CHADEMA yatangaza uchaguzi wa kujaza nafasi za waliotimuliwa Bawacha

Sio kweli maamuzi ya mkutano mkuu hayajafanyika bado wanachama halali na watambwaga Mbowe na kamati kuu yake mapema tu

Sema Mbowe anafanya kusudi kuvuruga mchakato sababu keshavuta pesa ya kila mwezi kutoka kwa hao wabunge anataka tu kuzusha mgogoro wa kisheria sababu wale wamekata rufaa kikatiba.Kikao cha kikatiba waluchokata rufaa hakijaketi kuamua yeye ansitisha uchaguzi mmmmm ni fix tupu hapo
Unacho kiweza ni kuuza visheti tu
 
Baraza la wanawake wa Chadema ( BAWACHA ) , limetangaza rasmi kuanza mchakato wa kujaza nafasi za Wasaliti waliotimuliwa ndani ya Chama wakiongozwa na Halima Mdee .

Fomu za Kugombea nafasi hizo za uongozi wa Bawacha Taifa zinapatikana kwenye ofisi za Mikoa za Chadema , ofisi za Kanda zote na ofisi ya Bawacha Makao Makuu , DSM , ambapo wanawake wote wa Chadema wenye uwezo wanaombwa kuchangamkia nafasi hizo Muhimu na zenye heshima kubwa .

Form zinaanza kutolewa tarehe 25 february 2021 ambapo zoezi la kuchukua na kurejesha form hizo litadumu hadi tarehe 3 March 2021 saa 10 jioni .

View attachment 1711946

Mungu ibariki Chadema
Hivi mtu anasemaje eti walio saliti chama

Chadema hii ya kisanii? Yamkini kabisa kabisa wasaliti ni walio baki,ni vile tu waTanzania wengi ni vipofu
 
Hivi mtu anasemaje eti walio saliti chama

Chadema hii ya kisanii? Yamkini kabisa kabisa wasaliti ni walio baki,ni vile tu waTanzania wengi ni vipofu
Wewe endelea kuwaramba miguu wanao kupatia mkate wako wa kila siku
JamiiForums1992601550.jpg
 
Mdee kwisha habari yake dadadeq. Sasa kwenye CCM hatakubalika na huko CDM kashaharibu...

CV ya mwanasiasa ( mtaji) daima huwa ni msimamo wake usioyumba - huyu mwanadada pamoja na wenzake washapoteza kete hii adimu.

Namuona sasa akitangatanga..safari yake ya kubakia CCM ama kwenda ACT inanukia kama siyo NCCR. ..

Kacheza karata zake vibaya mno - pole yake!!

BAWACHA wacmsheni indicators ombeni njia kitu kiingie njia kuu...hakuna kulala...!!
 
Baraza la wanawake wa Chadema ( BAWACHA ) , limetangaza rasmi kuanza mchakato wa kujaza nafasi za Wasaliti waliotimuliwa ndani ya Chama wakiongozwa na Halima Mdee .

Fomu za Kugombea nafasi hizo za uongozi wa Bawacha Taifa zinapatikana kwenye ofisi za Mikoa za Chadema , ofisi za Kanda zote na ofisi ya Bawacha Makao Makuu , DSM , ambapo wanawake wote wa Chadema wenye uwezo wanaombwa kuchangamkia nafasi hizo Muhimu na zenye heshima kubwa .

Form zinaanza kutolewa tarehe 25 february 2021 ambapo zoezi la kuchukua na kurejesha form hizo litadumu hadi tarehe 3 March 2021 saa 10 jioni .

View attachment 1711946

Mungu ibariki Chadema
Safii sana
 
Kisheria wakirudisiwa unachama, basi wanakuwa wamerudishiwa na haki zao zote walizokuwa nazo kabla ya kuvuliwa uanachama, ikiwa ni pamoja na nafasi za uongozi walizokuwa nazo wakati huo. Subira huko BAWACHA ilihitajika.
Sio lazima. Baraza linaweza kuamua kuwasamehe bila kuwarudishia nyadhfa zao. Itakuwa unavyosema kama Baraza litaona kuwa hawakutendewa haki na Kamati Kuu na kutamka kuwa kufukuzwa kwao na adhabu nyingine walizopewa zilikuwa batili. Sidhani kama hili litatokea. Likitokea Kamati Kuu itabidi ijiuzuru. Kinachohitajika ni unyenyekevu kutoka waliokuwa wanachama wa CHADEMA na kukubali hukumu yeyote itakayotolewa dhidi yao. Ukimya wao hadi sasa unaelekea huko.

Amandla...
 
..katiba ya chadema hairuhusu mwanachama kukishitaki chama chao.

..zitto alifukuzwa kwasababu alifungua kesi dhidi ya chadema.

..hawa kina mama nia yao ni ubunge, siyo nafasi za uongozi ktk chama.

..wanachotakiwa ni kuwa wapole ili waendelee kuwa wanachama wa chadema.
Habari ya uanachama wa Chadema kwa hawa wakina mama imekwisha na imefungwa , makosa waliyoyatenda ndani ya Chadema adhabu yake iko ndani ya katiba , hakuna namna yoyote ile ya hawa kurudi Chadema kupitia rufaa.

Never Ever !
 
Baraza la wanawake wa Chadema (BAWACHA) , limetangaza rasmi kuanza mchakato wa kujaza nafasi za Wasaliti waliotimuliwa ndani ya Chama wakiongozwa na Halima Mdee.

Fomu za Kugombea nafasi hizo za uongozi wa Bawacha Taifa zinapatikana kwenye ofisi za Mikoa za Chadema, ofisi za Kanda zote na ofisi ya Bawacha Makao Makuu, DSM, ambapo wanawake wote wa Chadema wenye uwezo wanaombwa kuchangamkia nafasi hizo Muhimu na zenye heshima kubwa.

Form zinaanza kutolewa tarehe 25 february 2021 ambapo zoezi la kuchukua na kurejesha form hizo litadumu hadi tarehe 3 March 2021 saa 10 jioni.

Mungu ibariki Chadema
Fyekelea mbali hao COVID-19!
 
Back
Top Bottom