TANZIA Chaki (Jaffar Kasmali) mchezaji wa Cosmopolitan na timu ya taifa amefariki leo New York

Mohamed Said

JF-Expert Member
Nov 2, 2008
20,921
30,266
CHAKI (JAFFAR KASMALI) MCHEZAJI WA COSMOPOLITAN NA TIMU YA TAIFA AMEFARIKI LEO NEW YORK
Chaki alikuwa golikipa hodari wa Cosmo katika miaka ya 1960 wakati huo wachezaji wenzake ninaowakumbuka walikuwa Msuba, Mansur Magram, Mustafa Mabuge, Emil Kondo, Kitwana Popat (Kitwana Manara) ni miaka mingi sana majina yanakuja lakini sina hakika kama hawa walikuwa pamoja na Chaki.

Chaki aliacha kucheza golini na kuhamia kucheza mbele na nafasi yake golini ilichukujliwa na Kitwana Popat kama alivyokuwa akijulikana miaka hiyo.

Kitwana alicheza golini Cosmo na Timu ya Taifa ya Tanganyika na Chaki alicheza kama mshambuliaji katika Timu ya Taifa akicheza na wachezaji wa wakati ule kama John Limo, Mbwana Bushiri, Sembwana, Awadh Matesa, Abdallah Aziz, Miraji, kwa kuwataja wachache.

Chaki aliondoka Tanzania miaka hiyo ya 1960 katikati na kwenda Amerika.
Hakusikika tena hapa nyumbani.

Nilifika New York mwaka wa 2011 na nikamuuliza mwenyeji wangu Abdillah Rijal kutoka Zanzibar kama anawajua Chaki na Nanji vijana kutoka Dar es Salaam ya miaka ya 1960s.

Alikuwa wote anawafahamu na watu maarufu katika jumuia ya Watanzania pale New York akaniambia Chaki na Nanji wote wakisomesha vyuo vikuu.

Nakumbuka nilimwambia Abdillah Rijal kuwa mara ya mwisho kumuona Chaki ilikuwa Dar es Salaam baada ya mechi ya Cosmo na Chaki alikuwa anarejea nyumbani kwao Upanga anaendesha baiskeli yake ''sports.''

Nyumba ya akina Chaki ilikuwa United Nations Road nyumba yao mkono wa kulia ikitazamana na Msikti wa Tambaza.

Baiskeli ya Chaki ilikuwa aina ya baiskeli ambazo mwendeshaji anainama kufikia usukani wa baiskeli na zikitumika katika mashindano ya mbio za baiskeli.

Zilikuwa basikeli maarufu kwa vijana khasa ambao walikuwa wanatoka familia za kujiweza.
Nakumbuka kijana mwingine ambae alikuwa na baiskeli kama hii alikuwa Sauti Plantan, mtoto wa Thomas Plantan.

Siku ile ile Abdillah Rijal akampigia simu Chaki Long Island alipokuwa akiishi akamwambia kuwa kuna mtu katoka Tanzani kakuuliza na kasema mara ya mwisho kukuona ulikuwa unaendesha baiskeli yako ''sports.''
Chaki alimwambia Ahmed kuwa huyo mtu atakua ananijua sana maana kakumbuka hadi baiskeli yangu.
Hivyo ndiyo Chaki na Ahmed walipopanga tusali Ijumaa pamoja katika msikiti wao Manhattan si mbali na Makao Makuu ya UN.

Chaki alifurahi sana kuniona na alishangaa nilipomuuliza nduguye Polly yuko wapi.
Huyu Polly alikuwa mshoni bingwa wa vipaji vyote kuanzia nguo za kike hadi za kiume.
Hii ilikuwa katika miaka ya 1970.

