CHADEMA kina wanachama wangapi?

CHADEMA kina wanachama wangapi?

Kamwe cdm isitarajie kuongoza nchi kwa sanduku la kura,kwani in wafuasi wakujaza mikutano lakini si wapiga kura.
HILO TUMELIONA 2010 NA MWEZI WA OKTOBA 2012 KWENYE CHAGUZI ZA MADIWANI.

Sijatoa comment maana nimetoka kutoa comment kwenye mada nyingine niliyoipitia karibuni ikieleza hayo kwa mapana zaidi kama ifuatavyo hapo chini. Inaonekana kuna ukweli mikutano ya Chadema kujaa mashabiki badala ya wapiga kura kama tunavyoona kampeni na matokeo ya chaguzi zinazotokea nchini. Mtoa mada nadhani ni Candid.

[h=1]Mwongozo Chadema baada ya uchaguzi mdogo[/h]Uchaguzi mdogo wa madiwani ulikamilishwa na wapiga kura nchini Jumapili October 28, Chadema kimepata funzo kubwa lenye kutoa tafsiri kadhaa zenye kuleta matumaini kwa wenye moyo mkuu au kufifisha kwa wenye moyo mchache.

Kauli ya Freeman Mbowe yazaa tunda la kwanzaMwenyekiti wa Chadema miezi michache iliyopita alitoa kauli ya kuwaasa vijana wasomi na wengine kujitokeza na kuchagua maeneo ya kugombea nafasi mbalimbali zikiwemo za uwakilishi ili waandaliwe. Wengi tulipongeza kwa utashi huo, kwa bahati nzuri katika uchaguzi huu mdogo wa Madiwani uliomalizika, kuna kijana mmoja msomi ambaye ameamua si kusubiria nafasi ya kugombea ubunge, bali ameamua kuanzia nafasi ya udiwani naye si mwingine bali ni diwani mchaguliwa wa kata ya Mlangali katika wilaya ya Ludewa ndani ya Mkoa mpya wa Njombe. Tunampongeza kwa kujituma, kutetena azima yake na kushinda. Kwa wengi haikuwa katika picha kwamba Chadema yaweza kupata kiti cha udiwani huko kuliko ngome ya CCM miaka nenda rudi kwa akina hayari Horace Kolimba, ni dalili kwamba mipango ikifanyika kwa umahiri na kumsimamisha mwenye sifa yawezekana, na imewezekana. Ni dhahiri Chadema imeshafunguliwa mlango Ludewa.

Diwani mchaguliwa ametoa mwanga kwa vijana wengi ambao pengine kwa kutokuwa na ujasiri wa kuthubutu wanahofia kitu wasichokuwa na hakika nacho kama watashinda au la, lakini kwa uchaguzi huu tumapata jibu kuwa wananchi wengi wanatuhitaji vijana katika kuleta mabadiliko katika jamii na maendeleo ya taifa letu. Chadema zoezi hilo limefana sana, wana mfano wa kuwafunda vijana wasomi wengi wajitokeze.


Kutofanya vizuri uchaguzi huu chadema sababu kusimamisha wagombea dhaifuMaeneo mengi ambayo nguvu kubwa ya Chadema imetumika tumekuja kushuhudia kutoambulia hata kiti kimoja. Unaweza kujengeka utetezi wa aina mbalimbali, lakini kubwa zaidi ni Chama kuwaandaa wagombea wanaofaa ndio tatizo. Chama kisitegemee tu jina la Chadema limpatie mgombea kura, ila auzike na wapiga kura ndipo waridhie. Tatizo kubwa ambalo naona wagombea wengi wa Chadema kula mwanguko wa mende ni kukosa sifa kulinganisha na wagombea wa CCM. Eneo hilo linatakiwa kufanyiwa kazi na Chama.

Mbinu za Chadema kujitanua zibadilishwe kuendana na upepo unavyovuma.Yale maandamano na mikutano ya hadhara inaonekana kutokuwa na nafasi kubwa kwa watanzania leo, kwani kama kuwasikia Chadema tumewasikia sana tu na jina la Chadema linalia masikioni mwa wengi kama mwangwi wa mlima Kilimanjaro. Tabia ya kinyonga kujibadilibadili rangi kuakisi mazingira yanayomzunguka ndiyo inayohitajika kwa Chadema sasa hivi.

