Bongo new york ( album ya soggy doggy)

Feb 6, 2024
40
50
SOGGY DOGGY ANTER.

Jamvi la Ukwaju wa Kitambo lilibahatika kupiga stori na Msanii mkongwe katika Game ya Bongo fleva soggy doggy.

Tulibahatika kuzungumza mengi ila kwa faida ya wafuatiliaji wa page hii ya "ukwaju wa kitambo"

Mazungumzo hayo ni kama ifuatavyo:

Ukwaju wa Kitambo :-

brother soggy doggy hivi album Yako ya Bongo New York ilitoka mwaka gani.

Lakini pia unaweza kutukumbusha ni nyimbo zipi zilipatikana katika hiyo Album ( side A & B )

Sogg doggy :_-

Bongo New York ilitoka mwaka 1999, nilirekodi FM Srudio Enzi hizo ikiwa Mnazi mmoja. Sikumbuki majina ya nyimbo zote na haziko kokote

1.Clap your hands Feat.Mr Paul

2.Kifo Remix Feat.Remmy Ongala

3.I love you too Feat.Unique Sisters

4.Maisha ya ghetto Feat.BDP

Ukwaju wa Kitambo :- @Sogggy Doggy sory kuna stori kibao nilikuwa nasikia vijiweni kwamba way back in 1990s wasanii ili afanye show nae ilimpasa kulipa kiingilio kama mshabiki wa kawaida anapolipa kiingilio kutazama show..

Sogggy Doggy: Yes ilikuwa kawaida hiyo labda aliyeandaa disco awe anakujua

Ukwaju wa kitambo :- Duuh hatari sana vp na show ikiisha unapewa stahiki zako ilihali kiingilio ulilipa

Sogggy Doggy: Hakukuwa na stahiki (malipo)

( katika picha)

Katika hilo bango yuko Adili Hisabati enzi hizo akiitwa "RUFFNEC THE LUNATIC" akiitwa hivyo, pia yuko marehemu Cpwaa hapo kitambo akiitwa Crazy Power

Sogggy Doggy: Cpwaa na Adili walikuwa watu wabaya sana

Ukwaju wa Kitambo : H & F promotion waandaji wa hii show walikuwa wanafanya kila mwaka kama ilivyokuwa " fiesta " au lilikuwa ni concert tu ya muda ( iliandaliwa kwa sababu ya jambo fulani maalumu).

Soggy doggy :-
Hata waandaaji siwakumbuki, zamani Mbeya kulikuwa kama ndio home ya Rap...mji ulikuwa na mashindano ya kila mara ya rappers na upinzani ulikuwa mkubwa mno

Ukwaju wa Kitambo :-

Naona hapo katika Tangazo wamewataja kuwa ndio waandaaji wa hiyo show..

Baadae A town nao wakaja kwa kasi ( maana wasanii wengi wanaofanya hip hop wametoka A town) Arusha..

Sogggy Doggy: Hakuna takwimu sahihi, labda kwa umri wako.Nakutajia wachache niliokuwa nao Mbeya na niliojua baadae kama wametoka huko.

1.Soggy
2.Sugu
3.Weusi Wagumu Asilia (Fresh F)
4.Profesa Jay
5.Mchizi Moxie
6.Jay Moe
7.Jaffarie
8.Adili The Hisabati
9.Cpwaa
10.KBC (Kwanza Unit)
11.Terry Fanani (Hard Blasters)
12.Zay B
13.Mike Tee
14.AY
15.Quick Rocka
16.Izzo Business
17.Nay wa Mitego
18.Young D

Nimewasahau Uswahilini Matola
& marehemu Vivian wa Complex na Computer wa BDP

Ukwaju wa Kitambo :-

Mbeya kiukweli ni noma mpaka Sasa ila hii mikoa mingine ya Mwanza na Arusha inapewa tag coz wasanii wao wa HIP HOP wako Mainstream bt hata Sasa ukilifuatilia lile kundi la Makanta" ni noma sana Kuna vichwa mule vinapiga real HIP HOP ambayo huwezi ikuta mikoa mingine" pia Kuna kina Salu tee, Azma, Lugombo, Jada" Inshort Green wapewe Heshima Yao, mi nimekaa sana Mwanza Hakuna sana Harakati kama nazozionaga kwa mbeya " kwaiyo mwanza na Arusha ni airtime tu bt uhalisia uko Mbeya🖐🏿

.Vip kuhusu bei ya kiingilio Msanii alipaswa kulipa tsh. Ili afanye show au ilitengemeana na ukubwa wa show husika.

