CHADEMA kina wanachama wangapi?

CHADEMA kina wanachama wangapi?

Wanachama wa Chadema ukitaka kuwaona subiri mikutano ya Chadema Chopa akitua utawaona, Chopa ikiondoka na wao wanaondoka.

Maswali ya MMK yamelenga kama ulivyobainisha. Kwa nini chama kinashindwa wakati kinapenda kuwaaminisha umma kama kina wanachama, wapenzi na washabiki wengi zaidi ya vyama vingine nchini.

Unakumbuka pale walipokuja na jina lao pale uwanja wa jangwani eti kwa vile kulikuwa na nyomi ambayo haijawahi kutokea.

Wana CDM Hawapendi kuambiwa ukweli. Halafu nafikiri wengi wanapumbazwa na hii mitandao wakati uwanja hasa wa mapambano uko vijijini ambako Watanzania wengi wanaishi. Viongozi wao huwa wanaenda vijijini na chopa kama watalii.

Nafikiri hawa makamanda wanapambana na adui ambaye siye. Hawawezi kumpata na kumuua adui kupitia mitandao ya 'kijamii'.
 
Jipange upya mkuu, hata kama ulikuwa na nia njema na kutaka tujadili kitu fulani faida za kuwa na mtaji wa Wanachama lakini hapa umekurupuka, na thread yote imekuwa useless.

Swali la idadi ya Wanachama wa Chadema unaweza kujibiwa na uongozi wa Chadema tu na siyo JF.
mkuu Viongozi wa cdm jf hawapo au ?
 
Unapoteza muda wako kumsikiliza Kibonde................ameambulia zero mlimani hapo juzi...shame on HER
 
Mwita Maranya ahsante kwa ufafanuzi lakini idadi ya wanachama wapya 170 ambao hupewa kadi mwishoni mwa mkutano anayewaandikisha majina na mtu mmoja au wanaandikwa na zaidi ya mtu mmoja; chukulia unatumia dakika moja kuandikisha mwanacha mmoja, 170 ni sawa na masaa matatu (170/60); na labda kazi mnaanza nusu saa kabla ya muda mnaoruhusiwa kisheria kuendelea na mkutano

Mkuu kama umenisoma vizuri nimesema hiyo idadi ya 174 ilipatikana katika mikutano mitatu. Hata hivyo kwa ufafanuzi zaidi tunapofanya mikutano tunakuwa tumjiandaa kwa kuweka watu wanaotoa kadi kwa wanachama wapya, hasa tunawatumia makatibu wa matawi na kata katika eneo la mkutano. Tunawatumia makatibu ambao ndio wenye jukumu la kutunza kumbukumbuza kiofisi.

Kama nilivyosema, baada ya mikutano majina ya wanachama wapya hukusanywa na kuchambuliwa ili kufahamu kila mmoja anaishi wapi ili sasa mawasiliano rasmi yafanyike na uongozi wa eneo husika waweze kumfuatilia mwanachama huyo, na wakati huo huo na wanachama wapya hao huelekezwa mahali ofisi na viongozi wa matawi na kata zilipo katika eneo analoishi ili aweze kuwasiliana nao.
 
Nafikiri hawa makamanda wanapambana na adui ambaye siye. Hawawezi kumpata na kumuua adui kupitia mitandao ya 'kijamii'.

Ndio maana sisi ambao tunafanya siasa majukwaani na mitaani kila mara tunawaasa nanyi wenzetu msiishie kubonyeza keyboards tu shukeni huko mitaani kwenu mkasaidie kuwaelimisha wananchi wenzenu na kuwasaidia kukabiliana na hadaa za ccm.

Sisi tunaopigana huko kwenye "battle ground" ndio tunajua ugumu na urahsi wa kupambana na ccm pamoja na vyombo vyake vya dola, na tunapowaambia kwamba tunahitaji support yenu hamtaki kutuelewa, zaidi sana mnachojua kufanya kwa umahiri mkubwa ni kutupa lawama kwa viongozi na wanachama, na wengine mnakwenda mbali kwa kutaka watu wajiuzulu bila kutaka kujua juhudi wanazofanya kwa ajili ya mustakabali wa maisha ya wanachi wanyonge wa nchi hii.
 
Ila inapasa kuwa CHADEMA kuwa na data kamili za wanachama wake hata kwa kuweka kwenye internet na mitandao ya kijamii na kila namna ya wanachama wake
 
Kuna watu wanataka Mzee Mwanakijiji aisifie CHADEMA kwa "mazuri" yake lakini hao hao hatuwaoni wakiisifia CCM kwa "mazuri" yake!
 