Pendekezo kwa Chadema ni:


  • Kuachana na maandamano kwani yanachelewesha watu kuwajibika katika kujenga uchumi wa nchi
  • Kupunguza mlolongo wa mikutano kwani inapoteza nguvu na rasilimali za chama wakati chama sera zimeshafahamika.
  • Kuanza mkakati wa kupeleka wajumbe vijijini na mitaani kwa kusaka wafuasi watakao kuwa wanachama hai nyumba kwa nyumba na mtaa kwa mtaa hapo uchaguzi ujapo Chadema itakuwa na uhai wa kura kuanza kuhesabu wanachama hai walio nao kama CCM ifanyavyo, la sivyo watabaki kuvimbisha mishipa usoni majwakwani na kuambulia patupu kura zipigwapo.
  • Zoezi la kuwapata wanachama mijijini liwe endelevu na kuimarisha kuwa na wajumbe wa nyumba kumi wenye kuhakiki wanachama kwa kulinda na kuhamasisha uhai wao chamani.
  • Chama kuweka msingi vijijini na kuwa na wanachama ni mtaji mkubwa kwani ndiko kwenye wapiga kura wengi na majimbo mengi ya uchaguzi.
  • Chambo cha mawasiliano kitaifa iwe ni radio au TV ili harakati na sera za chama ziweze kuwafikia wengi badala ya kutumia tu blog kwa njia ya online ambayo mwenye kufikiwa ni Candid Scope badala ya walengwa wapiga kura walio wengi wa vijijini.


Posho za watumishi wa matawiniKufanya kazi kwa ridhaa kuna madhara yake. Mfano, unaposikia Katibu Mkuu wa Chadema analipwa Tsh. 7,000,000 huku watumishi wa matawini, katani, mikoa na wengineo wakifanya kazi kwa ridhaa huathiri utendaji na ukuaji wa chama. Chama kiwe na mkakati maalumu kuwapa posho walao kidogo kinachowezekana hawa watumishi.

Ruzuku inayopewa isielekezwe kwenye mikutano na maandamano tu, bali watumishi wa mawawini, katani, mkoani na wengineo wafikiriwe ili wafanya kazi kwa moyo wa matumaini zaidi. Pengine ongezeko la wadiwani sasa hivi litapandisha dau la ruzuku, hivyo ongezeko hilo bora lingeelekezwa kuwapa posho watumishi hao kila mwezi kila inapowezekana ili kupunguza manung'uniko ya hapa na pale na hivyo kuathiri utendaji na uwajibikaji wao. Kumbuka CCM inatumia mwanya wa ukata wa vyama vya upinzani kuwarubuni wapiga kura.


Kuandaa wagombea nafasi mbalimbali wenye sifaJitihada kubwa zinatakiwa kuwekwa katika kuandaa nguvu ya kutosha katika kuwaandaa wagombea katika chaguzi mbalimbali zijazo kwa kipindi kirefu kutosha. Isitumike ila ya zima moto. Kama alifanikiwa Nasari wa Arumeru mashariki kwa mtindo wa zima moto tusitazamie mtindo huo huo utatumika kufanikisha chaguzi nyingine, kwani wagombea wanatakiwa umma uwafahamu kwa kipindi cha kutosha na hivyo wanatakiwa kuwa karibu na maeneo yao wanakotegemea kugombea mara kwa mara.

Kuunganisha nguvu za upinzaniMwenyekiti wa Chadema ambaye ni mbunge na mkuu wa kambi ya upinzani bungeni, mara baada ya uchaguzi mkuu uliopita alisema kuungana kambi ya upinzani wapate muda kwanza kwa sababu ya majeraha ya uchaguzi. Hilo lilieleweka. Sasa majeraha ni karibu yamepona labda kama yapo ambayo yamegeuka kuwa donda ndugu.

Viongozi wa Chadema kitaifa wanatakiwa wataremke kutoka pale walipo ili wawafikie wenzao na kupika na kula meza moja chakula kinakuwa kitamu zaidi. Unyenyekevu ni siri moja kubwa katika kujiwekea malengo ya mafanikio. Ushupavu umewaweka wengi katika hali ya kubakizwa isolated. Ukiwa na mtoto jifanye kama watoto wafanyavyo, kwa wachezaji utajifanya mwanamichezo, wasomi utaongea mambo ya kisomi nk. Ndilo linalotakiwa Chadema wawaone wenzao vyama vya upinzani ni hazina katika kubuni, kupanga na kufanikisha mikakati ya kuikomboa nchi. Kura nyingi katika uchaguzi mdogo uliomalizika utakuta kama wangeunganisha nguvu CCM ingetelekeza viti vingi zaidi, sasa bora lipi? Kuthoofisha nguvu za CCM kwa kunyang'anya himaya yao kuwa chini ya umoja wa upinzani au kubaki na unyonge wa mwenye kiti kimoja abaki kivyake na wenye viti vingi wajisikie kujitutumua huku kuchukua dola ikibaki ndoto za kufikirika?

