Chadema Iringa Mei 19, 2011: Picha na Matukio

Chadema Iringa Mei 19, 2011: Picha na Matukio
























Wahehe waliwapiga wajerumani
chacha kweli watababaishwa na m k w e r e ?​
 
chaajabu hakuna hata media moja iliyoonesha hili nyomi kwenye habari wameishia kutuonesha Kagasheki tu...pipoz power mpaka kigeleweke lkn sasa CDM ijipange kumiliki media zake ili tuepukane Na hizi za hawa wenye media ambao pia ni makada wa magamba,IRINGA asanteni kwakujitokeza kwa wingi naa hiyo,najua mzee wa kaya hili nyomi leo analitazama ugenini huko alipoenda kwenye safari zake zisizo na tija kwa wanyonge
 
Hakika Iringa imeweka historia tangia wanairinga wapate ukombozi,umati ulikuwa mkubwa sana,VIVA......CHADEMA
 


















Mkombozi ni CDM bado tutaanza
kuwapiga bakora Chichiemu .... ..

​
 
DSC04677.JPGDSC04697.JPGView attachment 30354DSC04708.JPG
pencil.png
 
​


​



​



​


Uongo wa JK wa kuwalinda EL, RA, Chenge na Mkapa
hauwezi kuvumilika, ati anasubiri wakombe tena pesa za walipa kodi ... ​



Picha kwa hisani Daudi Mchambuzi pamoja na Nkasoukumu​
 







Saa ya ukombozi imewadia .. .. ​

njia ile ni nyembamba iendayo uzimani,dalili za mafanikio na ukombozi zipo karibu,tuombe,tusali na ikibidi tufunge ili mungu atupe nguvu ya mapambano ya haki yetu.imeandikwa abishae hodi hufunguliwa,aombae hupewa.mungu ibariki tz mungu ibariki chadema.
 
CDM wanatisha, nafikiri CCM sasa hawalali maana hata huko Bungeni safari hii kwenye bajeti kama wakigangamaa namna hii itakuwa poa sana.
 

Chadema kimeshutumiwa kwa mengi. Msishangae kusikia kutoka kwa NAPE kwamba hawa wote walioandamana kule Iringa jana hawakuwa watu wa Iringa bali waliletwa na CDM kutoka Kilimanjaro.

Nyie wenyewe si mnaona hizi picha zilizopigwa kwenye maandamano ya Iringa ? Sasa nimeamini kwamba CDM ni chama cha Wachaga !


IMG_8207.JPG


IMG_8209.JPG


IMG_8229.JPG


IMG_8233.JPG

paperclip.png
Attached Thumbnails
 
msameheni nape,hajitambui kabeba gunia la misumari sasa inamchoma anachanganyikiwa. kwani hata sumbawanga na songea ni wachaga?. dalili za mtu aliyefilisika kisiasa ndo hizo. keep it up chadema
 
Thursday, 19 May 2011 22:39

abwezitto.jpg


Naibu Katibu Mkuu wa Chadema, Zitto Kabwe

Boniface Meena, Iringa

NAIBU Katibu Mkuu wa Chadema, Zitto Kabwe amemtaka Waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja kuachia ngazi kwa kuwa tangu amekaa kwenye wizara hiyo, mgao wa umeme umekuwa kitu cha kawaida na kusababisha uchumi wa taifa kuporopoka kwa kasi.

Alisema kuwa waziri huyo amekuwa sasa ni waziri wa mgawo badala ya kuwa waziri ambaye angewasaidia wananchi kuondokana na adha ya umeme unaowawezesha vijana na watu wote kufanya kazi.

"Huyu si waziri na hafai kwa kuwa mgawo kila siku saa 16 kukosa umeme ni hatari kwa makampuni, wafanyabiashara na wananchi kwa jumla,"alisema Zitto na kuongeza:

"Umeme wa mwaka huu kutoka Januari hadi Mei, umeikosesha Serikali kiasi cha Sh850 bilioni. Mwaka 2006 mgawo uliozaa Richmond ulisababisha uchumi kushuka kwa asilimia moja, kitu ambacho ni hatari,"alisema.

