KIMBURU
JF-Expert Member
- Jan 12, 2011
- 210
- 189
Akiongea leo jioni na wakazi wa Iringa mjini Mpendazoe Sitta, Mwakyembe na Nape ndio waanzilishi wa CCJ na kudai kuwa Sitta ndiye aliyetoa Furniture za chama, alilipia pango la ofisi na ndiye aliyeasisi na kuratibu mchakato mzima wa "online registration".
Aidha amedai kuwa Stta na Mwakyembe wapo kwa maslahi yao binafsi kwani wamepoozwa na uwaziri, na wanaaendelea kuitumikia serikali ambayo wanajua ni ya kifisadi na kuwasahau wananchi.
Naye mbunge wa Kigoma kaskazini Zitto Kabwe ameyaponda vikali magazeti ya Uhuru, Jamboleo n.k ambayo yanaandika habari zinazodai kuwa CDM inampasuko. Amesema kuwa yeye na Mbowe hawana Mgogoro wowote na kwamba mahusiano yao yalianza muda mrefu; na kuwa yeye amekuwa maarufu kwasababu ya Mbowe na juhudi za kuwatenganisha hazitafanikiwa milele.
Naye Dr Slaa (PhD) amesema Serikali ya Tanzania haina sifa ya kulipwa fedha za rada kwani wao ndio waliomsafisha Chenge kuwa si fisadi wakati ni fisadi na hivyo kupoteza uaminifu wao kwa serikali ya Uingereza.
Naye kamanda Freeman mbowe ameelezea kwa kirefu mauwaji ya Tarime na kudai kuwa baada ya kuhitimisha mkoani Iringa watahamia Tarime ambapo wameshamtuma Lema, Mabele Marando na Tundu Lisu.