Viongozi kitaifa watambue kasoro zisemazo wajitahidi kujirekebishaViongozi wa kitaifa Chadema yanayolalamikiwa na baadhi ambao wamewahi kufanya kazi nao na kisha kuamua kujitoa hayawezi kubezwa, kwani lisemwalo lipo kama halipo laja, na tujue hawa ni binadamu kama tulivyo wengi tulivyo na kasoro nyingi tu za kimaumbili, kimaadili, kifikra, kujikuza, kujiona baora, na kiutambuzi. Siyo kubeza tu, wanatakiwa kujitathmini, maana kuendekeza sana tabia binafsi na nafsi ya mtu katika uongozi ni hatarishi katika nyanja za siasa. Yalisemwa, yanasemwa, lakini kuyaacha yapite tu kama tunataka mageuzi ya kweli hatutakuwa wa kweli na kuwatakia mema.
Hulka ya kiaongozi katika jamii:


  • ushirikiano na ushirikishi,
  • unyenyekevu na ukakamavu,
  • uvumilivu na ustahimilivu,
  • hekima na busara

ni mambo ambayo yanamjengea heshima na mafakio katika utumishi. Maamuzi ya papo kwa papo ni hatari, majuto ni mjukuu kwani maji yakishamwagika hayazoleki.

Viongozi wanatakiwa kuondokana na kulewa sifa, kulewa umati wa wahudhuriaji mikutano. Wanaohudhuria mikutano ya Chadema walio wengi ni mashabiki ambao si wapiga kura tofauti na mikutano ya CCM ambayo wahudhuriaji ni wapiga kura. Mkutano wa CCM wahudhuriaji 75% ni wapiga kura wake wakati wahudhuria wa Chadema kiwango hicho hicho wahudhuria ni mashabiki tu kama inapotokea tukio fulani watu wanafurika isivyotegemewa ndivyo Chadema wanavyotakiwa kusoma mwelekeo huu unavyowalaza chali katika chaguzi. CCM inapobeba watu kwa malori ni wanachama wake si mashabiki wakati mikutano ya Chadema wanaofurika ni mashabiki wasio wapiga kura. Hii ndiyo hali halisi ya tathmini yangu.

Diwani wa Mlangali, Ludewa ni changamoto na hasa kwa vijana wasomiVijana wasomi na wahitimu wengi vyuo vikuu tumekuwa na kasumba ya kuhangaika huku na kule huku tukilazimika kumaliza kandambili zetu kwa ajili ya kutembeza RESUME wakati tuna nafasi tele kama za huyu msomi mwenzetu kuelekeza nguvu huko matawini, vijijini, katani na wilayani kujenga msingi wa maisha. Ametufunza mengi, ametufunza mengi, wenye upeo wa masafa marefu wamempata, wenzangu mimi wenye kufikiria leo na kesho tu tutabaki kuchakaza kandambili kutembeza resume huku na kule.


 
Hivi tulivyokuwa tunawaambia ukubwa wa pua sio wingi wa makamasi mlikuwa hamtuelewi?

Chadema hakina viongozi wa maana, asilimia kubwa wana matatizo ambayo Watanzania wengi wanayatazama kwa mtazamo hasi.
 
Mbona hamuongelei the fact kuwa chadema haijapoteza nafasi ya udiwani hata moja, na kuwa imepokonya ccm nafasi zake za udiwani japo kwa uchache.
Sio mafanikio makubwa sana lakini.pia sio loss. Ccm is loosing the grip.
 
Hivi tulivyokuwa tunawaambia ukubwa wa pua sio wingi wa makamasi mlikuwa hamtuelewi?

Chadema hakina viongozi wa maana, asilimia kubwa wana matatizo ambayo Watanzania wengi wanayatazama kwa mtazamo hasi.
ohooo!!!! Gaidi ndani ya nyumba
 
Namkubali MM kwa makala zake mbali mbali, anao uhuru wa kimawazo pamoja na uhuru mwingine wowote kama binadamu. Ila kila mwanadamu ana utashi wake na ni vigumu kuwahi kupenda kitu halafu ukakichukia ghafla, labda uwe umefanyiwa kitu ambacho hakisameheki.

