CHADEMA inatumia koti la UKAWA kujikongoja kisiasa

CHADEMA inatumia koti la UKAWA kujikongoja kisiasa

Ni ukweli uliowazi na usiopingika kuwa CHADEMA imeyumba kisiasa na imepoteza mvuto kwa wananchi katika kipindi cha miezi sita sasa. Mambo makubwa yaliyochangia kuchuja huko kwa chama hiki kwa uchache ni ifuatavyo.

1.Matukio ya kihalifu na umwagaji damu, mfano kumwagia watu tindikali kama ilivyokuwa kwa mussa tesha huko igunga ambapo akina henry kileo walitamkwa moja kwa moja.

2.Siasa za vurugu, vitisho, matusi na lugha za kuudhi. Hili lmeiathiri sana CHADEMA kwa sababu mtanzania kwa asili yake hapendi na hajazoea vurugu,anapenda amani na ushirikiano,sasa hawa jamaa ni washari washari mno. Watu wamengastukaa..

3.Kufanya vibaya "bad calculations and timing" kwenye mchakato wa katiba mpya. Katika hili ni kwamba, wangesusia baadhi ya vipengele au sura za katiba watz wangewaelewa sana kuwaunga mkono lakini hii ya kupinga katiba yote ndio limewapiga vibaya.

Walivyota bungeni baadae watz wa kada mbalimbali na makundi tofauti tofauti ktk jamii kuwashauri warudi bungeni wao wakagoma na kung'ang'ana halijawafurahisha watz. Wameonekana kuwa ni wabishi na hawashauriki. Madikteta in the making.

4. Kuungana kama kitu kimoja wakati kiuhalisia sio hivyo....kwamba mwanachama wa cuf si wa chadema wala wa NCCR Mageuzi si wa CUF and vise versa...sababu iliyomfanya kafulila ahamie nccr kutoka chadema baada ya kuitwa sisimizi haijawa solved...sasa leo hii wanaambiwa wakae meza moja..itatoka moyoni? Itafanya kazi?

5.madonda ya chadema kuwaita cuf mashoga, kuwaita nccr vibaraka wa ccm tena hadharani hayajaisha kwa wanachama wa kawaida. Pengine yamefubaa kwa viongozi.

so koti la ukawa litapwaya si mda, its time...tusubiri plan B

Nafikiri upo ndotoni ukiamka utakuwa sawa. Cmd ni mpango wa Mungu so Haiwezi kufa kamwe labda ww utangulie kufa kwanza. Mlisema Cmd inakufa kabla ya 2014 lakini tumeonyesha uhai uchaguzi serekali za mitaa pamoja na hujuma zote dhidi ya CDM. Cmd inakaribia kukomboa nchi yetu Tz. Mungu endelea kuibariki Cmd daima
 
Msema kweli kipenzi cha Mungu na kama Mjamaa halisi "Nitasema kweli daima, Uongo kwangu mwiko!.."

UMOJA wa Katiba ya WANANCHI kama wanavyojiita UKAWA ni kiini macho kwa Watanzania wapenda mageuzi kwa sababu nyingi za msingi na nitazitaja hapa maana kuna tuhuma nyingi sana zimeanzishwa dhidi ya ACT kuwepo kwake wakasahau kabisa kwamba adui yao mkubwa ni Mfumo wao wenyewe. Leo hii nchi yetu ina vyama 22 vya Upinzani na kati ya hivyo ni vinne tu ndivyo vimeunda Umoja kwa lengo lao lakini kwa mashambulizi ya kuviziana.

Nimesema hapo nyuma ya kwamba kizingiti kikubwa cha UKAWA ni NEC, TISS. MAHAKAMA na Vyombo Usalama kama vile Polisi na Jeshi letu maana hawa ndio husimamia sana zoezi zima la upigaji kura na kutoa ulinzi unaohitajika.Vyonmbo hivi sio HURU bado vipo chini ya serikali tawala wakitumikia Katiba ya mwaka 1977. Kwa hali yoyote ile vyombo hivi vitaendelea kuitumikia katiba hiyo kwa nidhamu na misingi ilovianzisha vyombo hivyo chini ya ofisi ya rais. Hawa wote ni wateuliwa wa rais na wataendelea kuifanya kazi wakitegemea kuteuliwa tena na rais katika madaraka yao muhula ujao.


