Challenge ya kusave pesa UTT

Challenge ya kusave pesa UTT

Sio kwa namna hiyo mkuu, na sio kuichungulia kuiona, kuishika na kuifanya iongezeke kwa namna niitakayo saa niitakayo.
Ni kweli ila kuishika hela napo ni risky pia.

Nenda soma tabia za hela na utaona jinsi gani UTT ni mkombozi.

Kuna njia nyingi za kuzalisha hela uliyonayo au unayomiliki.

Njia yako ni njia pia ila wewe unaangalia faida zaidi hujaangalia upande wa hasara.

Kwa upande mwingine mimi nimeangalia hasara na nikaona bora kupata faida kidogo ila nikaepukana na hasara kubwa.

Zote hizo ni njia za uwekezaji na zote zina gain tofauti na hasara tofauti.

📍High gain(Faida kubwa)=High risk( Hasara kubwa)

📍Low gain(Faida ndogo)=Low risk(Hasara ndogo)

📌KUPANGA NI KUCHAGUA!!!
 
I am speaking from personal experience as well.
I did the math and realized government bonds are far much better than UTT. However,having a portfolio that comebines the two is even better. Return zangu za bonds,nazimimina UTT.
Naomba ufafanuzi mkuu kwa hilo
 
Nipe risk zake mkuu, Kuna pesa niliweka nmb bonus nilitaka kuihamishia huko utt
Hujachelewa risk za UTT ni ndogo ndogo kuliko ambapo naweza kukueleza kuwa ili upate hasara ni pale nchi itakapofilisika au kuwe na anguko kubwa la kiuchumi duniani au pawe na Majanga makubwa ya kidunia.

Hivyo kwa muktadha huo ni salama zaidi kuwekeza UTT kwakua UTT wao wanaekeza kwenye soko la HISA na kwenye hati fungani za serikali ambazo ni za muda mrefu kufikia miak 25.

Wekeza kwenye mifuko ya LIQUID FUND na BOND FUND huko risks ni ndogo/lowest kwakuwa wanawekeza kwenye hati fungani za serikali.Wakati mifuko mingine iliyobaki risk ni moderate kwakuwa wanawekeza kweye mifuko ya hisa.

UTT intrest rate yake ni 12%-15% wakati kwa benki nyingi hapa nchini interest rate haivuki 9%.

Ukimfata mtu wa benki kumuomba ushauri atakupinga na kukushawishi uachane na mpango huo wa kujiunga UTT kwakuwa watu wa benki wanavutia kwao hizo pesa wanazihitaji ili waendelee kuzikopesha.

Na kuna malalamilo toka kwa watu wengi tu kuwa wanapoenda benki kutoa hela na kuziweka UTT huwa wanapata kausumbufu flani hivi ambako hakana msingi.So kama unampunga wa kutosha unaweza uchepusha kwa njia ya mtandaoni maana kila benki mpaka azam pesa wanayo huduma ya UTT. Au ukautoa huo mpunga kwa awamu.
 
Imagine nmb bonus account, mil 20 ndani ya miezi 8 inaongezeka 160k tu. Kwa utt hapo ingeongezeka ngapi?
 
Usiwaamshe waliolala watu tupo tunachungulia tu daily maximization of kibunda pale mjini UTT

Baadaye wataanza kutuita freemason

Sent from my TECNO KG5j using JamiiForums mobile app
Hii ni sadaka yangu kwa watu wangu.Sio vyema kuona vijana wenye nguvu wanagongea jerojero maskani.

Wengine wanawaza kila akipata hela akazikomoe mbususu😀😀😀

Kijana wa kiume kwanzia miaka 25-35 kwa nchi yetu anawaza ngono 24/7.A change in mindset and ideology must be made.Pia watu wafundishwe FINANCIAL EDUCATION(ELIMU YA FEDHA).

Vijana wanajitutumua kuwamiliki wanawake,kuwahonga na kwenda kwenye mabaa na maclub kuwaspoil wakati hawana investment yoyote ya maana.Taifa linaangamia kwa kukosa maarifa.

Vijana wa kike wanajitahidi hela zao wanafanya ya maana kwa kiasi flani japo nao kuna mambugira wanawaza kutumia tu bila kutengeneza mirija ya pesa.

Na bahati mbaya wanaume hatuamini katika kucheza vikoba bora kwa wanawake wanacheza, ila sijawahi kuvielewa na kuona faida yoyote ya hivyo vikoba bora UTT.

