CHADEMA kuchukua nchi ni baadae sana

CHADEMA kuchukua nchi ni baadae sana

Pasco,
Naungana na wewe kwa ushauri wako mzuri sana. Kazi iliyobaki kwa CDM ni kuenda vijijini kuwaamsha waliolala wanaodhani usipoichagua CCM hakuna maisha, nimejaribu kuangalia nyendo za Dr Slaa nimegundua kazi hii anaiweza sana kwa kuwa ana ushawishi mkubwa sana kwa Watanzania wa rika zote.
Kwa hali inavyoendelea na makosa ya waziwazi ya serikali ya CCM ambayo wakuu wa chama hiki hawataki kuyarekebisha na kuyadhibiti, uwezekano wa CDM kuchukua nchi 2015 ni mkubwa sana. Nawashauri CDM kwa sasa wakaze buti na kuanzia waanzie mikoa ya kati hasa Dodoma, Singida na Tabora ambayo ninadhani elimu ya uraia kwao imewapitia pembeni.
Then waelekee mikoa ya kusini na iliyoko katika mwambao wa bahari ya Hindi, sehemu hizo nilizozitaja wapekeke majembe hasa kwa kuwa asili ya watu wake ni wagumu kuelewa na hasa elimu ya uraia.
Kama mtakuwa mlikuwa makini kuangalia taarifa ya habari jana, Mama Kilango alijitahid mno kuwalaghai wananchi wa kata ya Kiwira-Tukuyu kwa kuwachonganisha na CDM ili wainyime kura, kilichotokea ni wananchi hao kumgezia kibao pamoja na kukiadhibu chama chake kwa kumpigia kura mgombea wa CDM.
Dalili hizo zinzonyesha ni kwa kiasi gani Watanzania wamechoka na ndoto za 'alinacha'. Kete hii ikitumiwa vizuri na CDM, basi tukiri wazi kuwa CCM kitakufa kifo cha mende! Refer; President Wade wa Senegal wiki iliyopita. Wanachi amkeni nchi imeuzwa tuko gulioni!
 
Mungu alishaonyesha nuru yake kwamwe ccm hawatashinda urais mwaka 2015
 
Chadema wafanye kazi kweli kweli. Wasibweteke na haya matokeo. 2015 sio mbali. Na sio guarantee kuwa watashinda. They need to prepare the way from now.

Kingine, hii miaka iliyobaki, wajitahidi kufungua kituo cha TV. Itawasaidi sana kuelimisha jamii kwa pamoja na hata 2015 kwenye kampeni.

Kuna watu wengi wanataka kujua kuhusu CHADEMA. Lakini hawawezi kuingia humu Jamii Forums. Wala hawawezi kuhudhuria mikutano yenu. TV ndo itakayowapa umaarufu zaidi.
 
MKAKATI WA KUIONDOA SSM HAUJAANZA LEO UNAENDELEA NA UTAFANIKIWA....pesa siyo zaidi ya mungu ..
 
kuporomoka kwa CCM
Picha ya matokeo ya uahaguzi armeru na sehemu zingine
inaonesha kuwa mporomoko wa CCm upo kwa kasi kubwa japokuwa wengine tunaweza kujifariji na maneno ya kujifurahisha au kujifariji. ukiangalia Armeru Nguvu kubwa ya chama tawala ilikuwa huko na uwezo mkubwa wa watendaji wake kusimama majukwaani kutoa sera mbalimbali lakini watu wame pembua mbovu na bivu wakatofautisha,
kwa hali hiyo basi ukiangalia kwa makini vyama vingine vimejipanga kushindana na chama Tawala lakini chadema ndo chama pekee kilicho jijenga vizuri zaidi kwanza
  1. Elimu
  2. utaalamu wa upambanaji kisiasa
  3. Uwezo wa mtu mmojammoja katika chama
  4. utendaji kazi kichama
  5. Mbinu na miongozo yao
nikiongelea mada moja baada ya nyingine nikianza na Elimu .
Chama cha chadema kiliwekeza zaidi kielimu kwa kutumia vijana kwenye vyuo ambamo ndio tegemeo la taifa kupata nguvu kazi ya taifa ktk kukuza uchumi na maendereo ya nchi kwa kwa ujumla wake na ujue vyuo vinazalisha watu wengi kumbuka hawa watu ni wasomi wa kila sector serikalini wakiwa wamefunzwa mbinu,mifumo,misingi na ukombozi wao hasa wakiwa wana chama wa chadema toka vyuoni sasa mripuko wa watu hawa kwa muda wa miaka kazaa utashangaa maamuzi mazito ya watu yakitoka bila kujali ninani yupo yukowapi na anafanya nini. leo niishihapo kesho nitaendelea.
 