MM ni mwana NYINYIEM, hivyo ataendelea kukikosoa chama chake akiwa na ndoto kuwa siku mojakitabadilika. Ni muhimu kwa CDM kuwa na wanchama wake ili kuona inaungwa mkono kwa thati kiasi gani, lakini kwa angalizo kuwa NYINYIEM imekuwa ikipandikiza wanachama upande wa upinzani ili kuwavuruga.

Hivyo hili la wanachama linakuwa na walakini kidogo. Ushindi wa CDM unahitaji ushawishi wa wanachama wa vyama vingine pamoja na wasio na vyama. RE: uchaguzi wa 2010.
 
Wana Bodi hii ni sehemu ya andiko zito sana kwa wana CDM kutoka kwa Dkt. Kitila Mkumbo. Nimeona nilimwage hapa jamvini ili tuone ni kwa kiwango gani CDM inaweza kukata kiu ya Wanamageuzi wengi wanaotaka kuona mwaka 2015 kunakuwa na mabadiliko ya kiuongozi na hatimaye mfumo mbovu uliopo. Ni vema ukalisoma kwa umakini sana na kutafakari.

Chama cha siasa hupitia hatua kuu nne katika kufikia hatua ya kushinda uchaguzi. Hatua ya kwanza ni ya kisheria ambapo chama kinatambulika kisheria kwa kusajiliwa rasmi na kuruhusiwa kufanya shughuli za kisiasa.

Hatua ya pili ni kujulikana kwa wapiga kura, kwamba kuna chama cha siasa na kina viongozi fulani. Juhudi za viongozi katika kukiuza chama chao hukifisha chama hicho katika hatua ya tatu ambayo ni ufuasi. Ufuasi wa chama cha siasa huonekana katika mazungumzo ya kila siku ya wananchi na kwa jinsi wananchi hao wanavyoitikia mikutano na shughuli nyingine za umma kama vile kukichangia chama hicho.

Hatua ya mwisho ni kubadilisha idadi fulani ya wafuasi kuwa wafia chama, ambao ndio wanaoweza kukipatia chama ushindi, hasa katika mazingira makali ya ushindani.

Kwa sasa hivi hakuna shaka kwamba CHADEMA wameweza kupata wafuasi wengi kama inavyoonekana katika mazingira mbalimbali. Katika mazungumzo ya kila siku linapokuja suala la siasa unaona hamasa ya Watanzania kwa CHADEMA.

Kwa wale waliowahi kusafiri na gari mpya za CHADEMA (M4C) watakumbuka jinsi ambavyo wananchi huhamasika barabarani mara wazionapo gari hizi kwa kuonyesha vidole viwili. Madereva wa malori na mabasi ya abiria hawasiti kupiga honi mara wazionapo gari hizi, na hata baadhi ya askari wa barabarani hudiriki kuonyesha vidole viwili mara wazionapo gari hizi zikipita.

Mikutano ya CHADEMA imebadilika kabisa kutoka enzi za akina Mzee Mtei kuhutubia ‘miti' na sasa mikutano hiyo ikijaza maelfu kwa maelfu ya wananchi waliojaa hamasa na hamu kubwa ya mabadiliko.

Hata hivyo, bado CHADEMA hawajifikia hatua ya nne, ambayo ni muhimu sana katika kujihakikishia ushindi. Hatua hii ni ile ya kupata wafia chama. Ili kujihakikishia ushindi ni muhimu kabisa chama cha siasa kiwe na wanachama wafia chama.

Hawa ni aina ya wanachama ambao watakipigia kura wakati wowote iwe mvua, iwe jua. Hili ni kundi muhimu sana kujihakikishia ushindi katika mazingira ambayo wananchi wengi hawajitokezi kupiga kura, ambalo limeanza kuwa jambo la kawaida katika chaguzi zetu.

Ni kundi hili ndilo ambalo limebaki kama mpira wa kupumulia kwa CCM. Hawa ni watu ambao hawatakuja kamwe kugundua ubaya wa CCM hadi kitakapotoka madarakani na ni kundi hili ambalo limeiwezesha CCM kushinda katika uchaguzi wa madiwani uliokamilika wiki jana, ambapo katika baadhi ya kata idadi ya wapiga kura waliojitokeza walikuwa chini ya asilimia 20.

