Kinachoendelea CHADEMA Mitandaoni: Je, ni Ushujaa wa Mhe. Lema au ni Udhaifu wa "Kule Juu"?

Status
Not open for further replies.

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
50,442
113,451
Wanabodi,

Hiki kinachoendelea kwenye Mitandao ya Kijamii na haswa Jamiiforums, kwa Mbunge wa Arusha Mhe. Godbless Lema, kumkabili na kumshambulia Naibu Katibu Mkuu wa chama chake Mhe. Zitto Kabwe, bila ushahidi wowote, Jee tukiite ni kitendo cha Kishujaa?, kwa Mhe. Lema kuonyesha "ushujaa" wake wa kuzungumza ya moyoni bila kuongopa, hivyo kustahili sifa ya kuitwa "Shujaa wa Chadema", au ni dalili ya udhaifu fulani "kule juu", uliompa kiburi Mhe. Lema kuibuka na tuhuma na shutuma hizo mchana kweupe?!.

Chadema walipowatimua kina Shonza, chanzo kilianzia humu humu jf, niliandika waraka wangu kwa uongozi wa Chadema kuhusu kukiukwa kwa sheria, taratibu na kanuni, na kuwasihi viongozi wakuu wa Chadema "to act on suo moto" sio kusubiri barua za rufaa!, they did nothing bali kubariki maamuzi yale!.

Kulipotokea lile tifu la Madiwani wa Arusha, Mhe. Lema was at the centre stage, and played a very big role!, ilipofuata timua timua, he was spared, na sijui kama kuna chochote alichofanywa!, who is behind him?!.

Juzi katika kikao, Mwigamba amefanya "whister blowing" mambo ya ndani ya Chadema, Kamanda Lema ndie aliyeongoza kikosi cha "udukuzi", wakamdakua ndani ya kikao, na Mwenyekiti yupo!, wakamkabili, wakampokonya Ngamizi pakatwapajani yake (laptop computer), na kumshushia kipigo cha nguvu, huku M/Kiti akiangalia!.

Japo sikuwepo, ila nahisi (thinking aloud) baada ya pale, Mhe. Lema aliitwa na kupongeza kwa kitendo kile cha kishujaa!, hapa natumia hisia zaidi kuwajengea the motive behind haya mabandiko mawili ya Mhe. Lema humu jf jana na leo!.
Katika pongezi zile, dhana ya "usaliti" ikaongelewa!, na kuna "mtu" aliongelewa kama "msaliti!" ila kwa vile chama hakina ushahidi wowote wa moja kwa moja!, "hoja ikabaki hewani!".

Kama kawaida ya mgema akisifiwa!, "Shujaa" yule akaamua yeye hamuogopi mtu yoyote!, atajitoa mhanga kumkabili "msaliti" huyo!, na ndipo jana akapandisha uzi huu, na leo kumalizia na huu kwa kumtaja Mhe. Zitto Kabwe.

Wengi wa wachangiaji wa uzi ule, wanamsupport Mhe. Lema hadi kumpongeza kwa ushujaa, kitu pekee wasichoelewa ni kitendo cha Mhe. Lema kuzipandisha nyuzi zile, ni kitendo tuu, yaani ni action, kitu kikubwa na muhimu zaidi ni "the motive behind" mabandiko ya Mhe. Lema na most important ni "who is behind Lema!".

Kitendo cha Mh. Lema, mbunge mchanga wa juzi tuu bungeni, kuibuka na shutuma kwa mbunge mahiri kuliko wabunge wote wa bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kwa michango na hoja makini zenye mashiko kwa maslahi ya taifa, hakiwezi kuwa ni hivi hivi tuu!, huyo hawezi kuwa ni Mhe. Lema just acting alone under the pretex of "freedom of expression", bila backing yoyote kutoka "juu!".

Kwa watazama mbali, alichofamya Mhe. Lema ni " great act of insubordination" to his superiors, na kikiachwa kupita hivi hivi bila kukemewa, na Lema asipokuwa very seriously reprimanded!, then huo ushujaa wa Mhe. Lema, utakuwa sio ushujaa lolote, sio ushujaa chochote, bali ni confirmation ya serious weakness "kule juu!".

Kwa kumchafua Zitto humu mtandaoni, Mhe. Lema anastahili adhabu kama wale wachafuzi wengine wowote, japo nakiri kiwango cha adhabu sio lazima kiwe kikubwa kivile, kisije kula mtaji!, hivyo ili "kule juu" kujivua lawama, lazima Chadema iachane na adhabu za "double standards", vinginevyo hapa Chadema will be spairing the rod and will spoil the child!, mwaka 2015, itavuna baadhi ya mazao ya hawa spoiled broth ndani ya Chama!.

