CHADEMA wafahamu kuwa suala la kutaka Tanzania iwekewe vikwazo ni usaliti mkubwa kwa wapiga kura wake

Nimeona viongozi mbalimbali wa CHADEMA wakitaka Tanzania iwekewe vikwazo baada ya kushindwa katika uchaguzi mkuu uliopita.

Mimi ninauhakika Tanzania haijafikia hatua ya kuwekewa vikwazo vya kiuchumi kwani hao wafadhili wanajua moja kwa moja mwananchi wa kawaida ndio atakayeumia na vikwazo hivyo.

Ni aibu kwa mtanzania kukimbilia Belgium na kuomba waliompigia kura kuwekewa vikwazo vya kiuchumi wakati yeye na familia wakila Bata huko. Tanzania kwanza tuache masuala ya vyama.
Kwani CHADEMA imepigiwa jura na nani?
 
Wewe mleta mada ni ujinga tu ndio unakusumbua, unafahamu Ayatollah Khamenei alikimbilia wapi wakati anashinikiza wananchi wa Iran waandamane dhidi ya serikali ya Shah.

Obote alikuwa wapi akishinikiza uasi dhidi ya Amin au unafahamu wakati wa utawala wa makaburu kule SA ni kwa nini karibu dunia nzima ilishinikiza hiyo nchi iwekewe vikwazo kwani hawakujua kuwa ni waafrika walio wengi ndio wangeathirika au labda ulikuwa hujazaliwa.

Wakati nyumba 🏠 inapoungua ni haki kwa waokoaji kubomoa milango na madirisha ili kuokoa watu bila kujali gharama au thamani ya nyumba. So please grow up.
 
Nimeona viongozi mbalimbali wa CHADEMA wakitaka Tanzania iwekewe vikwazo baada ya kushindwa katika uchaguzi mkuu uliopita.

Mimi ninauhakika Tanzania haijafikia hatua ya kuwekewa vikwazo vya kiuchumi kwani hao wafadhili wanajua moja kwa moja mwananchi wa kawaida ndio atakayeumia na vikwazo hivyo.

Ni aibu kwa mtanzania kukimbilia Belgium na kuomba waliompigia kura kuwekewa vikwazo vya kiuchumi wakati yeye na familia wakila Bata huko. Tanzania kwanza tuache masuala ya vyama.
Si viongozi tu wanaotaka.Hata sisi raia wa kawaida tuliofanywa wajinga kwa kupiga kura na kupigwa changa la macho.

Na acha upotoshaji.Wanaotakiwa kuwekewa vikwazo ni magufuli na genge lake si nchi! magufuli ataondoka lakini nchi itabaki.Huyo si nchi!
 
Post zote 34 za waliotangulia kuchangia wamepingana na mleta mada!Wewe wa 35 ndiye umeungana na mleta mada!
Hii inamaana watanzania hawapendezwi na ukandamizwaji wa haki unaofanya na serikali ya CCM kwa kutumia dola!Wakulaumiwa hapa ni serikali ya CCM!
Mmetugawa sana wananchi,mnapandikiza chuki katika jamii!
Wewe ulitakaje kwa mfano?
 
6 Reactions
Reply
Back
Top Bottom