Mimi ni mgumu sana kumpa mtu hela huwa nIna desturi ya kumuonyesha njia za kuipata.Kutoa hela yangu nasikia uchungu sana🤗🤗🤗
 
Imagine nmb bonus account, mil 20 ndani ya miezi 8 inaongezeka 160k tu. Kwa utt hapo ingeongezeka ngapi?
Screenshot_20250810-090700_1.jpg

Hiyo ni hesabu ya mwaka kwa lowest intrest rate 12%
 
nenda maendeleo
UUnswekezaunapewafaidayakosameday
Ubaki na akilizako ukimaliza mwaka unachukua.mzigo wako wa Faidakamakawaidaa
Andika vizuri basi kaka tukuelewe huenda unahoja ya msingi
 
shida risk hamuongelei mkuu, mnazungumzia upande wa faida tu. Bank usalama wa amana yangu upo 100%. Vp upande huo? Tupeni elimu wakuu. Tunaelekea uzeeni hiki sio kipindi cha kufanya makosa
Hakuna kitu kisichokuwa na risk kiongozi, risk zake ni ndogo sana Ukilinganisha na namna nyingine za kulinda & kuongeza thamani ya fedha yako.
 
shida risk hamuongelei mkuu, mnazungumzia upande wa faida tu. Bank usalama wa amana yangu upo 100%. Vp upande huo? Tupeni elimu wakuu. Tunaelekea uzeeni hiki sio kipindi cha kufanya makosa
UTT ni taasisi inayofahamika na serikali na mtaji walipewa na serikali na uwekezaji wake unafanywa katika misingi na sheria za BOT na wizara ya fedha.

Kama hujaridhika au unawasiwasi fika makao makuu yao pale posta Dar-es-Salaam jengo la SUKARI HOUSE utapewa darasa/elimu bure na utajibiwa maswali yako yote.
 
Imagine nmb bonus account, mil 20 ndani ya miezi 8 inaongezeka 160k tu. Kwa utt hapo ingeongezeka ngapi?
Duuh watu mnautajiri alafu mnauchezea , hiyo kwa kila mwezi unaingiza 200k - miezi 8 ungekuwa 1.6M faida sasahivi na maongezeko kibao. Cheki mfano huo hapo chini watu walivyo na hasira , mtu ana kamilioni tano kake ana maswali kibao anaona kama anaibiwa , cheki watu walivyo na salio chini hapo na hawazi kuibiwa , that why masikini ataendelea kuwa masikini na tajiri atazidi kuwa tajiri
 
Attachments

  • _20250119_080531.JPG
    _20250119_080531.JPG
    111.8 KB · Views: 25
shida risk hamuongelei mkuu, mnazungumzia upande wa faida tu. Bank usalama wa amana yangu upo 100%. Vp upande huo? Tupeni elimu wakuu. Tunaelekea uzeeni hiki sio kipindi cha kufanya makosa
Mkuu ata usiogope list yake ni ndogo sana kupoteza pesa zako.
 
-Mimi nashauri diversification kwenye investment, like Utt, mashamba, viwanja, biashara, hisa,
Umeongea point , mimi Utt niliifahamu toka mwaka jana mwezi wa nne - then nikaanza kufanya utafiti wangu nje ndani kwasababu waga sikurupukii vitu na ikanichukua miezi mitatu kuielewa vzr , then mwezi wa nane mwaka jana rasmi nikaanza ku invest , nimekimbiza mpaka mwaka huu mwezi wa nane nilikuwa na jumla ya shilingi 13Million , juzi nimetoa 7Million nimenunua hisa za CRDB kwahiyo mdogo mdogo nimeanza kufanya uwekezaji mseto nachanganya huku na huku
 
hiyo risk ndogo ndio uniambie ni ipi mkuu. Maana serikali yetu tunaijua kila kiongoz anaeingia anakuja na matamko yake
Kuna wadau hapo juu wamekufafanulia vzr , moja kuna sheria ambayo inalinda hii mifuko na serikali haiwezi kuingilia wala kufanya chochote isipokuwa kutengeneza mazingira wezeshi tu ,pili uhakika wa kuendelea kupata faida - kwasababu wanawekeza kwenye biashara ambazo ni uhakika wa interest mfano bonds za benki kuu na bonds za mabenki.Ndio maana taasisi kama UTT ilianza toka mwaka 2003 hivi na leo ina miaka zaidi ya 22 sokoni , ila ajabu inapiga kazi miaka yote hiyo na hakuna ambaye amewahi kuripoti kuibiwa wala kutapeliwa.
 
Back
Top Bottom