Kauli ya Zitto imekuja wakati Tanesco ikiwa umetangaza kuanza kwa mgawo wa umeme ambao ulianza jana na utaendelea kwa wiki kadhaa zijazo. Mgawo huo wa umeme unaelezwa kwamba utakuwa unadumu kwa saa 16 kwa siku na hivyo kuathiri shughuli za kiuchumi.

Alisema kuwa aliposema kuwa Serikali haina fedha hivi karibuni alishambuliwa na viongozi wa Serikali, lakini taarifa yake imewaamsha kwani Serikali na kutaka mishahara iwe inalipwa tarehe 25 ya kila mwezi.

"Nimeambiwa Wizara ya Fedha na Uchumi imewaagiza wakuu wote wa Serikali kuwa ikifika kila tarehe 25 ya mwezi lazima wafanyakazi wawe wamelipwa la sivyo watawajibishwa,"

"Tumekwenda vijijini kabisa ambapo raia wa nchi hii wanaishi pamoja na wakulima ambao ni uti wa mgongo wa taifa, lakini hali zao ni mbaya na Serikali inaendelea kuwakandamiza wananchi hao na hawana pa kusemea,"alisema Zitto.

Mbowe na mauaji Tarime
Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe jana alitoa tamko la chama kuhusu mauaji ya Tarime akieleza kuwa haiwezekani polisi wakaendelea kuua raia hivyo wanahamia Tarime mpaka kieleweke.

"Tutahamia Tarime kwa kuwa kwa mujibu wa taarifa ya awali hakuna raia ambaye alipigwa risasi kwa mbele hivyo inaonekana walikuwa wakikimbia hata kama wana makosa wameuawa kikatili,"alisema Mbowe.

Mbowe alisema kuwa hawaendi Tarime kuwatetea wahalifu bali wanakwenda kuwahakikishia haki inatendeka.

Dk Slaa amkaba Membe
Wakati huo huo Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Willibrod Slaa amemshangaa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernad Membe kwa kueleza kuwa Tanzania ni nchi inayojitegemea na yenye Rais, lakini walipoletewa barua kutoka SFO kuhusu Andrew Chenge, hawakuchukua hatua.

Dk Slaa alisema ni bora hizo fedha ambazo Serikali ya Uingereza inataka kuzitoa kwenye NGO ziende huko kuliko kuzipeleka serikalini kwa kuwa Serikali iliyopo madarakani ni ya kifisadi.

"Ni bora hizo fedha ziende kwa NGO ambayo inaaminika na kuweza kuwasaidia wanyonge,"alisema Dk Slaa.
Alitumia wakati huo kumtaka Ridhiwani Kikwete kwenda mahakamani kwa siku zake alizotoa kwani hana cha kuweza kumsumbua kwa kuwa ni mtoto mdogo.

Alisema kuwa maisha ya wananchi yameendelea kuwa magumu hivyo ni bora Rais Kikwete akae chonjo kutokana na hali hiyo."Juzi nimejiwa na askari polisi wameniambia kuwa usione tunawapiga mabomu, maisha yetu ni magumu,"alisema Dk Slaa.

Mbunge wa Iringa Mjini, Peter Msigwa aliwaambia wananchi wa jimbo hilo kuwa CCM ni meli inayozama, hivyo wawahi mitumbwi Chadema ili waweze kuokoka."CCM njooni Chadema tuwaokoe kutoka katika meli inayozama na msihangaike kupanga viti katika meli inayozama,"alisema Msingwa.Msigwa ambaye ni Waziri Kivuli wa Maliasili na Utalii, alisema kuwa ata pambana katika bajeti yake ili kuhakikisha maliasili zinawanufaisha wananchi maskini na si viongozi wa CCM waliokalia ufisadi."Nimeagizwa na chama changu kuhakikisha bajeti ijayo tunabanana na Serikali ya CCM ili kuhakikisha wananchi wananufaika na rasilimali zao,"alisema Msigwa.

