Chadema Iringa Mei 19, 2011: Picha na Matukio

Chadema Iringa Mei 19, 2011: Picha na Matukio

ktk maandamano ya chadema mkoan iringa nimeona kijana kabeba bango linalosome kwa maandishi km hayo hapo juu. Kifupi sajaelewa LOGIC YA BANGO HILO!
 
Nimeipenda hiyo.
Kanyaga twende tutafika
IMG_8013.JPG
 
MAANDAMANO ya kufunga mikutano ya kitaifa ya mikoa ya yanda za juu kusini ya chama cha Demokrasia na maendeleo (CHADEMA) yatikisa mji wa Iringa huku chama cha mapinduzi (CCM) kikikwama kuhujumu maandamano hayo pamoja na kujaribu kuwachanganya wananchi kwa kuwatoa madarasani wanafunzi shule ya sekondari ya wazazi Mwembetogwa ili kuushikiria kwa muda uwanja wa Mwembetogwa .

Mbali ya mbinu hizo pia baadhi ya vijana wanaosadikika kuwa walipandikizwa na CCM kuingia katika maandamano hayo ili kuvuruga waliishia kunusurika kichapo baada ya mmoja kuangusha kofia na skafu ya CCM iliyochanwa na kuchomwa moto majira ya saa 5 asubuhi kabla ya kuanza maandamano hayo eneo la Kihesa .

Uchunguzi uliofanywa na mtandao huu wa Francis Godwin ni mzee wa matukio daima umebaini kuwepo kwa njama za hali ya juu kwa CCM kutaka kuvuruga maandamano hayo ambapo njama ya wazi ni ile ya kuuzuia uwanja wa Mwembetogwa ili Chadema isitumie kwa mkutano huo na badala yake kuwatoa wanafunzi madarasani na kuutumia uwanja huo huku baadhi ya wazazi wakilalamikia hatua hiyo ya uongozi wa shule hiyo kukubali kutumiwa kisiasa na CCM.

Mtandao huu wa Francis Godwin ni mzee wa matukio daima ulimshuhudia mkuu shule hiyo Ahmed Mbata akiwa na mwalimu mmoja katika uwanja huo wa Mwembetogwa akisimamia zoezi la wanafunzi hao kufanya tamasha ambalo linadaiwa kuanza kuandaliwa ndani ya wiki moja baada ya kutokana na agizo la CCM mkoa kama njia ya kuhujumu maandamano hayo ya Chadema Taifa.


Hata hivyo baadhi ya wananchi ambao walizoea uwanja huo wa Mwembetogwa kama uwanja mkuu wa mikutano ya Chadema walionyesha kubabaika na kujikuta wakisubiri kwa muda katika uwanja huo bila kuona rangi ya bendera za Chadema zaidi ya sare za wanafunzi hao hali iliyopelekea kutoka barabara kuu ya Iringa -Dodoma na kuungana na maandamano hayo huku baadhi yao walilazimika kuwauliza viongozi wa Chadema kwa simu.


Hata hivyo katika tamasha hilo lililobatizwa kuwa ni tamasha la kusaka vipaji kwa wanafunzi baadhi ya wanafunzi walisema kuwa tamasha hilo limeandaliwa na CCM na sio uongozi wa shule hiyo kama inavyoelezwa na baadhi ya watu.

"….Jana vionngozi wa CCM walifika shuleni kwetu na kushinda katika ofisi ya mkuu wa shule kwa ajili ya kuandaa tamasha hili …japo tunashindwa kujua lengo la CCM kuandaa tamasha hili kwani kama lingekuwa ni tamasha la shule tuna ukumbi mkubwa wa shule na siku zote tumekuwa tukifanyia katika ukumbi huo ila leo tumeshangazwa kuambia tuje hapa uwanjani ambako hatujawahi kufanyia tamasha kama hili la ghafla ….wana sema ni bonanza la shule mbona katika ratiba za mabonanza yetu hakuna kitu kama hiki"

Mmoja kati ya walimu wa shule hiyo alimweleza mwandishi wa habari hizi kuwa suala hilo limezua mgawanyiko mkubwa katika shule hiyo baada ya mkuu wa shule kuingiza ratiba ambayo haikuwepo na ndio sababu ya walimu wote kutofika katika uwanja huo kuungana na mkuu wa shule ambaye ni kada wa CCM.