Last edited by a moderator:
Kuna ugonjwa fulani MMM ameanza kuugua siku za hivi karibuni,ni jambo la wakati tu utajidhihirisha wazi

Mzee Mwanakijiji huenda nikweli anataka mabadiliko lakini anadhani kuishinda CCM yenye mfumo wa zaidi ya miaka hamsini ni rahisi! M4C ina phase zaidi ya tano, na kwanza ndo tuko phase one, ambayo ni awareness ya chama! Hii level ni kuwajengea wananchi uelewa sawa juu ya mabadiliko na kumobilize supporters wa chama country wide na kutengeneza mtandao, ni kukipeleka chama chini kwa wananchi! Phase hii ya kwanza inakumbana na mifumo, sheria, na taasis gandamizi ambazo zimejijengea tabia ya muda mrefu kufanya mambo kinyume as if hivyo divyo ilivyo ndo maana unakuta hata mauaji yanatokea pale CHADEMA inapojaribu kuchallenge mifumo gandamizi ili wananchi wafikiwe na elimu ya chama na hatimaye mabadiliko, ni rahisi kusema watu wanayosema, lakini mngejua kuwa CCM haiko tayari kuachia madaraka kwa garama yoyote msingekuja na lugha zenu hizo za kejeli kwa kazi ambayo imefanywa na viongozi katika mazingira magumu sana! Mimi nawakubali mawazo mnayoyasema yote ni mazuri lakini lazima tujue pia hali halisi ya mazingira ya siasa za tanzania, CCM wanaua watu! Wanatishia watu, maisha ya wanachama wa chadema yako hatarini 24/7, hii inaogopesha watu wengi sana, CCM wanatumia fedha, kwa kufanya kampeni na pia kuhonga, pia wana mfumo wa chama ambao ni mfumo dola umejengwa kwa fedha na walipa kodi for years. Napendekeza badala ya kulaumu tushirikiane kukijenga chama na kukiaandaa kwa ajili ya mabadiliko! Tatizo kubwa na watu wengi wanataka wao ndo wao beneficiaries wa mabadiliko yatakayo letwa na chadema, ukiwaza hivyo utakata tamaa mapema, cha msingi pigania mabadiliko kwa ajili ya vizazi vijavyo hata kama haitatokea in your life time, lakini watoto wako au watoto wa watoto wako watakuja kufaidika!
 
Last edited by a moderator:
Sikutegemea mtu kama MMM aje hapa na hadithi za kumquote Yusuf Makamba, huku ni kupungukiwa kwa hekima na maarifa.

Hivi hii JF ina hawa Members?
Registered Members: 96,985

take that number devide by 3,you will get the answer, maana watu wana ID tatu tatu humu ,sawa tu na mwanachama mmoja kuwa na kadi ya CCM,CHADEMA na CUF. Tofauti hapa tunajisajili kidigitali zaidi na kule ni kianalogia zaidi.
 
mimi nina simcard 3 nabadilisha kila ninapoihitaji...

Vivyo hivyo vote yangu toka 1995 huwa inaenda NCCR, CUF na CDM kutegemea na uwezo wa wagombea wa vyama hivi.
 
Matokeo ya udiwani ni ujumbe mzuri kwa ukaidi wao.
Hapa sina hakika kama nakubaliana nawe. Chadema from nothing to five unadhani kidogo hiyo? I mean viti vilikuwa vya CCM na vimekwenda cdm. Nilidhani its something. Mkubuke Roma haikujengwa kwa siku moja. Its a process, hata kama kutokana na kuchoshwa na mambo ya CCM watu wanataka mabadiliko leo leo. Hii haitawezekana unless you are dreaming of mapinduzi
 
Kama kweli wewe Mwanakijiji ni Man of his words, ulishindwa vipi kutumia busara hizi kwa chama chako cha CCJ na kikashindwa kufanyiwa uhakiki na kikafa kabla ya kusajiliwa, is this simple Mathematics kama unavyotaka kutuaminisha wakati wewe mwenyewe uliferi kwenye hili?
.....

Matola ebu tuwekee iyo thread ya Mwanakijiji anayoikampenia CCJ..Maana nashindwa kuelewa hawa CCJ walikuwa wanagombea nini!?
Au pengine ukumuelewa kama ambavyo haujamuelewa hapa..!!
 
Matola ebu tuwekee iyo thread ya Mwanakijiji anayoikampenia CCJ..Maana nashindwa kuelewa hawa CCJ walikuwa wanagombea nini!?
Au pengine ukumuelewa kama ambavyo haujamuelewa hapa..!!.......

Si nilikwambia wewe huna akili? muulize wewe mwenyewe Mwanakijiji wakati anaamasisha na kutushawishi tujiunge CCJ Chadema haikuwepo? mimi sina muda kuelimisha watu half empty glass, shake well before use.
 
Back
Top Bottom