Polly alikuwa anashona Mtaa wa Uhuru mbele Mtaa wa Livingstone na alikuwa na mafundi hodari sana.
Baada ya kusali Ijumaa pale tulikwenda kula chakula cha mchana kwenye restaurant yao wanayoipenda.
Chaki aliniuliza maswali mengi sana kuhusu wachezaji mpira wa nyakati zake waliokuwa Cosmo, Yanga, Sunderland na Timu ya Taifa.

Chaki alikuwa anaingiwa na huzuni sana ninapomwambia kuwa fulani kafariki.
Inaelekea hakuwa na taarifa nyingi za nyumbani.

Nikamuahidi kumpatia picha za enzi zake za mpira na hili nililifanya.
Furaha yake haikusemeka.

''Mohamed nasikia wewe msomaji sana wa vitabu nataka nikupe container zima la vitabu uendenavyo nyumbani.''

Chaki hakuwa anafanya maskhara alikuwa na nia khasa ya kunipa container moja la vitabu nilipakie lije Tanzania.

Yeye kama mwalimu alikuwa na vitabu vingi sana alivyokusanya.

Chaki alinikaribisha nyumbani kwake Long Island lakini bahati mbaya sikuweza kufika.

Chaki aliniambia kuwa hilo jina la ''Chaki'' si jina lake alipewa na mama mmoja ambae alikwenda kumuona mama yake baada ya mama yake kujifungua yeye.

Alipokuwa anamtazama mtoto akasema, ''Huyu mtoto ana rangi ya chocolate.''
Basi hiyo ''chocolate,'' ikageuzwa ikawa ''chaki'' na hilo jina likamganda.

Mimi hilo jina la Jaffar Kasmali nimelisikia hapo New York sikuwa nalijua kabisa na naamini si wengi wakilijua.

Leo nilitembelewa na mgeni kutoka Marekani na tulipokuwa tunaagana akaniuliza kama namjua Chaki; akanipa taarifa ya kifo chake akaniambia kimetokea muda mfupi uliopita.

Allah amsamehe makosa yake na amtie mahali pema peponi.
Amin.

PICHA:
Chaki tukiwa nje ya msikiti baada ya Sala ya Ijumaa New York na picha ya pili Chaki ni wa pili kutoka kushoto akiwa katika Timu ya Taifa ya Tanganyika.

Kwanza kulia ni Hemed Seif, Mbwana Abushiri, Awadh Matesa, John Limo...

1693079498748.png

1693079544730.png

Dr.
NImezungumza swali la bandari labda limekupita.
Ikiwa nitaona In Shaa Allah nitakuwekea hapa.
"Hii wananchi wengi..."

Huu wingi nini kipimo chao?

Nauliza swali hili kwa kuwa wanaoonekana kupinga ni kutoka sehemu moja.

Kuna kundi kubwa liko nje na kimya.

Hii hali ikoje?

Je, umefika wakati kundi hili nalo likajitokeza kueleza msimamo wao?
 
Kundi la watazamaji lilkiingia uwanjani kucheza mpira nani atashangilia goli.
 
CHAKI (JAFFAR KASMALI) MCHEZAJI WA COSMOPOLITAN NA TIMU YA TAIFA AMEFARIKI LEO NEW YORK
Chaki alikuwa golikipa hodari wa Cosmo katika miaka ya 1960 wakati huo wachezaji wenzake ninaowakumbuka walikuwa Msuba, Mansur Magram, Mustafa Mabuge, Emil Kondo, Kitwana Popat (Kitwana Manara) ni miaka mingi sana majina yanakuja lakini sina hakika kama hawa walikuwa pamoja na Chaki.

Chaki aliacha kucheza golini na kuhamia kucheza mbele na nafasi yake golini ilichukujliwa na Kitwana Popat kama alivyokuwa akijulikana miaka hiyo.

Kitwana alicheza golini Cosmo na Timu ya Taifa ya Tanganyika na Chaki alicheza kama mshambuliaji katika Timu ya Taifa akicheza na wachezaji wa wakati ule kama John Limo, Mbwana Bushiri, Sembwana, Awadh Matesa, Abdallah Aziz, Miraji, kwa kuwataja wachache.