Kwa hiyo hata kama ACT isingekuwepo leo hii, CCM wangeweza kuchukua asilimia 2 au 3 ya kura ya chama chochote cha UKAWA kilichoshinda jimbo iwe Chadema, CUF au NCCR na kuziharibu na bado wakalindwa na vyombo hivi vya serikali. Tunapoingia kupiga kura mwenyekiti wa chama ambaye ndiye rais huwa bado yupo madarakani, hivyo hapotezi mamlaka yake wala hakuna chombo kinachokuwa juu yake hivyo anaweza bado kutumia nguvu yake kuhakikisha ushindi wa chama chake.

Jambo la Pili, Tukubali tusikubali ni wanaharakati pekee ambao wataweza kuipa kura yao mgombea wa UKAWA iwe Chadema, CUF au NCCR pale aliposimamishwa na hawa ni wachache sana nchini ukilinganisha na hesabu kubwa ya Waumini, Manazi na Washabiki wa siasa. Ni vigumu sana mnazi wa Chadema kuipa kura yake mgombea wa CUF katika jimbo lake. Vile vile wa CUF kuipa Chadema maana ukimwambia baina ya CCM na Chadema mzee wa CUF asiyekuwa mwanaharakati atakwambia bora ya CCM. Hata huko vijijini mtu aloipenda Chadema leo ukamsimamishe mtu wa CUF au NCCR, kura yake usiwekee dhamana ya hesabu kabisa.

Kifupi ni kwamba wananchi wengi wataingia Uchaguzi ujao kwa kuendelea kutazama vyama vyao na sio UKAWA kaa Umoja wao kwa sababu akisimamishwa mgombea wa NCCR eneo langu, hata kama mgombea anakubalika tukumbuke kwamba wapiga kura waliokataa NCCR uchaguzi wa 2010 hawataichagua NCCR kwa sababu zile zile hivyo kura zao badala ya kwenda Chadema au CUF waloichagua mwaka 2010,itakwenda katika vyama vingine 18 vilivyobakia, iwepo ACT isiwepo wigo ni pana kwa mtu kuchagua chama kingine na sio NCCR. Hivyo hivyo katika majimbo ya Chadema au CUF bado zipo kura zilizokwenda vyama vingine hazitahesabika kama za UKAWA maana hakipendi chama kilichopo.

Kuna jambo jingine ambalo UKAWA hawakulitazama kwa makini. watu wengi wanaounga mkono UKAWA ni wanaharakati na hawa sii wengi sana ukilinganisha na waumini wa chama, Manazi na washabiki wa vyama. Wanaharakati wapo radhi kufuata maelekezo ya viongozi wa UKAWA lakini sio wananchi wapiga kura wengi wenye unazi, ushabiki na waumini wa chama. Huwezi kumweka mgombea wa Chadema, Ukategemea kweli muumini, mnazi au mshabiki wa CUF kuipa kura yake hata kama Chadema inakubalika mahala hapo.

Huyu ataipa kura bora CCM kwake hata kama mwaka jana aliipa CUF na wakashindwa uchaguzi na Chadema. Hawa ni kama washabiki wa Mpira Ukategemea kwamba Mshabiki wa Arsenal anayeichukia Manu kesho ataishabikia wakicheza na Bacelona kwa sababu wanatoka wote Uingereza. Hakuna kitu hicho ila wenye mapenzi na nchi yao pekee ambao ni wachache sana wanaoweza kushabikia timu yao ila kama timu itakuwa ya Taifa hapo waingereza huungana na kuwa kitu kimoja hata kama timu hiyo ina wachezaji wengi wa ManU.

Hivyo basi, kama wananchi wapiga kura watakuta jina la mgombea limesimamia ktk tiketi ya UKAWA, wasingeweza zipeleka kura zao kwingineko au CCM hata kidogo na hivyo ile nguvu ya jumla ya wanaharakati, waumini, manazi na washabiki wa kisiasa ingekuwa kubwa kwa UKAWA badala ya mwendo wanaotaka kuchukua UKAWA wa kugawana majimbo. Hili nawambieni hamtashinda na haiwezekani mgombea Urais atoke Chadema wakati Zanzibar hawana mgombea anayekubalika.

Mtaweza vipi kumsimamisha Slaa wakati Chadema haikubaliki zanzibar? nani atakuwa mgombea mwenza ambaye kweli anaweza kuwavuta wapenzi wa CUF wamchague Slaa na mgombea mwenza. Wenye nafasi pekee ya bara na Zanzibar ni CUF na nawahakikishia ya kwamba CCM itapata ushindi kirahisi sana maana hasa bara maana CCM hawaogopi kutumia karata ya Udini, Ukabila mahala popote wanapotaka.

