Yapo mengi sana ambayo tunaweza kujadili kwenye hoja zako hapa. Lakini kwa uhaba wa muda niseme tu methodology ya kuanzisha chama kimoja cha upinzani haiwezekani. Kati ya vyama vilivyopo sasa hivi vipo vingine viongozi wao wapo kwenye payroll ya CCM. Hivi utamshawishije Dovutwa aungane na upinzani?!!!
Mkuu shukran sana kwa kuuweka ukweli huu hapa jambo ambalo ndilo kiini cha kusema UKAWA ni kiini macho kwa sababu kama hizi. Kifupi umeongezea hoja ya maana sana ambayo sikutaka kuisema. Sasa iweje leo Chadema kweli iwe pamoja na kundi la viongozi ambao inajua wapo kwenye payroll la CCM ilihali hii ndio vita yake kubwa? Kama Zitto na ACT ni CCM iweje wajiunge na watu ambao wameisha dhihirisha kuwa wapo ktk payroll ya CCM tumeona majibu na ujumbe wa JK kuhusu maridhiano juu ya Katiba Mpya.
Imani yangu mwenyewe inanituma ya kwamba kama Chadema ile ya mwaka 2010 isingevurugwa japo wapo watu wanaokisiwa kuwa wasaliti lakini wakaendelea kufanya kazi kuelekea 2015, ninashawishika ama kwa uhakika, Chadema ingechukua bunge peke yake pasipo CUF wala NCCR maana hawa waliisha jimaliza zamani. Nguvu walokuwa nayo katika katiba haihusiani kabisa na uchaguzi wa wananchi.
Na sina lengo la kuubomoa umoja huu wa UKAWA lakini inanipa shida kuelewa malengo yao haswa maana siuoni ushindi hapa ikiwa baadhi ya viongozi wapo ktk Payroll ya CCM ina maana watakuwa radhi kuachia majimbo fulani ili CCM ishinde na wa dominate bunge na kutawala.
Ndio maana nikasema kama kweli nwalikuwa na nia ya dhati wangeunganisha nguvu zao wakaunda UPINZANI wa kweli ambao wangetumikia Katiba na kanuni za UMOJA huo lakini nje hapo kila chama kitatazama interest zake mbele na itakuwa vigumu sana kumshinda CCM.
Mimi sijali watu wanavyonifikiria maana nimeshasema sana vya kutosha, lakini wakumbuke tu hawashindani na Mkandara hapa bali hali halisi iliyopo ktk chaguzi zetu.
Pasco kazungumzia Sheria kuwa kipingamizi mimi sidhani kama sheria zina tatizo kama zitatekelezwa ipaswavyo na uwajibikaji wa vitengo vya NEC, TISS, MAHAKAMA na Polisi maana utaipima sheria katika utekelezaji wake. NEC wanadai kuweka uwanja sawa kwa vyama vyote lakini inapokuja uchaguzi kuna watu huzuiwa na Polisi kupiga kura kwa sababu wamevaa nguo ama kofia za Chadema au CUF kule Zanzibar. Sheria haisemi wakatazwe isipokuwa utekelezaji wa sheria ndio huvunjwa. Masanduku ya kura huzuiwa, huporwa na mengine kura kuharibiwa na vyombo hivi hivi vya serikali kwa kutumia vijana wahuni tu.
Sasa basi isije kuwa UMOJA huu wa kiini macho ukazivunja sheria Kabla kwa kutangaza nguvu ya Mande kuhakikisha CCM hachukui ushindi wakati sheria inasema NEC lazima wahakikishe uwanja uko sawa kwa wote kushiriki. Kwa nini muwape sababu ya kupewa ushindi wa bure kabisa wakati mlijua kwamba sheria zilizopo haziruhusu Mande?. Je, kweli wale waliopo katika payroll ya CCM watashiriki kwa moyo safi ama ndio wanawaweka Chadema kati ili wawamalize kabisa miaka ijayo Chadema isiwe mpinzani kwao...Je, hadi itokee ndio mtaanza kuitana WASALITI maana ilikuwa hivyo uchaguzi wa mwaka 2010.