojua sheria, taratibu na miongozo mbalimbali ya kodi, hii ni changamoto kubwa sana kwa wafanyabiashara wa kuagizisha mizigo,wengi wao wanaanza tuu biashara bila kujua wajibu wa kikodi kutona na aina biashara wanazofanya na mara nyingi wanapata matatizo ya kikodi mara kwa mara kwa sababu vitu vingi vya kikodi vinatokea katikati ya Biashara Kama mshituko(surprise) ni kwa sababu ya kuanza biashara pasina kuwa taarifa na ushauri sahihi kwenye eneo la kodi.
✅Changamoto ya kupewa assessment ya kodi za lazima(Jeopardy assessment).
Wafanyabiashara wengi kuagizisha mizigo kutokana na kutofuata na kujua sheria, taratibu na miongozo mbalimbali ya kikodi wamekua wakipata changamoto kupewa assessment za kodi za biashara zao pasina kuwasilisha hesabu za biashara hii ni kutokana na kutojua wajibu wao kikodi mara nyingi hawajui ni nyakati gani ya kufanya makadilio, kiasi gani na kwa sababu ip, nyakati gani ya kuwasilisha hesabu za mwisho wa mwaka (Return of income) na kwasababu ip, vitu gani vya kuzingatiwa kabla na baada kuanza biashara, vilevile ata wakipewa wito na TRA mara nyingi mazingatio yanakua madogo sana na hatimaye wanapata matatizo makubwa sana kwenye biashara zao.
✅Changamoto ya kukosa washauri wenye sifa na weledi wa kutosha kwenye maeneo ya Uhasibu(Accounting), kodi(Tax), Ukaguzi(Auditing) na Business compliances. Hii pia imekua changamoto kubwa sana kwa wafanyabiashara wa mtindo wa kuagizisha bidhaa wengi wao hawayapi mazingatio ya kutosha maeneo niliyotaja juu kwa umuhimu unatakiwa kwani ndo maeneo muhimu kwa Ulinzi wa biashara yako bila kuzingatia maeneo niliyoyataja hapo juu ni sawa na kujaza maji kwa juhudi kwenye ndoo iliyotoboka kwakweli maji yatatoka na kuisha maana yangu biashara itafilisika ni suala la muda tuu.
Mwisho Naomba nimalizie kwa kusema biashara sio kununua na kuuza vilevile kuilinda.
Kwa mawasiliano zaidi:
Barua Pepe:
Momsconsultingltd@gmail.com
Namba:0712685025/0783262125
#Momsconsulting#Consultant_Silwano#Businessconsultant#Tax#Accounting#Auditing#Businesscompliances#Businessfaciltatioms