Mpendazoe adai Sitta alitaka kuipindua CCM
Kada wa Chadema, Fred Mpendazoe aliendelea kukishambulia CCM kwa kueleza kuwa kimepoteza dira kutokana na kukumbatia na kulinda watu wachache badala ya kupigania watu maskini na wanyonge.

"Ndani ya CCM kuna watu wamejivika ngozi ya kondoo, lakini ni mbwa mwitu wakali, wakina Sitta, Nape Nnauye na Dk Mwakyembe wamekuwa wakijifanya wanawapigania wananchi, lakini ni wanafiki,"alisema.

Alisema kuwa Sitta ndiye aliyetoa samani za ofisi ya CCJ na mpango mzima wa kuipindua CCM, lakini leo bado wapo humo na wanaendelea kuwakandamiza wananchi na kulinda wachache kwa maslahi yao binafsi.

Mpendazoe aliendelea kumkandamiza Sitta kwa kuwaeleza wananchi kuwa aliahidiwa uwaziri baada ya kutemwa uspika na ndiyo maana ameamua kuwasaliti wananchi kwa maslahi yake binafsi.

Hotuba za viongozi hao wa Chadema zilikuja baada ya maandamano makubwa yaliyofanyika jana na kuuteka Mji wa Iringa ambapo wananchi walikusanyika pembezoni mwa barabara wakishangilia huku wengine wakifuatana na viongozi wa ngazi ya juu ya chama hicho.

Maandamano hayo yalianzia Kihesa hadi Uwanja wa Shule ya Msingi Mlandage na ndiyo yaliyokuwa yakihitimisha operesheni ya Chadema katika mikoa sita kwa muda wa wiki mbili.Operesheni hiyo ya chama hicho iliyoambatana na maandamano katika mikoa hiyo iliweza kupita katika majimbo ya uchaguzi 37 na kuzifikia Kata 224 na vijiji 457 kwa kutumia timu nane ambazo zilikuwa zikiongozwa na viongozi wa ngazi ya juu wa chama hicho.
 
Kwa upande wake Naibu Katibu Mkuu wa CHADEMA, Zitto Kabwe, aliutumia mkutano huo kupinga kile alichokiita propaganda za CCM zinazolenga kumchonganisha na mwenyekiti wake, Freeman Mbowe. Akipinga propaganda hizo alisema si kweli kuwa yeye ana ugomvi na Mbowe kama inavyoenezwa na vyombo vya habari vyenye uhusiano wa karibu na CCM.

Alisisitiza kuwa CHADEMA ni moja na imara na kamwe hatakuwa tayari kugombanishwa na mwenyekiti wa chama chake kwani ndiye aliyemjenga kisiasa na kiuongozi tangu akiwa mwanafunzi wa chuo kikuu.
“Kataeni propaganda zenye lengo la kuigawa CHADEMA kwa kuwachonganisha viongozi. Zitto siwezi kumpinga Mbowe kama wanavyodai…Zitto nimekuwa Zitto kwa sababu ya Freeman Mbowe. Ndiye aliyenijenga tangu nikiwa chuoni. CHADEMA yetu ni moja na itaendelea kuwa imara…propaganda za kutugawa zimeshindwa, sasa tunachukua nchi,” alisema Zitto na kushangiliwa.

Tanzania Daima
 
Big up Zitto, sasa unaonekana kuanza kukomaa, kazana kujiimarisha kujumuika na wenzako hadi tuwanyong'onyeze zaidi hawa na magamba yao yenye kuficha sumu kali.
 
...now this is beautiful, and we hope you are the man of your words, .. lets go save Tanzanians..bravo kaka..:dance:
 
Back
Top Bottom