Hadi mwaka 2010 Chama cha Mapinduzi kilikuwa na wanachama takribani milioni tano kwa mujibu wa alkiyejuwa katibu mkuu wakati ule Bw Yusuph Makamba. Idadi hii ni ongezeko kutoka wanachama milioni tatu hivi waliokuwepo mwaka 2000. Ili kuweza kuelewa mwelekeo wa chama kikuu cha upinzani nchini na hasa kukubalika kwa ajenda yake ni vizuri kujiuliza CDM sasa hivi sasa wanachama wangapi wente kuveba kadi? Na wanachama hawa wametawanyika vipi katika nchi yetu?
Idadi ya wanachama wa chama cha siasa (siyo mashabiki) inaweza kujulikana to almost exact figures.
a. Mwanachama anapojiunga analipia kadi kwenye tawi lake
b. Kila tawi lina orodha ya wanacham wake
c. Mwanachama akihama tawi kuna utaratibu kuwa kule anakoenda atajiunga na tawi jipya na rekodi zitaonesha hivyo
d. Kila tawi linatuma idadi ya wanachama wake makao makuu
e. Kuna utaratibu wa kuupdate idadi ya wanachama (wanaoingia na kutoka)
f. Kwa kuangalia idadi hizo unaweza kuona movement ya wanachama na kupata demographia ya wanachama wako (vijana, wazee, kina mama, mijini, vijijini n.k).
g. Kulipa ada za kila mwezi za chama. Mfumo mbaya ni kulipa kwa mwaka! Ni vizuri kuweka quarterly fees ili kila baada ya miezi mitatu walio wanachama (loyal party members) wanaenda kulipa ada zao. Hii inakupa mwanga.
h. censored.
Sasa kujua hili la wanachama ni kuijua base yako. Huwezi kujenga chama kwa kutegemea independents au undecided voters. Ni kwa kutegemea your core supporters ndio chama kinaweza kusimama.