CHADEMA kuweni makini na mapokezi ya Lissu wakati huu wa msiba, mnafanya kosa la kiufundi, mtawapa watu mtaji wa kiasa kuelekea Uchaguzi Mkuu

Uyo Mkapa hakuwahi kukemea maovu yaliyofanyika kama lile la Lissu kupigwa risasi lakini pia alitukana watanzania waziwaazi kuwa ni wapumbavu na marofa sasa mtu kama uyo ya nini kumuomboleza katika msiba wake
Mkuu ukitulia utaona msingi wa hoja yangu ni nini.
 
Sioni kuna tatizo gani kwa cdm kwenda kumpokea Lisu. Kwanza iko wazi kuwa marehemu alikuwa ni kada wa ccm aliyekuwa na chuki ya wazi na upinzani hasa cdm. Ni kweli alikuwa rais wetu, lakini hakuwahi kuishi kama rais mstaafu, bali aliishi zaidi kama rais mstaafu wa ccm. Alijichukulia kuwa mwanaccm zaidi, kuliko kiongozi wa wote. Na yeye alikuwa ni sehemu ya chuki za kiitikadi ndani ya nchi hii. Hilo wala sioni shida yoyote kulieleza.

Watakachofanya cdm ni kumpokea mpendwa wao kwa amani aliye hai, baada ya kunusurika kufa, huku wanaccm wakiwa kwenye majonzi ya kuondokewa na kada wao aliyewahi kuwa rais wa nchi hii. Msitake kulazimisha hata watu walioumizwa na siasa za marehemu, kuwa sehemu ya majonzi yenu.
Mkapa alikuwa ni mwanaccm aliyekuwa rais wa nchi hii, na aliyekuwa na chuki ya wazi kwa wapinzani. Hakuna namna mtu aliyekuwa na chuki ya wazi kwa wapinzani, azuie mpinzani aliye hai kupokelewa kwa amani eti kisa kafariki. Alipokuwa hai hakuona umuhimu wa kuwa kiongozi wa wote, kwanini amefariki mlazimishe tuone kuwa ni msiba wa wote?
Huko nchi jirani hawajui alichokuwa anafanya huku ndani, hivyo ni haki yao kupeperusha bendera nusu mlingoti. Anayevaa kiatu ndio anajua kinapobania. Lisu atapokelewa kwa amani kabisa, na wala hakuna tatizo lolote. Watu wakiwa wengi ni vizuri, wakiwa wachache ni sawa pia. Cha muhimu wampokee kwa ustaarabu tu, wakijua kuna msiba wa kada wa ccm aliyewahi kuwa rais wa nchi hii. Lakini hakuwa na faida yoyote kwa cdm zaidi ya kuhakikisha wananyanyaswa ndani ya nchi hii.
Naona tatizo la kusifu kila kitu bila kutafakari mara mbili halipo kwa ccm peke yao kumbe hata huku upinzani nako Kuna tatizo lile lile kila kinacho semwa lazima kisifiwe na kiungwe mkono bila ya kuangalia kitaleta matokeo gani.
 
Nchi ipo kwenye maombelezo,itakuwa si vyema kuwa na aina au dalili yoyote ya shamra shamra wakati wa ujio wa Lissu.Chadema wawe makini.
Wewe hapo ulipo unalia? Au huendi bar? Au humpi Mumeo tendo la usiku kisa kuna msiba? Lazima mambo mengine yaendelee. Just kama ilivyokuwa kwa Corona. Hatuwezi kujifungia ndani tukaacha kwenda kumlaki mwamba eti kisa kuna msiba
 
Waache wawape watu chakusema, yani we bendera zinapepea nusu mlingoti hadi nchi jirani, watu wanaacha shughuli zao za kitaifa kwenye nchi zao huko wanakuja hapa nchini alafu eti wewe mtanzania unaenda kufanya maandamano ya mapokezi.
Wewe ni lofa kweli,mbona huzungumzii kura za maoni za ccm zinazoendelea
 
Salaam wakuu,

Maneno yangu ni machache sana kwa chama kikuu cha upinzani CHADEMA kuwa waachane haraka na mpango wao wa maandamano ya amani/ sherehe ya mapokezi ya mh Tundu A. Lissu siku ya jumatatu ya 27 jul 2020.

Ndugu zangu huu ni mtego ambao umejitokeza kwa bahati mbaya kwenye njia ya CHADEMA wanapaswa kuukwepa haraka iwezekanavyo, nchi ipo kwenye msiba wa kitaifa wa Rais mstaafu, tupo kwenye siku saba za maombolezo, nchi jirani mfano kwenye bendera zinapepea nusu mlingoti, viongozi wa mataifa mbalimbali watakuja hapa kuomboleza pamoja nasi n.k

Sasa kwa hali hii si sahihi kwa CHADEMA kufanya hayo mapokezi; mtakuwa mmefanya Jambo la kijinga na wengi watawadharau kabisa na mtapoteza Imani kwa watu wengi.

Kwenye sakata la kuondoka bungeni kujiweka karantini wakati wa kitisho cha COVID-19 tuliwashauri muachane na mpango ule hamkusikia na hatimae mkajitia aibu kubwa na kudharaulika kwa kiasi kikubwa sana, safari hii pia tunawashauri tena achaneni na huu mpango sio salama kwa ustawi wenu kisiasa kuelekea uchaguzi mkuu mtapoteza wapiga kura wengi sana kwa sababu hili tukio.

Licha ya hayo mtasababisha mgawanyiko ndani ya Chama kwa wale ambao hawata kubaliana nanyi kuto kuhudhuria msibani badala yake kwenda kwenye mapokezi, ikiwa ubabe utatumika kwenye hili basi hakika Kuna watu watenda kuunga juhudi.

