Chadema Iringa Mei 19, 2011: Picha na Matukio

Chadema Iringa Mei 19, 2011: Picha na Matukio

Nadhani kijana anapevuka kisiasa hivi sasa, alicho ongea zitto alitakiwa kukisema more often to strengthen the party, Namuunga mkono zitto kuwa mbowe ana weakness zake lakini amejitahidi kukibeba chama from one level to another level, better level

Lazima, tumpongeze mbowe kwa mchango wake mkubwa sana kuhakikisha chadema inafika mahali ilipo hivi sasa, Chadema au chama chochote cha upinzani kinachotaka kuchukuwa dola toka mikononi mwa ccm kinahitaji mtu jasiri, mwenye misimamo,mpambanaji, hodari, mikakati na mbinu za kijasusi kuweza kupambana na mbinu chafu za chama cha mapinduzi.

Mbowe is tough na hiyo imeisadia sana chadema kuweza ku survive umafia wa ccm na ukichangia busara za Dr. Slaa, zimelinda umoja wa chama. Chadema simameni pamoja na shikamaneni haswa kwani 2015, tunawakabidhi dola, watanzania tunawaamini na tunajiamini kuwa pamoja tunaweza.
 
hongera kabwe, watu walianza kukosa imani nawe, na magamba yalikuwa yakitumia ukimya wako kueneza sumu kwamba hamuivi na mwenyekiti wako.
 
Katika Operesheni sangara(CCM amshaamsha) pale Iringa Mjini, Mlandege ndo home....

Naibu Katibu Mkuu wa CHADEMA, Zitto Kabwe, aliutumia mkutano huo kupinga kile alichokiita propaganda za CCM zinazolenga kumchonganisha na mwenyekiti wake, Freeman Mbowe.

Akipinga propaganda hizo alisema si kweli kuwa yeye ana ugomvi na Mbowe kama inavyoenezwa na vyombo vya habari vyenye uhusiano wa karibu na CCM.

Alisisitiza kuwa CHADEMA ni moja na imara na kamwe hatakuwa tayari kugombanishwa na mwenyekiti wa chama chake kwani ndiye aliyemjenga kisiasa na kiuongozi tangu akiwa mwanafunzi wa chuo kikuu.

"Kataeni propaganda zenye lengo la kuigawa CHADEMA kwa kuwachonganisha viongozi. Zitto siwezi kumpinga Mbowe kama wanavyodai…Zitto nimekuwa Zitto kwa sababu ya Freeman Mbowe. Ndiye aliyenijenga tangu nikiwa chuoni. CHADEMA yetu ni moja na itaendelea kuwa imara…propaganda za kutugawa zimeshindwa, sasa tunachukua nchi," alisema Zitto na kushangiliwa.


source: Mi mwenyewe kwa macho na masikio yangu lakini maneno toka kitu cha daima
 
Nami naungana na wote juu kukupongeza Zitto! Naanza kuona ukomavu wako kisiasa. Uongozi ni zaidi ya kuwa mwenyekiti na sio ultimate goal ya mwanasiasa mzuri! Nafikiri ingechukulia maana halisi ya uongozi watu wasingegombana; lkn uongozi huusishwa na power zaidi, napenda tasfiri aliyoitoa Yesu kwa wanafunzi wake!

Kila mtu ni kiongozi; shida ni anaongoza kuelekea wapi? Au ni mtawala? Kwa nchi zetu watawala wanapaswa kuwa wananchi!

Najua mdogo wangu, uliathiriwa na shauri nyingi tofauti! Nafurahi umeibuka mshindi kwa kupembua na kuamua kilicho bora!

You have my n many of us' support! Keep it up! Amuoneaye WIVU mwenzake hampi ushauri wa kumjenga!
 
CDM mwendo mdundo mpaka kieleweke,waseme wasiseme wembe wetu uleule ni kukata kote kote!big up cdm
 
Kwa upande wake Naibu Katibu Mkuu wa CHADEMA, Zitto Kabwe, aliutumia mkutano huo kupinga kile alichokiita propaganda za CCM zinazolenga kumchonganisha na mwenyekiti wake, Freeman Mbowe.
Akipinga propaganda hizo alisema si kweli kuwa yeye ana ugomvi na Mbowe kama inavyoenezwa na vyombo vya habari vyenye uhusiano wa karibu na CCM.
Alisisitiza kuwa CHADEMA ni moja na imara na kamwe hatakuwa tayari kugombanishwa na mwenyekiti wa chama chake kwani ndiye aliyemjenga kisiasa na kiuongozi tangu akiwa mwanafunzi wa chuo kikuu. “Kataeni propaganda zenye lengo la kuigawa CHADEMA kwa kuwachonganisha viongozi. Zitto siwezi kumpinga Mbowe kama wanavyodai…Zitto nimekuwa Zitto kwa sababu ya Freeman Mbowe. Ndiye aliyenijenga tangu nikiwa chuoni. CHADEMA yetu ni moja na itaendelea kuwa imara…propaganda za kutugawa zimeshindwa, sasa tunachukua nchi,” alisema Zitto na kushangiliwa.

Source:Tanzania daima
 
Naona Zitto anaanza kurudi taratibu!! Naona ameona CCM hakufai tena.
Karibu tena kundini Zitto!!
 
THE END. Cinema imefika mwisho,watafute mkanda mwingine tuangalie
 
Nashukuru Zitto ameondoa wingu hilo, maana watu tulikuwa tunashindwa kujua ukweli. Zitto fanya kazi kijana, onyesha uwezo...nchi hii inahitaji watu kama wewe kupiga hatua. Acha magazeti ya chama cha magamba yaendelee na magamba type news.
 
Zito huo ndo ushujaa, na hilo ndo tulikuwa tunasubiri kusikia kutoka kwako sisi vija. CHADMA MOJA VYEMA, Pamoja tuikomboe nchi.
 
Chadema mkiwa kitu kimoja hakika mtaimaliza ccm bila shaka yoyote. Zitto you have very good future with chadema and not otherwise. Uwezo wako utaonekana tu kama utafanya kazi kwa moyo mweupe ndani ya chama.

Achana/na mambo ya kukaa katikati ya upinzani na chama tawala yanachelewesha mabadiliko tunayoyataka. chadema kazeni uzi si muda mrefu ccm itakatakatika, hawana ujanja wameshafuria hao.
Mungu ibariki chadema, Munggu wape umoja wa kweli uliojengwa ndani ya mioyo yao amen.
 
Zitto mwanampotevu ALIYEREJEA NYUMBANI, Siasa zako twazikubali sana mkubwa, we kamanda wa ukweli!
 
Bravo zitto kama haya maneno yametoka mdomoni mwako

jenga Chama, endeleza harakati zako zile za zamani tutakuunga mkono
 
I can see Zitto as potential CDM presidentil candidate for 2020 if he mantains the momentum brought him where he is today
 
Now we can conclude by saying, there ar no classes within a classles Chadema
 
Big up Zitto, Uliwaweka watu njia panda kwa msimamo legelege wakiuiga tu. Nasema wa kuiga kwa sababu hukuwa nao huko nyuma. Chapa kazi na hongera sana.
 
Nadhani kama kweli Chadema ni wabaya kwanini wanakuwa na umati mkubwa hivi?
Kama umati ni wa kutaka kumwona Slaa au Zitto tu, basi sawa lakini hata hivyo kwa mwanasiasa yeyote umati kama huu lazima umshtue na afikirie mara mbili kama si zaidi. Kwanza hawa Chadema wanapeleka ujumbe upi kwa jamii na jamii inaupokeaje ujumbe huo?
 
Back
Top Bottom