Mkuu uko sahihi sana. Miongozo hiyo ndiyo iliyokifanya chama kujjijenga na kinaendelea kukua kwa kasi. Cha msingi hapa ni makamanda waanze kukijenga chama hasa central part of the country pia vijana wengi wajiandishe katika daftari la kudumu la wapiga ili mwaka 2015 tembo auliwe kwa bua.
 
Bwana Pasco! heshima kwako mkuu kwa kunena kwa umakini!

JF imevamiwa na walowezi watu ambao hawawezi kujadili hoja ni wengi sana tumekuwa na mamluki wa kujadili watu na kila kinacholetwa kinaangaliwa kimewasilishwa na nani badala ya kimebeba ujumbe gani kwa hadhira iliyokusudiwa. Hii inadhihirisha jinsi ambavyo bado tunasafari ndefu katika kuupata ukombozi wa kweli. Mimi binafsi ninaamini ukombozi wa kweli wa mtanzania utaanzia katika mind yake binafsi ndipo uweze kuhakisiwa na jamii inayomzunguka huyu mtanzania. Bila ya ukombozi wa kifikra basi hata akishuka malaika toka mbinguzi kutuongoza hatutoweza kuvuka toka upande huu wa mto na kufika ng'ambo ya pili.

Ushindi wa Arumeru Mashariki kwa CDM ni pigo kubwa kwa wana CCM na pro-Lowasa wote. Ni muda mwafaka sasa bila kuwaacha wapumzike tuanze mpango mkakati wa kuwaletea mapinduzi ya kifikra watanzania kupitia M4C(Movement for Change) Presha kubwa iilekezwe kwenye majimbo ya watu wa ccm bila kusahau tunapoongoza kuzidi kuimarisha jitihada za ukombozi.

Kanda ya kati watu bado wamelala sana sijajua kama wanajua thamani ya ukombozi wao na faida zake kwa vizazi vijavyo.hali kadhalika kanda ya kusini. Kanda ya ziwa, kaskazini na nyanda za juu kusini inahitaji kuongeza nguvu tu.

Huu sasa ndio wakati wa HAKUNA KULALA MPAKA KIELEWEKE. Ukombozi wa kweli ni lazima uanzie katika FIKRA ndipo tutakapoona faida ya ukombozi bila ya hivyo tutakuwa tunatwanga maji kwenye kinu.

N.B: Ushauri wa bure kwa pro-CHADEMA ni lazima turuhusu kukosolewa na kuchalenjiwa ili tuzidi kukomaa bila ya hivyo tutajenga chama ambacho kitaturudisha kwenye ccm mfu.
 
ushauri wako wa wabunge wa magamba kuhamia chadema haujakaa sawa, wananchi na watanzania kwa ujumla wake hawahitaji chama na sura za wabunge, wanahitaji maendeleo, ole sendeka atabadilisha nini akiwa chadema? uongozi sio mavazi, ni utashi wa kuwatumika waliokuchagua, hata shibuda alitokea CCM.
 
Mkuu Pasco, napata shida sana siku hizi kukuelewa nini hasa huwa malengo ya posts zako. Mapema jana ulisisitiza kuwa kuongoza kwa CHADEMA katika yale matokeo ya awali si lolote, na kwamba hata Busanda na Biharamulo ilikuwa hivyo, lakini CCM waliibuka washindi. Leo hii maono yako kuhusu Arumeru hayakuwa sahihi. Sasa tena unatoa maono mengine kuhusu 2015. Nikuulize: Huwa unapima upepo tu au huwa uko serious?
 