Hivyo nasema UKAWA ni kiini macho tu tunapigwa changa la macho maana pasipo kuungana haiwezekani wao kumshinda CCM ikiwa wana choice ya vyama 19 vya kupandikiza kura. Hata wakiungana 10 bado CCM wataitumia nguvu walopewa na katiba ya mwaka 1977 kujipangia ushindi. Kama kweli UKAWA wanataka kuishinda CCM wangeunganisha nguvu ikiwezekana wote ama vikabakia vyama vichache kufikia Vinne au vitano tu katika uchaguzi wa 2015.

Hapo nina hakika CCM asingetoka pamoja na katiba ya mwaka 1977 au vyombo vyombo vitakavyo wakwaza kuwepo maana vile vyama vitakavyo achwa nje ni rahisi kuhesabiwa kuliko vyama 18 vya Upinzani vilivyoundwa kwa malengo binafsi. Naelewa sana akili za Kiafrika kuunganisha nguvu ni jambo la mwisho kufanyika na hivyo nalazimika kusema ukweli kwamba hawawezi kuungana na hivyo wamekuja na kiini macho hiki..
 
haya ni maoni yako ila njlitarajia kwa taluuma yako ungefanya angalau kautafiti kadogo uje na takwimu za kutushawishi kuliko kuja na thread ndeefu bila data yoyote
 
Tunapoingia kupiga kura mwenyekiti wa chama ambaye ndiye rais huwa bado yupo madarakani, hivyo hapotezi mamlaka

yake wala hakuna chombo kinachokuwa juu yake hivyo anaweza bado kutumia nguvu yake kuhakikisha ushindi wa chama

chake.

Point.
 
Ni hadithi nzuri ila tatizo ni ya kufikirika sana kuliko uhalisia
Ebu nipe Uhalisia mkuu wangu. Unataka kunambia mimi kama mfuasi wa TLP na Mrema naweza kweli kuwapa UKAWA kura yangu badala ya TLP? Mimi mfuasi wa Mtikila naweza kweli ungana na UKAWA kwa sababu gani?. lakini kama hawa wangekuwa chama kimoja kuna uwezekano mkubwa. Uhalisia ndio huu acheni ACT pembeni fikirieni picha kubwa
 
Kuna mtihani mwingine muhimu sana utaikabili UKAWA na watapaswa wauvuke.Mahakama ya Kadhi, upande wa CUF na wafuasi wao hili ni jambo muhimu sana lakini upande wa Chadema hili jambo ni nuksi, kuna mtihani mkubwa sana hapo kuziridhisha pande zote.Kila mtu anaweza akawa aliona kuwa bunge lililopita ilipofika hoja ya kadhi hakukuwa na UKAWA, ilikufa kwa muda.Sasa kwenye uchaguzi mkuu wafuasi wa CUF watataka wathibitishiwe hilo kuwa wakitoa kura inawekwa kwenye katiba??na ukiahidi hivyo utawaelezeje wa upande wa pili?

Kimsingi CUF na Chadema hazipo compatible, kama wakienda pamoja kwenye uchaguzi chama kimojawapo baada ya uchaguzi kitarudi mtaani na kukuta washabiki wake hawapo tena, wamehamia vyama vingine.

Kikwete aliongea kuhusu suala la udini kwenye uchaguzi uliopita.Nakubaliana 100% na Kikwete udini ulikuwepo sana kwenye uchaguzi ule, uzalendo sio kujifanya kipofu, ni kuyatambua matatizo tulio nayo, kuyakubali na kuyafanyia kazi.Nasikitika tu kuwa pamoja na Kikwete kuyatambua mapema baada ya uchaguzi ule hajafanya lolote kurekebisha hali hiyo na kufuta isijirudie tena hali ile.Anaondoka madarakani akiliacha taifa palepale.Hapa amefeli vibaya.

Kuna mtazamo usio rasmi kuwa wakati wa wa Rais Mkristo, ni chama kilichokuwa kinaungwa mkono na wapinzani-waislam wengi kilichokuwa na nguvu lakini baada tu ya Rais Muislam kuingia madarakani waislam wapinzania naturally wakapungua nguvu wakati upande wa kikristo wakawa motivated.Hizi element zipo kwenye jamii japo tunaweza tusipende ata kuziongelea.

Nawatambua watu kadhaa ambao ni wapinzani wa jadi wa CCM lakini ilibidi wampigie kura Mkapa badala ya Prof Lipumba mwaka 2000, na kuna wengine ambao katu hawataweza kumpigia kura Dr Slaa kwa misingi hiyohiyo.Tuna tatizo hili kwenye taifa.Tusilifumbie macho kama hatulioni, tulifanyie kazi.
 