Nahitimisha kwa kutoa wito kwa wapenda mabadiliko. Kwamba kupenda na kutamani tu mabadiliko hakutoshi, inabidi kushiriki katika kuyasaka hayo mabadiliko. Tabia ya baadhi ya wapenda mabadiliko kudhani kwamba kikundi fulani cha watu katika chama fulani ndio wenye jukumu la kuleta mabadiliko itatufanya tukae katika mfumo wa utawala tuliouchoka kwa muda mrefu.

Makala nzima unaweza kuisoma hapa; Raia Mwema - CHADEMA inakua, CCM inasinyaa, lakini kwa kasi ndogo!


My Take
Huu wimbo wa CDM kujipanga mbona umekuwa ukiimbwa muda mrefu sana lakini hatuoni strategies za uhakika na za kudumu? Je kwa muda huu uliobaki nini kitaweza kufanyika ili kuiondoa CCM madarakani kwa maana ya kuifanya CDM kuwa na wanachama wake wa uhakika na kuweza kuipigia kura kiasi cha kuipiku CCM? Si kwambahata wana JF wengi ni wafuasi tu wa CDM na si watu walio tayari kukifia chama? Kazi kubwa inahitajika
 
Majibu ya maswali yako ngojo utokee uchaguzi mgodo utayapata Sumbawanga na Igunga, ama yoyote wa magamba arest in peace ila subri mziki wa 2015...
 
Chadema ni upepo tu kama upepo mwingine na utapita Kama Nccr
 
hata ccm haina wafia chama wa kutosha kama makala inavyotaka tuamini.sidhani kama ni hulka ya mtanzania kuwa mfia chama.wafia chama watatokea baadae na sio sasa.hata kama chadema ingekuwa na wafia chama wa kutosha lazima ungefika wakati wa kushawishi ''wafuasi'' au wasiokuwa na upande,kwa chadema wakati huo ni sasa na hakuna kisingizio wala sababu za msingi za kusema haiwezekani.it is a DO or DIE 2015
 
Majibu ya maswali yako ngojo utokee uchaguzi mgodo utayapata Sumbawanga na Igunga, ama yoyote wa magamba arest in peace ila subri mziki wa 2015...

Mkuu hayo ni maoni ya Kitila Mkumbo na ni mema sana kwa CDM ndiyo maana nimeyaweka hapa jamvini.Anachosisitiza ni haja ya CDM kuwa na wanachama ambao piga ua ni wapigakura wa uhakika dhidi ya CCM. Kwa maneno mengine kwa sasa CCM imechokwa lakini inasafiria nguvu ya wanachama wa aina hiyo (yaani ambao piga ua wataipigia kura tu).

Kazi ya CDM ni kuwa na database hiyo. Chukulia mfano CDM ikiwa na wanachama wa uhakika na watakaoipigia kura Milioni 3.Huu si mtaji mkubwa sana kwa chama? Kitabaki kinatafuta idadi ndogo sana ili kushika dola.
 
mi nawashangaa ccm wanashindwa kuchukua simple logic waliopiga juzi na chaguz zote za hivi karibun ni wale walioandikishwa 2010 tena wengi ni wazee na bado kuna matokeo chanya mengi kwa CDM. subirin daftari jipya na vijana wote hawa wawe kwenye daftari uone mzik wake
 
salaam sana wakuu,

Mimi ni mmoja wa mashabiki wa Chadema na najiita shabiki kwasababu sii mwanachama wa CDM japo naipenda kwa moyo wangu wote baada ya kugundua wana nia ya dhati ya kuleta mabadiliko Tanzania.

Mimi ni mmoja kati ya waliokuwepo Furahisha jana na idadi kubwa ya waliokuwepo pale si wanachama kwani hawana kadi.na wengi walikuwa wanatamani kununua kadi pasipokujua pa kuzipata nimeanzisha uzi huu ili nitoe ushauri kwa chama kuuza kadi na katiba kwa njia ifutayo.

1.katika kila mkutano wa hadhara kuwe na meza mbili au tatu maalum kwa ajili ya kuuza kadi na katiba za chama,na hili linaweza kufanyika kabla na baada ya mgeni rasmi kuhutubia.
naomba kuwasilisha
 
Mkuu nimekusoma, ila natofautiana na wewe kimtizamo; Kama wewe ni shabiki wa CHEDEMA basi hutufai na nashawishika kusema kusema wewe ni masalia au pandikizi.

Ni vyema ukafahamu ndani ya CHADEMA kuna wapenzi wa CHADEMA na siyo mashabiki kama unavyotaka kutuaminisha kwenye post yako. Funguka njomba Mashabiki wapo CCM na ndo maana wapo kima-slahi zaidi.
 
Haya mkuu..wahusika wamekusikia naamini watalifa nyia kazi
Tumaini Makene pita kwa kipande hii uchukue hii........
 
Last edited by a moderator:
salaam sana wakuu .
mimi ni mmoja wa mashabiki wa chadema na najiita shabiki kwasababu sii mwanachama wa cdm japo naipenda kwa moyo wangu wote baada ya kugundua wana nia ya dhati ya kuleta mabadiliko tanzania.
mimi ni mmoja kati ya waliokuwepo Furahisha jana na idadi kubwa ya waliokuwepo pale si wanachama kwani hawana kadi.na wengi walikuwa wanatamani kununua kadi pasipokujua pa kuzipata
.nimeanzisha uzi huu ili nitoe ushauri kwa chama kuuza kadi na katiba kwa njia ifutayo.
1.katika kila mkutano wa hadhara kuwe na meza mbili au tatu maalum kwa ajili ya kuuza kadi na katiba za chama,na hili linaweza kufanyika kabla na baada ya mgeni rasmi kuhutubia.
naomba kuwasilisha

cdm ni wajanja sana ,hawa washabiki wanawapa sana viroba mkuu ,ndio maana kwenye mikutano ya cdm vijana wanakuwa hawajitambui
 
Ndio wafanye utaratibu wa kuwafanya mashabiki wawe wanachama na kukusanya wanachama zaidi ili come 2015 wavune kura nyingi.
 
mkuu master peace,kama huna kadi ya chama wewe ni shabiki tu,japo unaweza kupiga kura kwa hicho chama na kuudhuria mikutano na kadhalika,kama mimi ni shabiki wa simba na sikosi kuwashabikia au kuwatetea vijiweni na wote wananijua hivyo ila sina kadi ya uanachama simba.nachotaka chama kiweke utaratibu wa kuuza kadi kwenye mikutano ya hadhara.
 
Kwa jinsi dunia ilivyobadilika kwa sasa naona tuanze kuwaza kuwa uanachama sio lazima kuwa na kadi. Vyama vya siasa vitafute namna ya kusajili wanachama wake na kutunza kumbukumbu. Mfano nina kadi za benki zaidi ya nne, nina kadi ya bima za afya, kitambulisho cha kazi, cha mpiga kura, leseni ya udereva, leseni ya biashara, tin number na mizigo mingine ya kadi kibao,,,, halafu unaongeza na kadi ya uanachama wa chama cha siasa, kadi ya uanachama wa timu ya mpira wa miguu, timu ya mpira wa kikapu, timu ya mpira wa pete,,,,, pia unazo za uanachama wa saccos, vicoba nk... Kwa kifupi unakuwa na mafile kibao.

Ushauri wangu ni kuwa CDM watafute utaratibu wa kupata wanachama wao kwenye ngazi za chini, mtaa au kata ambako ndio mtu unaenda kujiandikisha. Kumbukumbu yako inaweza kuwa namba ya uanachama na namba ya simu ambayo chama kitaitumia kukutafuta kama kuna mkutano au maandamano au kazi za kujitolea au kazi za ujenzi wa taifa, au email adress na hata facebook, twitter account. Unapoenda kununua kadi ya chama kwenye mkutano mkubwa kama ule wa jana Furahisha unakuwa umefuata mkumbo. Mfano wewe unakaa Igoma, badala ya kuchukua kadi yako Igoma unafuata furahisha mkutanoni kwa kuwa Mh Mbowe yupo, then mkutano ukiisha na mwaka mmoja baadaye utailipia wapi hiyo kadi, au utahudhuria mikutano ya tawi gani??

Huu mfumo waasisi wake MaCCM wanasema wana wanachama milioni 7 nchi nzima lakini JK hakufikisha hizo kura milioni 7, umepitwa na wakati. Tena napendekeza uanachama wa chama cha siasa ujumuishwe kwenye kitambulisho cha taifa ambapo kumbukumbu za uanachama zinahifadhiwa halafu unatembea na kitambulisho kimoja kwa matumizi yote.
 
Back
Top Bottom