Jitihada za kumpata mkuu wa shule hiyo ili kuweza kuelezea malengo ya tamasha hilo hazikuweza kuzaa matunda .

Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Iringa mjini Abed Kiponza alipotafutwa kwa njia ya simu na mtandao huu wa Francis Godwin ni mzee wa matukio daima ili kujibia madai ya wanafunzi hao kuwa viongozi hao wa CCM walifika shuleni hapo ili kupanga mbinu hiyo ya kuhujumu mkutano wa Chadema ,alikanusha madai hayo na kuwa kwa sasa yeye yupo chuo kikuu huria cha Tanzania akijisomea kwa zaidi ya wiki sasa na hajapata kupata muda za kuacha darasa hata siku moja.

"mimi ni mwisilam na sijazoea kusema uongo mimi nasoma huku Openi Universt hata sasa nikija hapo ulipo nitakuwa na vifaa vyangu vya shule"

Mbunge wa jimbo la Iringa mjini Mchungaji Peter Msigwa na mbunge wa viti maalum mkoa wa Iringa Chiku Abwao walisema kuwa CCM ilipanga kuvuruga maandamano hayo ila imeshindwa na nguvu ya umma baada ya wananchi kukubali kutembea umbali wa zaidi ya kilometa zaidi ya 5 kutoka Kihesa hadi Mlandege .
 
Tunashukuru kwa Picha Edson tujuze na ujumbe uliotolewa hapo.
Naöna Watu wa Tosa wanakumbuka mbali.Watu wa Nsumba mpo!!Brother Felix,Mondlane nk em tukumbuke kidogo pia way Back.
 
Kweli kabisa ccm wawachunguze mapema hao waliotuhumiwa kuasisi ccj then wawatimulie mbali wasije vuruga chama...lol
 
Babu anatoa dawa ya magonjwa sugu i.e kisukari, bp

CDM ni dawa ya matatizo sugu i.e ufisadi, kutowajibika
 
Jamani mbona kuna mada ambazo siruhusiwi kuchangia? Kuna nini haswa hadi imefikia hivyo!
 
Mwache Nape Nnauye asumbuke na CCM iliyomshinda hata marehemu baba yake kulinyosha; sisi wengine tulishamuonya juu ya hilo na wala hakulizingatia.

Nguvu ya Umma kwa snaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa kote nchini!!!!!!!!!!!!1

kwa mujibu wa nape ni lazima wafuatao wapewe majina yafuatayo ili cdm ikae vizuri:dr w. Silayo
-Mabere Marandu
-Prof.A. Sawaya
-Zitto Kavishe
-FRendriki Mnganya
-Tindu Laswai
 
BOB

Hujaeleweka!
Nimejaribu ku post ktk mada ya Mohammed Shossi ktk swala la Mwanakijiji, ikaja message kunambia siruhusiwi kupost kitu hapo hali mada nyinginezo nimeweza kuingia na kuandika kama nilivyoweza hapa..
 
ni hivi, kuna thread humu Jf isemaa "CHADEMA KTK PICHA MKOANI IRINGA" sasa humo kuna kijana kabeba bango lisomekalo CDM km kikombe cha babu, sasa logic ya hilo bango hata mimi sijaielewa, bt bango lipo!
 
mkuu umenikumbusha mbali sana nilikuwa nalala azimio, mambo ya quarter mile maandazi kwa masista

duh. kweli nami umenigusa nilikuwa naishi azimio floor ya kwanza chumba chenye kibaraza juu kinaface utawala moja kwa moja. mie nimekaa tosa miaka saba one to six.unakumbuka tosa girls ni shule ipi wewe?
 
duh. kweli nami umenigusa nilikuwa naishi azimio floor ya kwanza chumba chenye kibaraza juu kinaface utawala moja kwa moja. mie nimekaa tosa miaka saba one to six.unakumbuka tosa girls ni shule ipi wewe?


iringa girls aka zooooo
 
Nimejaribu ku post ktk mada ya Mohammed Shossi ktk swala la Mwanakijiji, ikaja message kunambia siruhusiwi kupost kitu hapo hali mada nyinginezo nimeweza kuingia na kuandika kama nilivyoweza hapa..

MOD wamehemaishia hiyo thread! Nadhani wakati ukiwa unapost kazi hiyo ilikuwa hewani. Iliishanikumba pia, pole
 
Wa magamba walipita huko, sasa wanaume acha wanarudishie magamba! Peopleeeees Power!!!
 
Back
Top Bottom