Tindo
JF-Expert Member
- Sep 28, 2011
- 58,649
- 102,683
Tatizo lako ni kwamba chochote kitakachopangwa na Chadema kwako wewe kitakuwa kizuri tu. kama huoni kuwa kukusanyika uwanjani kwa mapokezi na nina hakika lazima zitakuwa ni kama sherehe tu naweza sema hivo na sina shaka hapatakosa mabango yenye jumbe tofauti tofauti huku wakati huo huo nchi ipo kwenye maomboleza bendera ziko nusu mlingoti basi utakuwa na matatizo fulani mkuu.
Unaposema kada wa ccm aliyewahi kuwa rais wa Tanzania unamaanisha nini? Inamaana siku wapinzani wakichukua nchi tutakuja pia tuseme kuwa mfano Mbowe ni kada wa Chadema ambaye ni rais wa Tanzania? Huoni kauli kama hizo zinamalengo ovu mkuu.
Ni kipi kimepangwa na cdm kikawa kizuri kwako au nyie? Wakati walipotaka kukusanyika ili kumuombea kulikuwa na msiba pia? Huu msiba mnataka kuutumia kama kificho, ila hata kama kusingekuwa na msiba, bado cdm wasingeruhusiwa kumpokea kwa shangwe. Nionyeshe post yako ambayo cdm wamefanyiwa ndivyo sivyo, kisha ww ukaanzisha uzi kuwa hawahafanyiwi sawa, ili nijue kuwa huwa unasimamia haki?
Narudia tena, Mkapa alikuwa ni kada wa ccm aliyewahi kuwa rais wa Tanzania. Ni wapi nimekosea hapo? Na alipostaafu kwenye urais, bado alikuwa akizunguka kwenye majukwaa vya ccm, kueneza siasa za chuki dhidi ya wapinzani. Hili wala hakulifanya kwa kificho. Nadhani una kifua kidogo cha kusikia ukweli usioupenda, ndio maana unapata tabu unapokutana na ukweli unaokera. Siku huyo Mbowe au yoyote akiwa rais, unaweza kusema ni kamanda wa Cdm aliyekuwa rais wa Tanzania, na utakuwa sahihi kabisa.
Usitake kunilazimisha kumuita mtu alikuwa rais wetu tu, huku nikiacha sifa yake nyingine ambayo hakuona aibu kujihusisha nayo, tena mara nyingi sifa hiyo ya ukada, aliitumia kwa namna hasi dhidi vya upinzani.