Mjadala ni hoja kujibiwa kwa hoja, hizi habari za kusemasema hovyo, inaonyesha wazi mada imewaingia maana hamna majibu. Mimi nachoandika ni Uhalisia, na explore reality ambayo inatokana na mazingira tuliyopo. Leo kuna Udini nchini kweli mnategemea mwana CUF ampe kura yake Slaa baada ya miaka 4 ya majibizano ya kidini?..Ama mnajidanganya hakuna Udini? hakuna Ukabila hakuna Uchama! isipokuwa ACT tu ndio maadui zenu.

Au MwaChadema kweli akubali Slaa asisimamishwe badala yake Lipumba wakati upande wa pili kuna Mwigula japo haipendi CCM.. Ni wanaharakati pekee wanaoweza fanya hivyo lakini hawa washabiki naowaona humu... Hai ingii akilini hata kidogo.
 
Jitihada za kubomoa UKAWA ni kubwa sana , namshangaa huyu jamaa ambaye ameishi Canada leo anakuja na hoja za udini na ukabila , bila aibu na anasema ana hoja anataka zijibiwe zipi za udini na ukabila ?
 
Sina muda wa kusoma hadithi hii,haielimishi wala kufundisha.
Nilipoona tu jina la Mkandara nikakimbilia kucomment,maana huyu kule Great Thinkers kwa akina NGURUVI 3,Mchambuzi,Selemani,Alinda nk ni kituko hana hoja,ni mtu wa kukwepa kwepa,kikisemwa hiki yeye anasema kingine. Hana jipya. Kaamua kukimbia huku. Pole kwa kutapatapa.
 
Kwanza kaanza Lizaboni na Hekaya zake,baada ya masaa mawili Mkandara naye kaja na hadidhi zake.

Napata shida kidogo kumwelewa Mkandara kwa sababu Mkandara wa kule jukwaa la GREAT THINKERS ni tofauti na huyu kwenye jukwaa hili la SIASA. Kumetokea nini mkubwa huku? Au kuna mtu ame - hack account yako aisee?

Nauliza kwa sbb, the way unavyojenga hoja huku na hususani katika bandiko hili ni tofauti kabisa na hoja zako kwenye jukwaa la kule sambamba na akina Mag3, Mchambuzi, Adharusi,NguruV na wengine kiasi ambacho mpaka wengine hatuna data za kutosha tunashindwa kusema chochote na badala yake tunakuwa wasomaji na kujifunza kutoka kwenu wakati tukiipima kila hoja ya mchangiaji!!

Ili kwa hili la leo mzee umechemka mno, hujaja kitafiti,ni kama umetokea usingizini na kutupia hii kitu!!

Nasema hivi kwa sbb haingii akilini kusema kuwa, kwako wewe muungano wa ukawa ungekuwa na maana na nguvu halisi za kuivurumisha CCM iwapo muungano wao ungehusisha na vile vyama vingine 19 vilivyo nje ya UKAWA. Unaendelea kusema kuwa, ilivyo sasa ni ngumu sana kwa wapenzi wa CUF kuipa kura CHADEMA palipo na mgombea wa CHADEMA au CHADEMA kuipa kura CUF palipo na mgombea wa CUF na badala yake hao wataipa CCM na kwa maana hiyo li CCM litaemdelea kushinda tu, UKAWA hawataweza kuisimamisha. Hitimisho lako ni kuwa bado kura zitatawanyika tu tofauti na malengo ya UKAWA kwa maana hata ACT nao watapata!!

Fine, what is the difference then? Kwamba hata vyama vyote 19 vilivyo nje ya UKAWA vikaamua kuingia ktk umoja huu, si bado dhana yako itakuwa ni ileile, au?
 
Na hili ndio tatizo.


Jambo la Pili, Tukubali tusikubali ni wanaharakati pekee ambao wataweza kuipa kura yao mgombea wa UKAWA iwe Chadema, CUF au NCCR pale aliposimamishwa na hawa ni wachache sana nchini ukilinganisha na hesabu kubwa ya Waumini, Manazi na Washabiki wa siasa. Ni vigumu sana mnazi wa Chadema kuipa kura yake mgombea wa CUF katika jimbo lake. Vile vile wa CUF kuipa Chadema maana ukimwambia baina ya CCM na Chadema mzee wa CUF asiyekuwa mwanaharakati atakwambia bora ya CCM. Hata huko vijijini mtu aloipenda Chadema leo ukamsimamishe mtu wa CUF au NCCR, kura yake usiwekee dhamana ya hesabu kabisa.
 