Chaki aliondoka Tanzania miaka hiyo ya 1960 katikati na kwenda Amerika.
Hakusikika tena hapa nyumbani.

Nilifika New York mwaka wa 2011 na nikamuuliza mwenyeji wangu Abdillah Rijal kutoka Zanzibar kama anawajua Chaki na Nanji vijana kutoka Dar es Salaam ya miaka ya 1960s.

Alikuwa wote anawafahamu na watu maarufu katika jumuia ya Watanzania pale New York akaniambia Chaki na Nanji wote wakisomesha vyuo vikuu.

Nakumbuka nilimwambia Abdillah Rijal kuwa mara ya mwisho kumuona Chaki ilikuwa Dar es Salaam baada ya mechi ya Cosmo na Chaki alikuwa anarejea nyumbani kwao Upanga anaendesha baiskeli yake ''sports.''

Nyumba ya akina Chaki ilikuwa United Nations Road nyumba yao mkono wa kulia ikitazamana na Msikti wa Tambaza.

Baiskeli ya Chaki ilikuwa aina ya baiskeli ambazo mwendeshaji anainama kufikia usukani wa baiskeli na zikitumika katika mashindano ya mbio za baiskeli.

Zilikuwa basikeli maarufu kwa vijana khasa ambao walikuwa wanatoka familia za kujiweza.
Nakumbuka kijana mwingine ambae alikuwa na baiskeli kama hii alikuwa Sauti Plantan, mtoto wa Thomas Plantan.

Siku ile ile Abdillah Rijal akampigia simu Chaki Long Island alipokuwa akiishi akamwambia kuwa kuna mtu katoka Tanzani kakuuliza na kasema mara ya mwisho kukuona ulikuwa unaendesha baiskeli yako ''sports.''
Chaki alimwambia Ahmed kuwa huyo mtu atakua ananijua sana maana kakumbuka hadi baiskeli yangu.
Hivyo ndiyo Chaki na Ahmed walipopanga tusali Ijumaa pamoja katika msikiti wao Manhattan si mbali na Makao Makuu ya UN.

Chaki alifurahi sana kuniona na alishangaa nilipomuuliza nduguye Polly yuko wapi.
Huyu Polly alikuwa mshoni bingwa wa vipaji vyote kuanzia nguo za kike hadi za kiume.
Hii ilikuwa katika miaka ya 1970.

Polly alikuwa anashona Mtaa wa Uhuru mbele Mtaa wa Livingstone na alikuwa na mafundi hodari sana.
Baada ya kusali Ijumaa pale tulikwenda kula chakula cha mchana kwenye restaurant yao wanayoipenda.
Chaki aliniuliza maswali mengi sana kuhusu wachezaji mpira wa nyakati zake waliokuwa Cosmo, Yanga, Sunderland na Timu ya Taifa.

Chaki alikuwa anaingiwa na huzuni sana ninapomwambia kuwa fulani kafariki.
Inaelekea hakuwa na taarifa nyingi za nyumbani.

Nikamuahidi kumpatia picha za enzi zake za mpira na hili nililifanya.
Furaha yake haikusemeka.

''Mohamed nasikia wewe msomaji sana wa vitabu nataka nikupe container zima la vitabu uendenavyo nyumbani.''

Chaki hakuwa anafanya maskhara alikuwa na nia khasa ya kunipa container moja la vitabu nilipakie lije Tanzania.

Yeye kama mwalimu alikuwa na vitabu vingi sana alivyokusanya.

Chaki alinikaribisha nyumbani kwake Long Island lakini bahati mbaya sikuweza kufika.

Chaki aliniambia kuwa hilo jina la ''Chaki'' si jina lake alipewa na mama mmoja ambae alikwenda kumuona mama yake baada ya mama yake kujifungua yeye.

