CHADEMA wafahamu kuwa suala la kutaka Tanzania iwekewe vikwazo ni usaliti mkubwa kwa wapiga kura wake

Bowie

JF-Expert Member
Sep 17, 2016
4,372
6,078
Nimeona viongozi mbalimbali wa CHADEMA wakitaka Tanzania iwekewe vikwazo baada ya kushindwa katika uchaguzi mkuu uliopita.

Mimi ninauhakika Tanzania haijafikia hatua ya kuwekewa vikwazo vya kiuchumi kwani hao wafadhili wanajua moja kwa moja mwananchi wa kawaida ndio atakayeumia na vikwazo hivyo.

Ni aibu kwa mtanzania kukimbilia Belgium na kuomba waliompigia kura kuwekewa vikwazo vya kiuchumi wakati yeye na familia wakila Bata huko. Tanzania kwanza tuache masuala ya vyama.
 
Naomba uelewe kwamba ikiwa wewe utaibiwa Mali yako na kwenda kulalamika kwenye vyombo vya Dola,happy nani atakayekuwa anaonewa? Mnyang'anywa haki au mnyang'anywa haki
 
Hakuna vikwazo vibaya na vinavyoumiza wananchi kama wananchi kuwa na serekali ambayo hawajaichagua wao!Unaelewa ni kwa kiasi gani wananchi wameumia baada ya zile TZS billion 70 za EU za kupambana na Corona kupigwa na serekali ya Magufuli ambayo siyo chaguo la wananchi?Unaelewa kuwa serekali ambayo siyo chaguo la wananchi ni vibaka?

Unaelewa kuwa kama serekali iliyopo madarakani ingekuwa ni chaguo la wananchi haya majanga ya vibaka ambao hawajachaguliwa na wananchi kupiga TZS billion 70 yasingetokea?Unaelewa hio serekali ya vibaka ambayo haijachaguliwa na wananchi kwa miaka mitano ijayo itasababishia wananchi majanga kama haya mangapi?
 
Hata kivuruge wetu wa uchaguzi anajuwa kuwa vikwazo vikiwekwa atakaye umia ni raia wa kawaida, hivyo kaamuwa kuwatumia kama ngao.
 
CCM na vibaraka wake ndio wanafaidika na hiyo misaada na si wapiga kura wa CHADEMA walioko magerezani kwa kesi za kubumba
 
Nimeona viongozi mbalimbali wa CHADEMA wakitaka Tanzania iwekewe vikwazo baada ya kushindwa katika uchaguzi mkuu uliopita.

Mimi ninauhakika Tanzania haijafikia hatua ya kuwekewa vikwazo vya kiuchumi kwani hao wafadhili wanajua moja kwa moja mwananchi wa kawaida ndio atakayeumia na vikwazo hivyo.

Ni aibu kwa mtanzania kukimbilia Belgium na kuomba waliompigia kura kuwekewa vikwazo vya kiuchumi wakati yeye na familia wakila Bata huko. Tanzania kwanza tuache masuala ya vyama.
Uchumi wa kati mnaogopaje vikwazo? Mbona Putin haogopi vikwazo kama wanalumumba?
 
Kuna mikataba tumeingina kama Taifa ya kuheshimu haki za binadamu na utawala bora. Ndiyo maana Mwalimu alikubali kubadilisha katiba na sheria ili kuruhusu mambo haya kufanyika, alitaka twende sambamba na matakwa na kiulimwengu maana alielewa fika kwamba hutuwezi kujitenga na mataifa kwa namna yoyote ile.

Sasa kuna kikundi cha watu kinaona alichofanya mwalimu ilikuwa ni Ujinga na usaliti, sasa kimeamua kufanya kinyume chake, yaani kuturudisha nyuma kabisa wakati tulikuwa tuna sauti moja tu - ya Kiongozi wa chama akishatamka basi kauli yake ni sheria tayari..(zidumu fikra za Mwenyekiti.....)

Majority ya ulimwengu wote wanafuata mfumo wa kidemokrasia wa vyama vingi, ni mfumo mzuri maana kila raia wa nchi husika anapata nafasi na sehemu ya kusema dukuduku lake liwe ama kukosoa au kuishauri Serikali iliyoko madarakani.

Sasa mataifa yameamua kututenga endapo hatutaheshimu MIKATABA YA KIMATAIFA tuliyo sign kwa hiari yetu sisi wenyewe, kututenga ni pamoja na kutunyima misaada na zaidi tunaweza kushitakiwa katika mahakama hizo za kimataifa.

Sasa sidhani CDM wanahusika kwenye hili, wanaohusika hapa ni CCM ambao wamegoma kabisa kuheshimu haki za binadamu na utawala bora, wamegoma kabisa kuruhusu shughuli za kisiasa za vyama vya upinzani nchini ingawa Katiba na Sheria inaruhusu, na kwa makusudi kabisa wamefanya udanganyifu mkubwa katika uchaguzi huu uliopita.

Sasa adhabu itatuangukia sisi sote ingawa ni kosa la mmoja yaani CCM. Maana tunavyojua Tanzania hii bado haina uwezo wa kujitegemea kwa asilimia mia. tunakwenda kupata shida ambayo ni afadhali ya ile shida tulipata baada ya vita ya Kagera kwa wale wakongwe wenzangu mtakumbuka namna tulivyofunga mikanda.
 
Hakuna mahali Chadema imeomba tanzania iwekewe vikwazo, ila dhulma za serikali iliyoko madarakani inatuweka katika kukosa sifa ya kuendelea kupokea misaada kutoka mataifa ya kigeni, kwa sababu hio vitendo vya serikali ndio chanzo cha migomo ya chini kwa chini ya hawo mnaowauta mabeberu. Fedha za maendeleo ya demokrasia na haki za msingi za raia ni masuala yenye utata hasa linapokuja suala la kupokea kupata mikopo kutoka kwa wafadhili.
 
NA ULE ULIOFANYWA NA CCM NI NINI ?

TISS,,, POLISI NA JESHI NDIO YALIYOTUUMIZA WANANCHI.


CHAMA DOLA KINATUMIA VIBAYA DOLA.
 
Back
Top Bottom