Jitihada za kubomoa UKAWA ni kubwa sana , namshangaa huyu jamaa ambaye ameishi Canada leo anakuja na hoja za udini na ukabila , bila aibu na anasema ana hoja anataka zijibiwe zipi za udini na ukabila ?
hovyo sana huyu jamaa na wakome hawawezi kuibomoa UKAWA zikija mada za kuiambia ukweli ACT jamaa wanaziondoa na kupiga watu ban lakini kama hizi wanaziacha kinachoendelea mkuu max watu watafikia wataichukia jf kama wanavyoichukia ccm kwani hakuna haki apa! unaweza kukuta nami napigwa ban
 
Kwanza kaanza Lizaboni na Hekaya zake,baada ya masaa mawili Mkandara naye kaja na hadidhi zake.

Napata shida kidogo kumwelewa Mkandara kwa sababu Mkandara wa kule jukwaa la GREAT THINKERS ni tofauti na huyu kwenye jukwaa hili la SIASA. Kumetokea nini mkubwa huku? Au kuna mtu ame - hack account yako aisee?

Nauliza kwa sbb, the way unavyojenga hoja huku na hususani katika bandiko hili ni tofauti kabisa na hoja zako kwenye jukwaa la kule sambamba na akina Mag3, Mchambuzi, Adharusi,NguruV na wengine kiasi ambacho mpaka wengine hatuna data za kutosha tunashindwa kusema chochote na badala yake tunakuwa wasomaji na kujifunza kutoka kwenu wakati tukiipima kila hoja ya mchangiaji!!

Ili kwa hili la leo mzee umechemka mno, hujaja kitafiti,ni kama umetokea usingizini na kutupia hii kitu!!

Nasema hivi kwa sbb haingii akilini kusema kuwa, kwako wewe muungano wa ukawa ungekuwa na maana na nguvu halisi za kuivurumisha CCM iwapo muungano wao ungehusisha na vile vyama vingine 19 vilivyo nje ya UKAWA. Unaendelea kusema kuwa, ilivyo sasa ni ngumu sana kwa wapenzi wa CUF kuipa kura CHADEMA palipo na mgombea wa CHADEMA au CHADEMA kuipa kura CUF palipo na mgombea wa CUF na badala yake hao wataipa CCM na kwa maana hiyo li CCM litaemdelea kushinda tu, UKAWA hawataweza kuisimamisha. Hitimisho lako ni kuwa bado kura zitatawanyika tu tofauti na malengo ya UKAWA kwa maana hata ACT nao watapata!!

Fine, what is the difference then? Kwamba hata vyama vyote 19 vilivyo nje ya UKAWA vikaamua kuingia ktk umoja huu, si bado dhana yako itakuwa ni ileile, au?
Mkuu wangu nakuomba sana nisome halafu toa maelezo yako dhidi ya kipengele chochote ambacho wewe unaona sii kweli, maana kwa mwenye kuelewa atajua kwamba nawapeni UKAWA chance ya kujirekebisha kabla ya hasara. Sina maana mbaya kabisa ikiwa haya yatazingatiwa na kuiokoa UKAWA inayojipa tegemeo wakati halipo. UMOJA WAO pasipo kuunganisha vyama ni uongo mtupu mkuu wangu utashinda vipi ilihali vikwazo vyote nimeviorodhesha.

Sasa nitakuwa vipi hasimu wa UKAWA ikiwa leo nawaonyesha makosa yao? nawapa njia za Ushindi badala ya kuuficha. Sii haya ndio ya CCM wanapopewa makosa yao huja juu na kupiga watu virungu.. Kumbe lengo na nia ya vyama vya Upinzani ni kuwarekebisha tu. ndicho nachokifanya hapa kwa moyo safi kabisa. Bila mimi kuandika haya UKAWA watayajua wapi? kama wanayajua na wamejipanga basi watuonyeshe watapita vipi vikwazo hivyo. In real life lazima ukubali kutazama na kukisia mwenzako anajiandaa vipi sio kudhani ushindi tuuu kama alivyofikiria Porto jana matokeo kapigwa goli 6.
 
Hao ndio wasomi wetu katika ubora wao, wengine mara sisi wachumi, leo usd inaenda 2000, mara ooh tuna raisi mchumi, hata zile nyimbo zake za ajira milioni tano hakumbuki kianzio cha huo wimbo...
 
Wakija akina Mchambuzi,Mag3,Nguruvi3 nk jukwaa hili utakimbia wewe muda sio mrefu.
 
Back
Top Bottom