Alipokuwa anamtazama mtoto akasema, ''Huyu mtoto ana rangi ya chocolate.''
Basi hiyo ''chocolate,'' ikageuzwa ikawa ''chaki'' na hilo jina likamganda.

Mimi hilo jina la Jaffar Kasmali nimelisikia hapo New York sikuwa nalijua kabisa na naamini si wengi wakilijua.

Leo nilitembelewa na mgeni kutoka Marekani na tulipokuwa tunaagana akaniuliza kama namjua Chaki; akanipa taarifa ya kifo chake akaniambia kimetokea muda mfupi uliopita.

Allah amsamehe makosa yake na amtie mahali pema peponi.
Amin.

PICHA:
Chaki tukiwa nje ya msikiti baada ya Sala ya Ijumaa New York na picha ya pili Chaki ni wa pili kutoka kushoto akiwa katika Timu ya Taifa ya Tanganyika.

Kwanza kulia ni Hemed Seif, Mbwana Abushiri, Awadh Matesa, John Limo...

Islamic fundamentalist, wewe na Faiza hamnaga kitu kingine cha kuongelea zaidi ya uislamu na waislamu. Unaumiza nafsi yako bure dunia haiwezi kuwa unavyotaka wewe
 
Tuletee story zako za Upagani na wapagani nazo tutasoma

unataka kujipa jukumu la kuamua nini azungumzie wewe kama nani? nyie ndio mlijifungia watu kadhaa mkaja na story Watanzania hawataki hiki wanataka kile…
 
Nitaleta story za wapagani wa kiarabu
 
Pole sana kwa umma wa kiislamu kwa kifo cha chaki nakumbuka nyerere alimfanyia dhulma kubwa sana 😭😭😭😭😭
 
CHAKI (JAFFAR KASMALI) MCHEZAJI WA COSMOPOLITAN NA TIMU YA TAIFA AMEFARIKI LEO NEW YORK
Chaki alikuwa golikipa hodari wa Cosmo katika miaka ya 1960 wakati huo wachezaji wenzake ninaowakumbuka walikuwa Msuba, Mansur Magram, Mustafa Mabuge, Emil Kondo, Kitwana Popat (Kitwana Manara) ni miaka mingi sana majina yanakuja lakini sina hakika kama hawa walikuwa pamoja na Chaki.

Chaki aliacha kucheza golini na kuhamia kucheza mbele na nafasi yake golini ilichukujliwa na Kitwana Popat kama alivyokuwa akijulikana miaka hiyo.

Kitwana alicheza golini Cosmo na Timu ya Taifa ya Tanganyika na Chaki alicheza kama mshambuliaji katika Timu ya Taifa akicheza na wachezaji wa wakati ule kama John Limo, Mbwana Bushiri, Sembwana, Awadh Matesa, Abdallah Aziz, Miraji, kwa kuwataja wachache.

Chaki aliondoka Tanzania miaka hiyo ya 1960 katikati na kwenda Amerika.
Hakusikika tena hapa nyumbani.

Nilifika New York mwaka wa 2011 na nikamuuliza mwenyeji wangu Abdillah Rijal kutoka Zanzibar kama anawajua Chaki na Nanji vijana kutoka Dar es Salaam ya miaka ya 1960s.

Alikuwa wote anawafahamu na watu maarufu katika jumuia ya Watanzania pale New York akaniambia Chaki na Nanji wote wakisomesha vyuo vikuu.

Nakumbuka nilimwambia Abdillah Rijal kuwa mara ya mwisho kumuona Chaki ilikuwa Dar es Salaam baada ya mechi ya Cosmo na Chaki alikuwa anarejea nyumbani kwao Upanga anaendesha baiskeli yake ''sports.''

Nyumba ya akina Chaki ilikuwa United Nations Road nyumba yao mkono wa kulia ikitazamana na Msikti wa Tambaza.