Sogggy Doggy: Kiingilio hakikuwa tofauti na wanacholipa wengine, vyote sawa tu ila katikati ya disco ndio msanii unaomba mic 🎤 unaimba

Nimekaa Mbeya, Arusha, Mwanza, Iringa, Lindi, Dar na kwetu Kagera....ila nikimsikia mtu anaifananisha Mbeya na mkoa wowote kimuziki namshangaa.

Ukisema kwenye mainstream je ni mwaka gani maana wakati mimi na Sugu tunavuma hakukuwa na mwanamuziki yoyote Arusha aliyekuwa anavuma

Ukwaju wa kitambo:-
Vip show za kutafutwa na promota kwa upande wako ziliaza lini ?

Vip kuna promota ambaye mlikubaliana inshu za malipo na yenye kiasi Fulani cha fedhaa ila cha ajabu kabla ya show jamaa akatembea zake. na wewe una maliza kufaya show unakuta nje hakuna mtu!

Sogggy Doggy:- Sikumbuki miaka ila kwenye 1997 hivi, promota kukimbia ilikuwa kawaida sana🤣🤣🤣🤣

Ukwaju wa Kitambo :- hivi katika Album inaitwa washgaji wenye vipaji kuna Msanii mmoja anaitwa Da Jo na shahuku ya kufahamu harakati zake ..

Ingawa nimeona brother soggy doggy ulikuwa na ukaribu zaidi na raper zay b kwa wasanii wa kike waliofanya muziki enzi hizo

Sogggy Doggy: Da Jo nakumbuka alikuwa anakaa Kigamboni, alikuwa mshkaji ila sio sana.

Zay B alinitangulia darasa moja Meta Secondary Mbeya so alikuwa mshkaji shule na ndio maana niliandika verse yake ya Gado pamoja na kutengeneza beat ila nimekuwa karibu zaidi na Dataz (dada yake Squeezer) ambaye nae nilikuwa namwandikia

Ukwaju wa kitambo :- eti ni kweli katika Simu Yangu ya Solo, yale maneno kwamba Simu yako ndiyo aliyotumia Caz T kumtongozea Dokii ama ni katika kutafuta urari wa vina? 😂😂😂🙌🙌🙌

Sogggy Doggy: Ni kweli
, simu yangu haina dola
Mambo ya Buzz😄
UKWAJU WA KITAMBO :-

@Sogggy Doggy vip ile track yako " nilisoma nae " ni true story au sehemu ya uandishi tu katika fasihi simulizi.

Sogggy Doggy: 70% kweli

Ukwaju wa kitambo :- bro hivi hii ngoma ni line gani ambayo ww mwenyewe unaipenda(ambayo unasema enhe hii line kali.

Sogggy Doggy: Wimbo gani
Ukwaju wa Kitambo :- Simu yangu ya Solo.

Sogggy Doggy: Usipige simu usiku nitakuwa nimeishalewa/
Majibu ntakoyokupa utashindwa kunielewa

Ni simu yangu tu alotumia caz t kumtongozea dokii nikawa bar usinipigie siskii 😄🙌

Ukwaju wa Kitambo :-

Pia mimi naona wasanii wa zamani pia ndio walioiheshimisha na ndumu pia..wengi ndumu walikuwa wanaidharau lakini wasanii walikuwa wanapiga lakini wanaandika vitu vya maana mwishowe ndumu ikaonekanika ni ya kawaida

Soggy :- ndio

.................................

Asante brother soggy doggy tutakuchek tena next time:.
FB_IMG_1709975239863.jpg
 

Attachments

  • FB_IMG_1709975248910.jpg
    FB_IMG_1709975248910.jpg
    31.9 KB · Views: 4

Similar Discussions

Back
Top Bottom