Ngongo
JF-Expert Member
- Sep 20, 2008
- 18,930
- 31,172
Heshima sana wanajamvi,
Nimefuatilia mienendo ya msiba wa Mzee Lowassa kwa kiasi fulani na kubaini yafuatayo.
Mosi, watawala baada ya kugundua wameshindwa kuwapatia wananchi umeme wa uhakika, wameamua kuhamisha magoli makusudi kutuaminisha kwamba walimpenda, wanampenda na wataendelea kumpenda Hayati Lowassa.
Wanajua mara nyingi Watanzania hawana kumbukumbu nzuri, ni watu wepesi sana kusahau matendo yaliyotendeka miaka michahce iliyopita. Wanafikiri kwa kutumia msiba huu hakika WAMAASAI watasahau madhila wanayokumbana nayo huko Ngorongoro.
Wanajua Lowassa hakuwa Mmasai kwa asili lakini wanajua Lowassa kakulia, huko Masaini na amekuwa Mbunge wa Monduli kwa kipindi kirefu sana. Wanajua jamii ya Kimasai wanaheshima kubwa kwa Lowassa.
Mwaka 1995 Lowassa alikataliwa na Kamati kuu ya CCM kwa hoja ambazo mpaka umauti unamkuta hakuweza kuzipangua. Kama hilo halikutosha Mwaka 2015 Lowassa akajitosa katika mchakato wa kuwania nafasi ya Urais ndani ya CCM bado hakuweza kupenya kwa hoja zile zile za Mwaka 1995 tena zikaongezeka hoja nyingine nzito wakati akihudumu nafasi ya Waziri Mkuu.
Kwa ufupi sana tunafahamu Lowassa alijiunga CHADEMA baada ya kuenguliwa CCM. Zipo hoja nyingi kwamba katika uchaguzi ule Lowassa alishinda kwa kishindo kama ulivyo utaratibu wetu wa tume yetu ya uchaguzi wakafanya yao.Sishangai sana CHADEMA kudai tume huru ya uchaguzi, baada ya kubaini madudu yanayoendelea katika chaguzi zetu.
Mzee Lowassa atazikwa 17/02/2024, ninachokiona mpaka sasa Watawala wameamua kumtumia baada ya maigizo ya Makonda kuanza kuzua maswali mengi pasipo majibu.
Ni wazi tena pasipo shaka Watawala kuanzia awamu ya kwanza hawakumwamini Lowassa, walimtenga mbali na kiti cha Magogoni kwa HOJA nzito nzito. Lowassa hayupo tena lakini ana faida kubwa kipindi hiki kuelekea uchaguzi watamsifu, watamtukuza, watambandika majina mazuri mazuri kwakuwa hana madhara tena.
Watawala wanauza BANDARI, wanauza Ngorongoro, hawawezi kutuletea umeme wa uhakika, hakuna sukari, hali ya maisha inaendelea kupanda kila uchao, hawana majibu kwanini tusimtumie Lowassa!
Ngongo safarini Monduli.