KalamuTena
JF-Expert Member
- Jul 7, 2018
- 13,189
- 17,157
Ushauri wako umeuharibu kwa kushindwa kuficha ushabiki wako.Salaam wakuu,
Maneno yangu ni machache sana kwa chama kikuu cha upinzani CHADEMA kuwa waachane haraka na mpango wao wa maandamano ya amani/ sherehe ya mapokezi ya mh Tundu A. Lissu siku ya jumatatu ya 27 jul 2020.
Ndugu zangu huu ni mtego ambao umejitokeza kwa bahati mbaya kwenye njia ya CHADEMA wanapaswa kuukwepa haraka iwezekanavyo, nchi ipo kwenye msiba wa kitaifa wa Rais mstaafu, tupo kwenye siku saba za maombolezo, nchi jirani mfano kwenye bendera zinapepea nusu mlingoti, viongozi wa mataifa mbalimbali watakuja hapa kuomboleza pamoja nasi n.k
Sasa kwa hali hii si sahihi kwa CHADEMA kufanya hayo mapokezi; mtakuwa mmefanya Jambo la kijinga na wengi watawadharau kabisa na mtapoteza Imani kwa watu wengi.
Kwenye sakata la kuondoka bungeni kujiweka karantini wakati wa kitisho cha COVID-19 tuliwashauri muachane na mpango ule hamkusikia na hatimae mkajitia aibu kubwa na kudharaulika kwa kiasi kikubwa sana, safari hii pia tunawashauri tena achaneni na huu mpango sio salama kwa ustawi wenu kisiasa kuelekea uchaguzi mkuu mtapoteza wapiga kura wengi sana kwa sababu hili tukio.
Licha ya hayo mtasababisha mgawanyiko ndani ya Chama kwa wale ambao hawata kubaliana nanyi kuto kuhudhuria msibani badala yake kwenda kwenye mapokezi, ikiwa ubabe utatumika kwenye hili basi hakika Kuna watu watenda kuunga juhudi.
Shitukeni CHADEMA, achaneni na huu mpango mtawapa watu mtaji wa kisiasa bure. Tafakarini upya mkiwa kama CHAMA makini.
Natanguliza hongera zangu kwenu kama mtakuwa wasikivu.
Ngoja nikuulize swali:
Kwani umesikia CHADEMA wana mipango gani? Umekwishasikia uongozi wa CHADEMA ukisema lolote kuhusu jambo hili?