Na hata kama ikithibitika, tuhuma zote zinazoelekezwa kwa ZZK ni kweli, he shoild not be spaired!, Wakati wa Nyerere, tumeshuhudia mpaka "rais" wa "nchi" fulani akishikishwa adabu na Nyerere, itakuwa Naibu Katibu Mkuu wa kijichama fulani cha kina fulani?!.

Nawaomba "Kule Juu" ya Chadema, onyesheni strength to put your house in order, vinginevyo tutawalable "weak", na kama kama haka kajumba chao kadogo tuu pale Togo, kanawashinda tu put it in good order, lile lijumba likubwa pale Magogoni, mtaliweza?!, nani awape?!.

Namalizia kwa hili swali nililoanza nalo,

hiki kinachoendelea CDM Mitandaoni, Jee ni Ushujaa Wa Mhe. Lema?!, Au ni Udhaifu wa "Kule Juu?!".

Wasalaam.

Pasco.

-----------------------
Update 1

Hili ni jibu la Mhe. JJ. Mnyika kwa hisani ya Wanamabadiliko

Nimetoka kwenye vikao na Serikali muda huu na kupokea Sms za kwamba kuna suala hili ambapo kauli yangu inahitajika.

Katika hatua hii ya awali nieleze tu kuwa shutuma na tuhuma hizo za Lema kwa Zitto kutolewa kupitia mitandao ya kijamii ni kinyume na kanuni za chama ambazo zimeweka bayana mipaka kwamba viongozi kuhojiana au kukosoana ni kupitia vikao halali vya chama.

Nimewapigia simu wahusika lakini simu zao wote wawili zinaita bila kupokewa. Iwapo yeyote kati yao atasoma ujumbe huu, kabla ya kuendelea kujibishana na kutuhumiana afanye rejea ya katiba.

Kwa wanachama na wapenzi, suala hili litamalizwa katika vikao vyetu vya ndani kama ilivyokuwa kwa masuala mengine ya nyuma. Kuna masuala makubwa muhimu kwa taifa wiki hii ambayo hatupaswi kuachia muda wetu ukatumika kwenye malumbano ambayo yanaweza kuepukwa. Iwapo kuna mwenye malalamiko juu ya yeyote yanayohusiana na mambo ya Bungeni awasilishe rasmi kwa Katibu wa Wabunge wa CHADEMA hatua ziweze kuchukuliwa. Katiba, Kanuni, Maadili na Itifaki viheshimiwe.

JJSimu: 0784222222
 
Ni udhaifu wa mwenyekiti..
Kushindwa kudhibiti haya madudu yanayoendelea.

Au ndio tuseme Mwenyekiti na Katibu mkuu wake hawajui kinacho endelea?

Au wameamua kukiua chama kwa mikono yao wenyewe?
 
Team Lowassa tulie pale pale. Pasco ni rahisi sana ngamia kupenya kwenye tundu ya sindano kuliko wewe kuitakia mema CHADEMA.

Hivyo basi wacha tushughulike na Kiongozi Mkuu almaarufu Mwenyekiti wa wanafiki & wasaliti ndani ya CHADEMA.

Utaratibu aliotumia Lema, of coz, sio sahihi kwa maoni yangu; lakini ni forced and hence necessary just to deal with unattended matter in point.
 
This is calculated political move huwezi kuelewa....hata ukija kuelewa ni baadae sana.......CDM si kama CCM watu wanashidwa kukoromeana na kuongea KIUME....hii ya lema inafanya CDM iogopewe na kuheshimiwa......Hakuna mtu aliyopo juu ya chama ....soma vizuri lema alichoandika hajajizungumzia yeye kazungumzia nchi na chama....na ndo inavyotakiwa......CCM ndo watu wanajizungumzia wao kuliko chama na nchi........alafu haya mambo ya kusema sijui mbunge mchanga....sijui hajakomaa YAMEPITWA na WAKATI.....CDM demokrasia za kishamba na kubembelezana kama tupo kwenye vikao vya HARUSI kama wanavyo fanya CCM tuache....STATE PARTY lazima watu wasimame kiume na kuelezana ukweli....na kama mtu anakimbilia facebook au jamii forum...UNAMFUATA HUKO HUKO....HAKUNA KUBEMBELEZANA
 
Nimekereka sana na mabandiko ya mheshimiwa Lema, na najiuliza tu kwamba kabla ya bandiko lake, keshawahi kumweleza mheshimiwa Zitto mambo yote haya? Keshayapeleka kwenye vikao halali vya chama?

Kiukweli this is a very good example of insubordination?.