  • Thanks
Reactions: FJM
Mkuu Pasco, napata shida sana siku hizi kukuelewa nini hasa huwa malengo ya posts zako. Mapema jana ulisisitiza kuwa kuongoza kwa CHADEMA katika yale matokeo ya awali si lolote, na kwamba hata Busanda na Biharamulo ilikuwa hivyo, lakini CCM waliibuka washindi. Leo hii maono yako kuhusu Arumeru hayakuwa sahihi. Sasa tena unatoa maono mengine kuhusu 2015. Nikuulize: Huwa unapima upepo tu au huwa uko serious?

Wako kwenye postmoterm

Wapi tumekosea, kwa nini,na kadhalika.

Wanajipanga upya kwa 2015.
 
Pasco bonge la kilaza na kipofu, in short nibbendera fata upepo..

Halafu hana mamlaka yoyote kuhukumu mtu kama ni great thinker au laa!!

In short acha kujikosha, endelea kuosha vinywa vya magamba upate ujira wako..:rockon:
 
Kwani wao nikina nani mpaka wasing'olewe?Wajipange coz mpaka sasaivi tumeishajua ni mbinu zipi wanatumia kuiba kura ndo this time wamekosa pakupumulia kwa ulinzi wa kura wa umma!Jipange!
 
Hakuna chama kinaweza kuongoza nchi hii kwa kutegemea watu wa dini moja! Hamjaona matokeo ya Udiwani!
 
Umewasahau wazaramo, wagogo, wakwere na wazigua.
Mkuu mimi m.kwere tena wa Msoga kijijini, nyumbani karibu kabisa na kwao m.kwere wa magogoni lakini nilishafunguka macho siku nyingi tu. Wanaoniangusha wenzangu tu.
 
ushauri wako wa wabunge wa magamba kuhamia chadema haujakaa sawa, wananchi na watanzania kwa ujumla wake hawahitaji chama na sura za wabunge, wanahitaji maendeleo, ole sendeka atabadilisha nini akiwa chadema? uongozi sio mavazi, ni utashi wa kuwatumika waliokuchagua, hata shibuda alitokea CCM.

Huwa mara nyingi nina-discourage watu kufanya crosscarpeting bila kuzingatia itikadi.Labda nimuulize Pasco,ushauri uliowapa hawa jamaa umezingatia ideology? Ni lazima tufanye siasa based on ideologies ili wanasiasa fragile kama akina Lusinde automatically wawe nje ya political landscape.Tukiweza hili tutakuwa tumeleta mageuzi makubwa ya fikra,hakutakua na ideology za matusi na falsafa ya mapanga au marungu unaposhindwa hoja.
 
kuna kazi kweli kweli, kama mwaka mmoja range ya 6000 ninauhakika miaka mi5 magamba hawata pata kabisa kura.!
 
aint this a bit ecstatic...?

Am all for Change, but in politics one month is a long time let alone three years...

Winning or Loosing of Chadema will be determined by what is done from now to then not what was done before..
 
Pasco.

NB. Ukumbi wa jf ambao ulikuwa ment kwa ma great thinkers wenye great mind wanao duscuss ideas umegubikwa na low thinkers wenye simple minds ambao kazi yao ni kudiscuss people!.

Ukishasoma thread hii kama hujaona any idea ya kuchangia nakushauri usichangie!. Ukijiona huna na kuchangia kwenye hoja iliyoko mezani au mchango wako unataka kuchangia kumhusu mleta hoja Pasco badala ya kuchangia hoja yake, nakushauri bora jinyamazie tuu, tunataka michango ya great mind to discuss ideas not simple minds ambao kutwa kucha wanajadili watu!.

Pasco.

Kwanza niwapongeze maana ndio mwendo wa mtu mstaarabu!
CCM na CDM wote mmechuana kiume Arumeru Mashariki, lazima tukubali, the better man won
Hongera!

Hata hivyo nimeingiwa na wasiwasi mkubwa kwa kusikia "the week end rout".

CCM tukae chini na tutafakari imekuwaje. Viboko vya Kiwira, Mwanza Songea na hata huko Tanga bado vinauma.
We cannot be losing na kusema ni bahati mbaya.

Hongera washindi, na tukutane 2015!
Naamini tutakuwa tumejirekebisha.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom