Ebu nipe Uhalisia mkuu wangu. Unataka kunambia mimi kama mfuasi wa TLP na Mrema naweza kweli kuwapa UKAWA kura yangu badala ya TLP? Mimi mfuasi wa Mtikila naweza kweli ungana na UKAWA kwa sababu gani?. lakini kama hawa wangekuwa chama kimoja kuna uwezekano mkubwa. Uhalisia ndio huu acheni ACT pembeni fikirieni picha kubwa
Mkuu wangu nakuomba sana nisome halafu toa maelezo yako dhidi ya kipengele chochote ambacho wewe unaona sii kweli, maana kwa mwenye kuelewa atajua kwamba nawapeni UKAWA chance ya kujirekebisha kabla ya hasara. Sina maana mbaya kabisa ikiwa haya yatazingatiwa na kuiokoa UKAWA inayojipa tegemeo wakati halipo. UMOJA WAO pasipo kuunganisha vyama ni uongo mtupu mkuu wangu utashinda vipi ilihali vikwazo vyote nimeviorodhesha.
Sasa nitakuwa vipi hasimu wa UKAWA ikiwa leo nawaonyesha makosa yao? nawapa njia za Ushindi badala ya kuuficha. Sii haya ndio ya CCM wanapopewa makosa yao huja juu na kupiga watu virungu.. Kumbe lengo na nia ya vyama vya Upinzani ni kuwarekebisha tu. ndicho nachokifanya hapa kwa moyo safi kabisa. Bila mimi kuandika haya UKAWA watayajua wapi? kama wanayajua na wamejipanga basi watuonyeshe watapita vipi vikwazo hivyo. In real life lazima ukubali kutazama na kukisia mwenzako anajiandaa vipi sio kudhani ushindi tuuu kama alivyofikiria Porto jana matokeo kapigwa goli 6.
Ebu nipe Uhalisia mkuu wangu. Unataka kunambia mimi kama mfuasi wa TLP na Mrema naweza kweli kuwapa UKAWA kura yangu badala ya TLP? Mimi mfuasi wa Mtikila naweza kweli ungana na UKAWA kwa sababu gani?. lakini kama hawa wangekuwa chama kimoja kuna uwezekano mkubwa. Uhalisia ndio huu acheni ACT pembeni fikirieni picha kubwa
Sheria gani inayokataza vyama kuungana wakaita jina moja. Kinachosajiliwa ni UKAWA, ni muungano huu wa kupiga mande chama kimoja kwa kushirikiana kupanga matokeo ndio haukubaliwi. Subirini uchaguzi mtanambia ama kama kweli unayo hiyo sheria naomba utuwekee hapa.Unataka watu waache kujipanga na kampeni waanze kuunganisha vyama sasa sio , halafu hicho chama kipya kitasajiliwa na nani? unataka kusema kuwa huujui ukweli wa sheria zetu za vyama kuwa kuunganisha vyama hairuhusiwi? halafu bado unajiita mchambuzi na mshauri, nyie ndio aina ya wale mliompoteza kiongozi mkuu kwa kumshauri kuwa aanzishe chama ndani ya chama na mkitaka avumiliwe ..........mkaenda mbali na kumpa ushauri wa kuwa na mamlaka ya Kidikteta kwenye kasacos kake .........unajitia ujinga ,
Jitihada za kubomoa UKAWA ni kubwa sana , namshangaa huyu jamaa ambaye ameishi Canada leo anakuja na hoja za udini na ukabila , bila aibu na anasema ana hoja anataka zijibiwe zipi za udini na ukabila ?
Sheria gani inayokataza vyama kuungana wakaita jina moja. Kinachosajiliwa ni UKAWA, ni muungano huu wa kupiga mande chama kimoja kwa kushirikiana kupanga matokeo ndio haukubaliwi. Subirini uchaguzi mtanambia ama kama kweli unayo hiyo sheria naomba utuwekee hapa.
Majibu ya serikali za mitaa yalionyesha kuwa wananchi wameungana , au wewe unatumia utafiti gani kuwa hawajaungana?Mkuu acha ushabiki wa kijinga mkuu jamaa kwa mtu mwenye fikiria yakinifu ndo anaweza kuliona hili KWA uhalisia muunganio wa ukawa upo kwa viongozi pekee.huku chini kwa wananchi kila mtu yupo kwenye chama chake . Ni bora useme ni mgonjwa ukaenda hospital utapona kuliko kujifanya kuwa ww ni mzima kumbe wew ni mgonjwa
nakubali kabisa lakini walipoungana ilikuwa swala la Katiba Mpya sio Uchaguzi mkuu jambo ambalo hata mimi sikukubaliana nao juu ya serikali 3. Hiyo haina maana nakubaliana na CCM na kupingana na UKAWA..Ningeulizwa ningesema serikali 1 ndio bora zaidi.1. UKAWA iliundwa wakati wa bunge la katiba. Vyama vyote vilivyokuwa na usajili wa kudumu ambavyo havikuridhika na mwenendo wa bunge la katiba vilikuwa huru kujiunga UKAWA. Vinne tu vilikuwa tayari, na wasingeweza kulazimisha wengine
Sawa yalikuwa extended na watu wale wale waliochaguana kuongoza Upinzani wa katiba Mpya juu ya serikali 3 na sio vinginevyo2. Maudhui ya UKAWA yalikuwa extended hadi uchaguzi mkuu washirikiane. Sina uhakika kama kulikuwa na fursa ya kuvihusisha vyama vingine in time ambavyo viliridhika na nia ya upinzani kuungana kwenye uchaguzi (hata kama havikuona umuhimu wa kuungana kupinga katiba ya Chenge)
Huwezi chukua matokeo ya mwaka 2010 na kuyafanya kiashirio cha mwaka 2015 kwa maana hiyo UKAWA haikuwepo. Unapotaka kujenge mikakati ya Ushindi unatazama mapana yake na chama kimoja tu kinaweza kujenga hoja mwaka 2015 na kikakubalika kinyume cha mategemeo yenu.3. Kati ya vyama kama 20 vilivyokuwepo uchaguzi mkuu uliopita zaidi ya asilimia 99 ya kura halali ambazo zilipigwa kwa upinzani zilipigwa kwa vyama vitatu kati ya vinne vilivyopo kwenye UKAWA sasa. Hii ni kusema vyama vingine vilikuwa na bado vipo insignificant
Unaweza vipi kupima makuzi ya chama nje ya upigaji kura? kuwa na wanachama wengi haina maana chama kinakubalika NCCR enzi ya Mrema ilikuwa na wanachama wachache sana ukilinganisha na CCM lakini record waloiweka haiwajawahi vunjwa na chama chochote nchini. tatizo la vyama vyote nchini wanapotosha maana ya uanachama wakidhani ndio hesabu ya kura za ushindi. Sio kweli, kukua kwa chama hupimwa wakati wa uchaguzi tu kinakubalika na wananchi kushika dola au laa.4. Tangu uchaguzi mkuu uliopita hadi sasa hakuna hata kimoja kati ya nyama vya upinzani visivyopo kwenye UKAWA kilichoonesha kukua. Hii ina maana hata katika uchaguzi ujao vyama hivyo vitakuwa insignificant
Kitakuwa wala sio kinaweza hilo tulikubali lakini kwa muundo uliopo bado kura itakwenda Upinzani na sio CCM Kwa hiyo maan nzima ya Umoja haipoikiwa kila chama kitasimamisha mgombea wake. Vyama vyote bado vitakuwa vyama vya Upinzani na kila kura yao itakuwa dhidi ya CCM haijalishi nani kaichukua.5. Kwa sasa chama cha ACT (ambacho hakikuwepo uchaguzi mkuu uliopita) kinaonyesha huenda kikawa na significant effect kwenye uchaguzi mkuu ujao.
tatizo ni kwamba vyana hivi vinne ndivyo vyenye maamuzi nani aungane nao nani hawamtaki. Mimi ningeshauri vyama vyote vya Upinzani wapewe nafasi hiyo waunde chama kimoja na kijiandikishe mapema, iwe hakuna Chadema, CUF, NCCR wala nani isipokuwa kwenye kumbukumbu zao tu. wakisha iondoa CCM huko mbele watajuana wafanye nini..6. Kama ACT watakuwa kweli na nia ya kuiondoa CCM then watajiunga na UKAWA.
Ikiwa lengo ni kumwondoa CCM unataka kujua nini kutoka ACT wakati una CUF na NCCR ambao huwajui wamesimama vipi katika swala hili nje ya Katiba Mpya. hapa kinachowaunganisha ni ile nia ya dhati ya kuindoa CCM madarakani lakini hawana chochote in common zaidi ya kwamba wanaitaka Katiba Mpya ya Wananchi.7. Sio rahisi, na sio busara kuharakisha kwa vyama vipya kama ACT kujiunga na 100% ya maudhui ya UKAWA kwa sasa. Kwa mfano sio rahisi ACT ikafiti kwenye maudhui ya kuachiana majimbo ya ugombea kwa sababu kwanza UKAWA wameshafika mbali katika hilo, lakini pia ACT haina data kutoka uchaguzi uliopita hivyo ni vigumu kwa wao au UKAWA wengine kujua ACT waachiwe jimbo/majimbo gani.
Kama UKAWA itajiandikisha nakuwa chama Kimoja uwezekano huo utawavuta hao kuingia Umoja huu badala ya kuanzisha chama maana swala kubwa hapa ni kuiondoa CCM madarakani. Kama mtawarahisishia kazi ya kuunda chama kwa nini wasijiunge na chama kisichokuwa na wenyewe?8. Upo uwezekano kikaibuka chama kingine chenye nguvu (miongoni mwa vyama vilivyopo upinzani) kabla ya uchaguzi mkuu ujao hasa kutokana na mpasuko unaoweza kutokea katika vyama vikubwa kwenye maslahi ya uchaguzi ujao. Kwa mantiki hiyo hata kama UKAWA itaviingiza vyama vingi vya upinzani kwenye umoja, bado sio guarantee kuwa vitakavyobaki havitakuwa na umuhimu
Mimi nadhani kama ACT itaunganisha vyama vingine vilivyobakia hapo ndipo kweli tunaweza sema sasa ACT imekuja vunja UKAWA maan wamekifanya kile ambacho UKAWA walitakiwa kukifanya wakapuuza..9. Cha kufanya ni ACT na vyama vingine vya upinzani visivyo kwenye UKAWA kujipima, na kuyapima maudhui ya UKAWA na kuanza mazungumzo ya kuingia katika baadhi ya maudhui hayo. Namna nzuri ni ACT kukubaliana na UKAWA kumuunga mkono mgombea uraisi atakayeteuliwa na UKAWA, lakini wao wakaendelea na mipango yao kwenye ubunge na madiwani. CHADEMA walifanya hivyo mwaka 1995 walipomuunga mkono mgombea uraisi wa NCCR lakini kwenye ubunge na udiwani waliendelea kuchuana kama kawaida...
. Kutangaza mgombea sio hoja isipokuwa umoja wao na hatari kubwa ni kwamba Kenya wana makundi mawili tu ya Ukabila. Wakikuyu vs Wajaluo hivyo ni rahisi kuzimaliza tofauti zao. Sisi tuna mengi sana na kibaya zaidi unapomtangaza Slaa dakika za mwisho hutawapa nafasi watu wa CUF kupata majibu why Slaa na sio Lipumba au kinyume chake. nakuhakikishia UMoja huu ukifanyika CCM hana pa kutokea.. Hii ya kumpiga mande mcheza karate atawamaliza vibaya vibaya..10. Ukiacha kwenye maudhui ya kugawana majimbo na kata, chama chochote (ikiwamo ACT) kitakachofikia makubaliano kwa mfano ya kumuunga mgombea uraisi wa UKAWA, bado upo mda wa kufanya tathmini na majadiliano. By the way mda mzuri wa kufanya hivyo ni siku chache kabla kampeni hazijaanza, ili kutowapa adui (CCM) mda wa kuingilia hiyo mipango. Katika hili kumbuka ule mkutano wa ODM kasarani, siku chache kabla ya uchaguzi, Mh Raila alipotamka "Kibaki atosha"... na akatosha kweli.
Wala mimi sina tatizo na ACT hata kidogo isipokuwa mpango wa UKAWA haukukaa sawa kabisa ni kiini macho na nakuhakikishia Ushindi hauwezi patikana kwa njia hizi hata kidogo kwa Tanzania hii nayoijua mimi..So hakuna haja ya papara, ACT bado ni wachanga, wajenge chama chao, then ukikaribia uchaguzi wajitathmini, je watagombea wenyewe, au wataunga mkono mgombea mmoja wapo mwenye nguvu? (Hata kama ni wa CCM, ili mradi waridhike na makubaliano yatakayoingiwa na kutegemea maudhui yake makuu)...
Majibu ya serikali za mitaa yalionyesha kuwa wananchi wameungana , au wewe unatumia utafiti gani kuwa hawajaungana?
Serikali za mitaa daftari lake jingine kabisa na watu walopiga kura zaidi ni wanachama. nilikuwepo Bongo kadi zikigawiwa haraka haraka na ahadi za uongo ukawape kura tu wagombea wao. Hili daftari la Uchaguzi mkuu ni kubwa tunazungumzia zaidi ya watu millioni 15 wanaotegemewa mwaka huu, sasa utalinganisha na uchaguzi mdogo wa Halamashauri? kwanza watu wengi hawakushiriki kabisa.Majibu ya serikali za mitaa yalionyesha kuwa wananchi wameungana , au wewe unatumia utafiti gani kuwa hawajaungana?
Sawa unaweza walau kunithibitishia ni wap wanachama wa cuf wamewaonga mkono cdm au kinyume chake . Ushindi wa vyama hivi vitatu unatokana na ukweli kuwa CCM imechokwa kila mahali
Serikali za mitaa daftari lake jingine kabisa na watu walopiga kura zaidi ni wanachama. nilikuwepo Bongo kadi zikigawiwa haraka haraka na ahadi za uongo ukawape kura tu wagombea wao. Hili daftari la Uchaguzi mkuu ni kubwa tunazungumzia zaidi ya watu millioni 15 wanaotegemewa mwaka huu, sasa utalinganisha na uchaguzi mdogo wa Halamashauri? kwanza watu wengi hawakushiriki kabisa.
Wewe ni boya
Nitasema Ukweli Daima, Uongo kwangu mwiko - Katiba ya CCCM
Mkuu na wewe mjinga kweli unatofauti gani sasa na mleta mada kwa mawazo yako haya.Tena si boya dogo bali kubwa sana. Ndiyo kawaida ya watu wasiojitambua wakati anaona UKAWA ni kiini macho, kwake huyu boya MACCM ndiyo kila kitu pamoja na wizi, upokeaji rushwa, ufisadi, ujangili, kuuza unga n.k. hawa wahuni ndiyo wanastahili kuendelea kuwepo madarakani milele. Mchezo mchafu na uhuni uliofanywa na MACCM kuchakachua maoni ya katiba mpya kama yalivyokusanywa na Tume ya Warioba hayaoni huyu, na badala ya kuwalaumu MACCM anataka kuilaumu UKAWA! Sijui kwa faida ya nani hasa!
Mkuu na wewe mjinga kweli unatofauti gani sasa na mleta mada kwa mawazo yako haya.
Utakuwa umenisaidia sana kama utanionyesha kifungu cha Katiba kinachokataza vyama kuungana maana hata NCCR iliasisiwa kwa vyama kuungana. CCM yenyewe ni muungano wa vyama vitatu TANU, ASP na UMMA party.. Sasa hili lenu mnalolisema sijui limetoka wapi ila nitashukuru kama mtanipa kipengele hicho.Mkuu Mkandara, heshima mbele.
Nadhani kuna sehemu nakubaliana na wewe na kuna sehemu sikubaliani. Nadhani kwenye karatasi UKAWA ni fikira pevu, lakini kama wanavyosema wazungu "the devil is in details", hapa ndio focal zaidi. UKAWA ilianzishwa kiupepoupo tuu lakini ukweli wa mambo unabaki palepale, kwamba Katiba ya mwaka 1977 haikubaliani na mgombea binafsi wala haitambui muungano wa vyama. Hivyo ni lazima kwa mgombea mwenza wa uraisi ajiunge ama na Chadema, CUF au NCCR. Kitu ambacho naona kama nikiini macho.
Lakini tatizo kubwa lipo kwenye timing, nadhani UKAWA wali underestimate nuts and bolts ambazo zipo ndani ya muungano wao. Na kingine kuja kwa ACT kama wataendelea na pressure hii hii basi dodosa za igizo zitakuwa zimebadilika. Ieleweke yakwamba wanaotaka kugombea maeneo ya ubunge walikuwa kwenye mission kwa zaidi ya miaka 2, wengine wanamashiko katika maeneo hayo lakini kutokana na Ugawanaji wa majimbo wengine itabidi wakatwe. Mfano, labda ubungo kuna mgombea wa CUF ambae anaimani sana kwamba angeweza kuiba Ubungo kwenye uchaguzi, lakini sababu Ubungo teyari ni ya CDM yule jamaa wa CUF ana chance kubwa sana kuswitch kwenda ACT na akagombea. Kitakacho tokea ataiba kura za CDM, ikumbukwe CCM wana 30-40% royal members hawa hata mvua inyeshe au jua liwake watapiga kura ya ndio tuu.
Kikubwa ni kimoja UKAWA ilikuwa idea ya kwenye karatasi, lakini in reality nadhani muda sio rafiki kwao. Na vilevile tatizo kubwa kwao ni ZNZ, na huko labda wamuweke Maalim Saif makamu wa raisi, kitu ambacho hakiwezekani hata siku moja. Yaani sumu kubwa ndani ya UKAWA ni CUF maana mtaji wao upo tofauti sana na CDM.