Miaka mitano au kumi ijayo maswali ya civics, development studies na general studies yanaweza kuwa kama ifuatavyo:

1. Elezea mchango wa msuguano kati ya Lema na Zitto ulivyoua matumaini ya ukombozi mwaka 2013.
2. Chadema ilijimaliza yenyewe. Fafanua
3. CCM ilishinda uchaguzi mkuu wa mwaka 2015 mwaka 2013. Changanua

Dah! Noma sana
 
Team Lowassa tulie pale pale. Pasco ni rahisi sana ngamia kupenya kwenye tundu ya sindano kuliko wewe kuitakia mema CHADEMA.

Hivyo basi wacha tushughulike na Kiongozi Mkuu almaarufu Mwenyekiti wa wanafiki & wasaliti ndani ya CHADEMA.

Utaratibu aliotumia Lema, of coz, sio sahihi kwa maoni yangu; lakini ni forced and hence necessary just to deal with unattended matter in point.
Utaratibu ni mzuri kwa sababu wanafki wote wanakimbilia facebook, jf na twitter wakati mwingine unawafuata huko huko ili ku-counter act sumu zao...
 
Anayemshambulia Zitto huwa haadhibiwi.

On top of that, Lema ni kijana wa Mtei, anaweza kusema chochote, wakati wowote, mahali popote, kuhusu yeyote na asiguswe na mtu.

Chadema ni chama kinachoendeshwa katika misingi ya kilaghai...
 
This is calculated political move huwezi kuelewa....hata ukija kuelewa ni baadae sana.......CDM si kama CCM watu wanashidwa kukoromeana na kuongea KIUME....hii ya lema inafanya CDM iogopewe na kuheshimiwa......Hakuna mtu aliyopo juu ya chama ....soma vizuri lema alichoandika hajajizungumzia yeye kazungumzia nchi na chama....na ndo inavyotakiwa......CCM ndo watu wanajizungumzia wao kuliko chama na nchi........alafu haya mambo ya kusema sijui mbunge mchanga....sijui hajakomaa YAMEPITWA na WAKATI.....CDM demokrasia za kishamba na kubembelezana kama tupo kwenye vikao vya HARUSI kama wanavyo fanya CCM tuache....STATE PARTY lazima watu wasimame kiume na kuelezana ukweli....na kama mtu anakimbilia facebook au jamii forum...UNAMFUATA HUKO HUKO....HAKUNA KUBEMBELEZANA

Mtu anatetea posho yake unasema anazungumzia nchi!
 
Huu ni utamaduni mpya ambao unaweza kabisa kusaidia nchi hii kupiga hatua mbele zaidi kama utajengeka na kutumiwa na jamii.

Zile zama za kuficha madudu ya viongozi katika kisingizio cha vikao vya ndani imepitwa na wakati. Mambo ya mewekwa wazi ni wajibu wa kila mmoja wetu kuya pima, kuya tafakari na kuchukua hatua.

Vinginevyo ni wape pole wale wanamikakati kuwa ndio umeshindwa hivyo waje na mwingine muda si rafiki kwao hata kidogo.
 
Huwezi kuandika tofauti na hvyo kwan Lema ni tishio kwa mgombea wako anaugulia jinsi kimada wake alivyogaragazwa.Kuhusiana na madiwani Arusha hyo inajulikana ZZK alikuwa mmojawapo wawaliowasapoti wale madiwani.
 
This is calculated political move huwezi kuelewa....hata ukija kuelewa ni baadae sana.......CDM si kama CCM watu wanashidwa kukoromeana na kuongea KIUME....hii ya lema inafanya CDM iogopewe na kuheshimiwa......Hakuna mtu aliyopo juu ya chama ....soma vizuri lema alichoandika hajajizungumzia yeye kazungumzia nchi na chama....na ndo inavyotakiwa......CCM ndo watu wanajizungumzia wao kuliko chama na nchi........alafu haya mambo ya kusema sijui mbunge mchanga....sijui hajakomaa YAMEPITWA na WAKATI.....CDM demokrasia za kishamba na kubembelezana kama tupo kwenye vikao vya HARUSI kama wanavyo fanya CCM tuache....STATE PARTY lazima watu wasimame kiume na kuelezana ukweli....na kama mtu anakimbilia facebook au jamii forum...UNAMFUATA HUKO HUKO....HAKUNA KUBEMBELEZANA

Acha Uongo wewe,mbona Mwigamba kasema kweli mkaja juu,si mnapenda Ukweli nyinyi???????????
 
mi nfikiri wote wataitwa na kamati kuu wachunguzwe hayawezi kupita hivi hivi. Tutawashangaa Kama chama kitakuwa na viongozi ambao hawaelewani lazima wapatanishwe kunusuru chama
 
Wakulaumiwa alimuandikisha Lema CDM(aliempa Kadi Lema ndo anayeiua CDM)sisi kama CCM tunataka Upinzani Madhubuti
 
Natamani Zitto afukuzwe kama mbwa CDM ili unafki na usaliti ufike kikomo
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom