CHADEMA kina wanachama wangapi?

CHADEMA kina wanachama wangapi?

sasa huyo adui si ndo anatakiwa kuwapa hizo leseni za TV? na huyo huyo adui ndiye anasimamia mifumo yote ambayo CDM itatumia. Huwezi kumkwepa adui na adui kama CCM ana uwezo wa kutosha kabisa wa kujua CDM inawanachama kiasi gani na anatumia kwa makini ujuzi huo. Think about it......

Hapa unaanza kupotoka MM kama sio kupotosha . Tumia lugha rahisi kufikisha unachotaka kuwasilisha .
 
MK, ni kweli; Lowassa ni noma. kwi kwi kwi....
Mnamuendekeza sana kiasi amekuwa kama jinamizi kwenye ndoto zenu..kila muendapo yupo. Wengine hatumpi hata umuhimu wa kuvinjari kwenye mawazo yetu. He is "has been "
 
Nyie endeleeni kuwapamba kwa mashada ya majani na kuwapaka mafuta kwa mgongo wa chupa mkidhani mnawasaidia. Watengenezeeni uduru wa kila namna ya kwanini hawakufanya vizuri sasa na kwanini hawakufanya vizuri 2010 au kwenye zile chaguzi za diwani zilizopita. Mjiandae kuwatengenezea udhuru mwingine wakikosa kufanya vizuri 2015.. na 2020. Mtakuja kushtuka sote tunawajukuu na vitukuu huku CCM kizazi cha nne kikiwa kimeshika hatamu ya madaraka.

Inasikitisha kuona kuwa unapenda kuonekana kuwa wewe ni msaada mkubwa kwa CDM kipindi inaposhinda,nilianza kukusoma kipindi cha kampeni Igunga na Tengeru . Kama imani yako kuhusu CDM ndio sanaa ya siasa uliyoionyesha TENGERU basi wewe hustaili kuuiliza wala kujadili kwa lugha nyepesi kiasi hiki .
 
dampen kuanza KIPINDI CDM kwa mkubwa msaada ni wewe kuwa unaonekana uwe

Inasikitisha kuona kuwa unapenda kuonekana kuwa wewe ni msaada mkubwa kwa CDM kipindi inaposhinda,nilianza kukusoma kipindi cha kampeni Igunga na Tengeru . Kama imani yako kuhusu CDM ndio sanaa ya siasa uliyoionyesha TENGERU basi wewe hustaili kuuiliza wala kujadili kwa lugha nyepesi kiasi hiki .

Tengeru kulikuwa na nini usije kuwa unaanza kuota visivyokuwepo.
 
Naona hili swala la uanachama liunganishwe na kurugenzi ya mawasiliano. Mimi nilichukua kadi pale makao makuu, hawakuchukua no yangu ya simu na wala sikumbushwi kama ada ya mwaka ya uanachama imekwisha. Ni mpaka niende mwenyewe.

Nashauri kuanze kuwekwa proper recording na kuwe na mawasiliano hasa kwa njia ya sms baina ya chama na wanachama.
 
Makamanda endeleeni kulumbana; ushauri nasaha CCM tupo kwa ajili yenu!

Chama
Gongo la mboto DSM
 
haya bana; miaka ishirini baadaye mko kwenye phase one; mkifika phase five itakuwa mwaka gani? 2099... ?........

Wewe Mzee Mwanakijiji uko confused, ni bendera fuata upepo, huna unachokiamini wewe, usifikiri tulioamua kupigania mabadiliko ya hii nchi tunajali ni lini yatatokea.

Inaweza ikawa karibu sana au mbali sana, ukichukua jembe kulima ukaanza kuangalia nyuma wewe hufai! Mkakati wa M4C hauna miaka ishirini una miezi takribani saba toka uanzishwe.

Ndo maana nasema wewe huelewi context za siasa za hii nchi tuachie sisi tunao jua tunapambana na nini! Kuna siasa za Kishenzi(Barbaric politics) kwenye hii nchi, I wish ungekuwa mstari wa mbele kwenye uchaguzi mmoja tu, halafu tuone utatoka na tathmini gani.
 
Jamani, mbona hili zoezi ndio kiini cha m4c. Kujenga matawi imara, kuhamasisha wanachama, kuwa na uongozi imara, na baadaya kuwa na national data base. Msiwe watu wa kulaumu tu, tuulizeni tulio front. Huu uchaguzi mdogo usiwawehushe. M4C ndio inapamba moto, tena kwa moto wa ajabu, maana tugundua kwamba inawezekana, kama tukishiriki.
 
Mnamuendekeza sana kiasi amekuwa kama jinamizi kwenye ndoto zenu..kila muendapo yupo. Wengine hatumpi hata umuhimu wa kuvinjari kwenye mawazo yetu. He is "has been "........

Sawa mkuu, lakini katika hili umepotoka, ni mwelekeo huu potofu wa kutotambua madadiliko ni 'process' ndefu ambao unawafanya watu wajaribu kukonect dots....; a fear of the unknown inakuwa generated dhidi yako hasa ukizingati wewe ni political analysist makini sana, una wafuasi wengi hivyo wanaogopa usiwapoteze 'ideologically'.

Mabadiliko tunayoongelea siyo kuweka sukari kwenye chai, au chumvi kwenye 'supu' halafu unahonja...

ZZK kwa mfano, pamoja na historia yake nzuri kisiasa wengine tunamchukulia kuwa ni mwanasiasa Tata, hii ni kutokana na anayoongea na kutenda yanakuwa yamepindapinda, mwanzoni nilifikiria jimboni kwake (ambako ndiko nami natokea) hawauoni huo utata, Mwaka juzi nilitembelea kule kwenye shughuli za kijamii (nilikwenda kumzika baba yangu mzazi) 'to my suprise' wazee kwa vijana nilioongea nao wanauona utata wa mwanasiasa wetu huyu jasiri.

hata wewe pia ni mchambuzi wa mambo ya kisiasa mzuri lakini mtata at some point.....
 
Naona hili swala la uanachama liunganishwe na kurugenzi ya mawasiliano. Mimi nilichukua kadi pale makao makuu, hawakuchukua no yangu ya simu na wala sikumbushwi kama ada ya mwaka ya uanachama imekwisha. Ni mpaka niende mwenyewe.

Nashauri kuanze kuwekwa proper recording na kuwe na mawasiliano hasa kwa njia ya sms baina ya chama na wanachama.
Unaweza kuniambia ni chama kipi cha siasa kinachopigia watu simu waende kulipia ada zao za uanachama? au klabu ipi kati ya Simba na Yanga yenye utaratibu huu? au unadhani utaratibu wa Insurance brokers kuwapigia simu wateja wao siku chache kabla ya bima zao ku expire ndio unatumika sekta nyingine?
 
Tengeru kulikuwa na nini usije kuwa unaanza kuota visivyokuwepo.

Unajua mchango wako kupelekea ushindi Tengeru na wadau wengine ,kama Mzee Mwanakijiji ndiye yule aliyesimama na makamanda kuonyesha sanaa ya siasa mpaka ushindi ukapatikana basi hata kipindi hichi ambacho unaona chama kinakosa kuelewa hiyo technique unayoipigia upatu (Idadi ya wanachama) unastahili uulizwe wewe umefanya nini ili majibu yapatikane na sio kuuliza maswali mepesi kiasi hiki humu jamvini. Ndio maana mwanzo niliandika kuwa wewe una jambo unataka kulieleza ila unasoma upepo kwa lugha ya picha.
 
Last edited by a moderator:
Wanachama wa chama cha siasa (siyo mashabiki) ndio hujenga msingi wa chama (political base). Siyo wanachama wenye kadi tu bali wale ambao wanazo kadi, na wanajihusisha na shughuli za chama. Watu wanaopuuzia kujua idadi ya wanachama au hata kuwa na umuhimu wa wanachama wenye kadi wanashindwa kuelewa (au hawataki) kuwa chama husimama migongoni mwa wanachama wake siyo kwa washabiki wake.
 
Hii ndio aina ya mijadala ambayo inaweza kujadiliwa milele bila kwisha wala ku-accomplish anything of tangible or significant result.

Zipo sababu nyigi lakini mojawapo ni kuwa mara nyingine majibu sahihi yameonekana ni rahisi sana hivyo kupuuzwa i.e. too simple to be true.
 
Kamwe cdm isitarajie kuongoza nchi kwa sanduku la kura,kwani in wafuasi wakujaza mikutano lakini si wapiga kura.
HILO TUMELIONA 2010 NA MWEZI WA OKTOBA 2012 KWENYE CHAGUZI ZA MADIWANI.
 
Unaonekana kama una hoja lakini hujaiweka vizuri na umeandika haraka haraka. Unashauri nini kifanyike?
 
Kamwe cdm isitarajie kuongoza nchi kwa sanduku la kura,kwani in wafuasi wakujaza mikutano lakini si wapiga kura.
HILO TUMELIONA 2010 NA MWEZI WA OKTOBA 2012 KWENYE CHAGUZI ZA MADIWANI.

Na wale wanunuzi wa shahada za kupigia kura na kumwaga rushwa ndio nani vile kama kweli CCm Magamba mnayaweza msimwage rushwa tuone kama mtatoka kama kweli mna wapiga kura iweje mnunue kura za wengine mkiwatumia kwa shida zao??Naomba wewe mtoa mada mwanafunzi wa chuo cha kata ujibu fast,Ke....nge.... mkubwa wewe
 
Kamwe cdm isitarajie kuongoza nchi kwa sanduku la kura,kwani in wafuasi wakujaza mikutano lakini si wapiga kura.
HILO TUMELIONA 2010 NA MWEZI WA OKTOBA 2012 KWENYE CHAGUZI ZA MADIWANI.

kaa chini, omba maji, tuliza mzuka... lete hoja mkuu
 
Dada KIBE naona Leo umeacha kazi yako ya kumlisha mtoto unakurupuka kuanzisha thread usisahau kuosha na vyombo
 
Last edited by a moderator:
Kamwe cdm isitarajie kuongoza nchi kwa sanduku la kura,kwani in wafuasi wakujaza mikutano lakini si wapiga kura.
HILO TUMELIONA 2010 NA MWEZI WA OKTOBA 2012 KWENYE CHAGUZI ZA MADIWANI.

mm mmoja wao
 
Back
Top Bottom