CHADEMA yatangaza uchaguzi wa kujaza nafasi za waliotimuliwa Bawacha

Asante kwa taarifa Ngoja niwahimize wana CCM walioko Chadema wachukue fomu upesi kugombea uongozi BAWACHA kuanzia uenyekiti hadi chini
 
Baraza la wanawake wa Chadema ( BAWACHA ) , limetangaza rasmi kuanza mchakato wa kujaza nafasi za Wasaliti waliotimuliwa ndani ya Chama wakiongozwa na Halima Mdee .

Fomu za Kugombea nafasi hizo za uongozi wa Bawacha Taifa zinapatikana kwenye ofisi za Mikoa za Chadema , ofisi za Kanda zote na ofisi ya Bawacha Makao Makuu , DSM , ambapo wanawake wote wa Chadema wenye uwezo wanaombwa kuchangamkia nafasi hizo Muhimu na zenye heshima kubwa .

Form zinaanza kutolewa tarehe 25 february 2021 ambapo zoezi la kuchukua na kurejesha form hizo litadumu hadi tarehe 3 March 2021 saa 10 jioni .

View attachment 1711946

Mungu ibariki Chadema
Cdm hatujawahi kukosea kwa bahati mbaya au makusudi.
Kamwe hatuwezi kukubali kuishi na covid ndani ya chama wakati tunajua ni nyoka wenye sumu kali.
 
kitu pekee ambacho kinaweza kutokea wakishinda rufaa ( japo hilo halipo ) ni kurejeshewa uanachama , si kurejeshewa uongozi
Na hawawezi kushinda kamwe maana hata watumie mamluki hawawezi tuuu wana cdm hatupo tayari kuwapokea wasaliti
 
..hawatorudishiwa nyadhifa kwasababu nafasi zao zilijazwa wakati chama kikiwa hakiwatambui kuwa ni wanachama.
Sio kweli maamuzi ya mkutano mkuu hayajafanyika bado wanachama halali na watambwaga Mbowe na kamati kuu yake mapema tu


Sema Mbowe anafanya kusudi kuvuruga mchakato sababu keshavuta pesa ya kila mwezi kutoka kwa hao wabunge anataka tu kuzusha mgogoro wa kisheria sababu wale wamekata rufaa kikatiba.Kikao cha kikatiba waluchokata rufaa hakijaketi kuamua yeye ansitisha uchaguzi mmmmm ni fix tupu hapo
 
Back
Top Bottom