Shitukeni CHADEMA, achaneni na huu mpango mtawapa watu mtaji wa kisiasa bure. Tafakarini upya mkiwa kama CHAMA makini.

Natanguliza hongera zangu kwenu kama mtakuwa wasikivu.
Yaani ww ni pimbi hatari ..yaani kumpokea Lissu kunahusiana vp na kifo Cha mkapa??? Tutakuja kuaga na isitoshe Lissu lazima atakuja kuaga pia ...usitutishe usitutishe usitutishe
 
Wewe ni lofa kweli,mbona huzungumzii kura za maoni za ccm zinazoendelea
Dah we jamaa aisee! Kwahiyo huoni tofauti ya hivo vikao na sherehe za mapokezi/ sijui maandamano ya amani?
 
Yaani ww ni pimbi hatari ..yaani kumpokea Lissu kunahusiana vp na kifo Cha mkapa??? Tutakuja kuaga na isitoshe Lissu lazima atakuja kuaga pia ...usitutishe usitutishe usitutishe
Kukurupuka ni kubaya sana mkuu sidhani hata kama umesoma uzi wote na kuelewa nilicho andika wewe.
 
Kukurupuka ni kubaya sana mkuu sidhani hata kama umesoma uzi wote na kuelewa nilicho andika wewe.
Nimekuelewa sana , kwanza msibani tutakuja licha mkapa alituchukia sana sana sisi wapinzani...lkn tutakuja hvyo hvyo tu na Lissu pia atakuja kuaga japo alimfunga kipindi anapambania madini ya nchi hii ....
 
Nimetua hapo JNIA mchana huu nikitokea Zanzibar hali ni shwari kabisa kila kona kuna jicho kali.

Hatari sana.
 
Dah we jamaa aisee! Kwahiyo huoni tofauti ya hivo vikao na sherehe za mapokezi/ sijui maandamano ya amani?
tofauti iko wapi,lissu ni mapokezi nani amesema sherehe,wewe unang'ang'ania chadema wakati ccm wanaendelea na kura,hebu balance shobo zako hata kama hupendi chadema ongea basi facts siyo unaegemea upande
 
Naona tatizo la kusifu kila kitu bila kutafakari mara mbili halipo kwa ccm peke yao kumbe hata huku upinzani nako Kuna tatizo lile lile kila kinacho semwa lazima kisifiwe na kiungwe mkono bila ya kuangalia kitaleta matokeo gani.

Mfano wako hauingii kwenye post yangu yoyote hapo juu, au umesoma post nyingine, ndio ukaja kuniquote mimi? Ni wapi nimesifia chochote hapo juu? Au ni madhara gani yatatokea kwa Lisu kupokelewa kwa amani, na kwa ustaarabu kuwa kuna msiba wa kada wa ccm aliyewahi kuwa rais wa Tanzania?
 
Wewe hapo ulipo unalia? Au huendi bar? Au humpi Mumeo tendo la usiku kisa kuna msiba? Lazima mambo mengine yaendelee. Just kama ilivyokuwa kwa Corona. Hatuwezi kujifungia ndani tukaacha kwenda kumlaki mwamba eti kisa kuna msiba

Upeo mdogo wa kufikiri,pole sana.Unaongea sana kwenye keyboard lakini viongozi wenu wakipata matatizo hakuna mwanachama wa kawada hata mmoja anaejitokeza wazi wazi kuwapambania,mnabaki kulia lia mitandaoni tu.Mimi ninayeona mbali,na ninaye thamini sana mchango wa Chadema katika Taifa hili naumia sana kuona hawa viongozi wanaumizwa kiasi hicho.
Pia Chama kipo katika harakati za uchaguzi,hakuna tena muda wa kupoteza kwenye hayo makesi ya kipuuzi watayowafunguliwa.Bila shaka barua ya Polsisiem umeiona.Labda utanielewa.
 
tofauti iko wapi,lissu ni mapokezi nani amesema sherehe,wewe unang'ang'ania chadema wakati ccm wanaendelea na kura,hebu balance shobo zako hata kama hupendi chadema ongea basi facts siyo unaegemea upande
Punguza hasira mkuu ya haja gani ku panic sasa.
Mimi nimekuuliza huoni utofauti ya vikao vya ndani na hayo mapokezi ya Lissu? ( Ni sherehe ndio au tunaweza kusema ni maandamano ya amani)
 
Mfano wako hauingii kwenye post yangu yoyote hapo juu, au umesoma post nyingine, ndio ukaja kuniquote mimi? Ni wapi nimesifia chochote hapo juu? Au ni madhara gani yatatokea kwa Lisu kupokelewa kwa amani, na kwa ustaarabu kuwa kuna msiba wa kada wa ccm aliyewahi kuwa rais wa Tanzania?
Tatizo lako ni kwamba chochote kitakachopangwa na Chadema kwako wewe kitakuwa kizuri tu. kama huoni kuwa kukusanyika uwanjani kwa mapokezi na nina hakika lazima zitakuwa ni kama sherehe tu naweza sema hivo na sina shaka hapatakosa mabango yenye jumbe tofauti tofauti huku wakati huo huo nchi ipo kwenye maomboleza bendera ziko nusu mlingoti basi utakuwa na matatizo fulani mkuu.
Unaposema kada wa ccm aliyewahi kuwa rais wa Tanzania unamaanisha nini? Inamaana siku wapinzani wakichukua nchi tutakuja pia tuseme kuwa mfano Mbowe ni kada wa Chadema ambaye ni rais wa Tanzania? Huoni kauli kama hizo zinamalengo ovu mkuu.
 
Back
Top Bottom