Baiskeli ya Chaki ilikuwa aina ya baiskeli ambazo mwendeshaji anainama kufikia usukani wa baiskeli na zikitumika katika mashindano ya mbio za baiskeli.

Zilikuwa basikeli maarufu kwa vijana khasa ambao walikuwa wanatoka familia za kujiweza.
Nakumbuka kijana mwingine ambae alikuwa na baiskeli kama hii alikuwa Sauti Plantan, mtoto wa Thomas Plantan.

Siku ile ile Abdillah Rijal akampigia simu Chaki Long Island alipokuwa akiishi akamwambia kuwa kuna mtu katoka Tanzani kakuuliza na kasema mara ya mwisho kukuona ulikuwa unaendesha baiskeli yako ''sports.''
Chaki alimwambia Ahmed kuwa huyo mtu atakua ananijua sana maana kakumbuka hadi baiskeli yangu.
Hivyo ndiyo Chaki na Ahmed walipopanga tusali Ijumaa pamoja katika msikiti wao Manhattan si mbali na Makao Makuu ya UN.

Chaki alifurahi sana kuniona na alishangaa nilipomuuliza nduguye Polly yuko wapi.
Huyu Polly alikuwa mshoni bingwa wa vipaji vyote kuanzia nguo za kike hadi za kiume.
Hii ilikuwa katika miaka ya 1970.

Polly alikuwa anashona Mtaa wa Uhuru mbele Mtaa wa Livingstone na alikuwa na mafundi hodari sana.
Baada ya kusali Ijumaa pale tulikwenda kula chakula cha mchana kwenye restaurant yao wanayoipenda.
Chaki aliniuliza maswali mengi sana kuhusu wachezaji mpira wa nyakati zake waliokuwa Cosmo, Yanga, Sunderland na Timu ya Taifa.

Chaki alikuwa anaingiwa na huzuni sana ninapomwambia kuwa fulani kafariki.
Inaelekea hakuwa na taarifa nyingi za nyumbani.

Nikamuahidi kumpatia picha za enzi zake za mpira na hili nililifanya.
Furaha yake haikusemeka.

''Mohamed nasikia wewe msomaji sana wa vitabu nataka nikupe container zima la vitabu uendenavyo nyumbani.''

Chaki hakuwa anafanya maskhara alikuwa na nia khasa ya kunipa container moja la vitabu nilipakie lije Tanzania.

Yeye kama mwalimu alikuwa na vitabu vingi sana alivyokusanya.

Chaki alinikaribisha nyumbani kwake Long Island lakini bahati mbaya sikuweza kufika.

Chaki aliniambia kuwa hilo jina la ''Chaki'' si jina lake alipewa na mama mmoja ambae alikwenda kumuona mama yake baada ya mama yake kujifungua yeye.

Alipokuwa anamtazama mtoto akasema, ''Huyu mtoto ana rangi ya chocolate.''
Basi hiyo ''chocolate,'' ikageuzwa ikawa ''chaki'' na hilo jina likamganda.

Mimi hilo jina la Jaffar Kasmali nimelisikia hapo New York sikuwa nalijua kabisa na naamini si wengi wakilijua.

Leo nilitembelewa na mgeni kutoka Marekani na tulipokuwa tunaagana akaniuliza kama namjua Chaki; akanipa taarifa ya kifo chake akaniambia kimetokea muda mfupi uliopita.

Allah amsamehe makosa yake na amtie mahali pema peponi.
Amin.

PICHA:
Chaki tukiwa nje ya msikiti baada ya Sala ya Ijumaa New York na picha ya pili Chaki ni wa pili kutoka kushoto akiwa katika Timu ya Taifa ya Tanganyika.

Kwanza kulia ni Hemed Seif, Mbwana Abushiri, Awadh Matesa, John Limo...

Unavyosimuliaga mitaa ya Dar huwa najikuta kama naiona Dar hivi usoni kwangu!
 
Back
Top Bottom