CHADEMA inatumia koti la UKAWA kujikongoja kisiasa

Tunko

Senior Member
Dec 24, 2013
181
41
CHADEMA ilianza kwa kasi kubwa katika medani za siasa nchini kutokana na sera ambazo ziliwavutia watu wengi hasa vijana.

CHADEMA ilianza kuja na sera mbalimbali pamoja na kauli mbiu zenye matumaini kwa wananchi kama vile M4C, na nyingine nyingi ambozo zilivuta hisia nyingi hasa kwa vijana, Lakini siku za hivikaribuni chama hiki kimepoteza mwelekeo kabisa kutokana na kuto kubadilika kwa sera zao na kujikita zaidi kwenye mambo yasio ya msingi kama vile mandamano, kauli mbovu, fukuza fukuza isiyo na mpango ndani ya chama hivo kufanya chama hiki kukosa mwelekeo kutokana na kuchokwa na wananchi.

Kinacho endelea sasa
CHADEMA imejivika koti la UKAWA kama kiki ya kutaka kukubalika zaidi kwa wananchi kutokana na kuvikamata masikio vyama vingine vya siasa kwa nia ya kutaka kujiuza tena kwa wananchi lakini cha ajabu pasipo kujitambua CHADEMA ndio kinazidi kujichimbia kaburi chenyewe pasipo kujijua.

Ushauri viongozi wa
CHADEMA jitafakarini tena na kujirekebisha ili mrudishe heshima yenu kwa jamii kama mwanzo mlivyokuwa mnakubalika.
 
kilichoipaisha chadema sio sera......ingekuwa sera kisingetetereka

slaa na zitto ndio walikipaisha chama, wanaweza jenga hoja

slaa kazidiwa na mahaba ya kupendwa na mamlaka kuu......zitto kasi yake hawakuiweza
 
CHADEMA kama vile inayeyuka lakini nguvu yake si haba tena ni muhimu chama kijiadhali sana, kinachonishangaza zaidi ni kuona chama kimesahau wajibu wake na kushindwa kufanya siasa nje ya UKAWA na BUNGE wakati CCM inajiimalisha kupitia UVCCM na KINANA na NAPE wao kimya hasa BAVICHA na katibu mkuu wake hawana njama za ushindi kuongeza wanachama, haya yangu macho.
 
kwa hiyo kama wamejificha tukusaidiaje sisi...sasa...

kujificha kwao kumekujengea barabara ma kutatua kero zako zoote....kama ndivyo Hongera kubwa.

great people discuss ideas....poor people discuss peoplez.
 
huwezi kutenganisha chadema na Zitto+slaa. kukosekana kwa hao wawili au mmoja wao ndo kaburi la chadema. sote ni mashahidi chadema inajiifia taratibu kabisa.
 
Huu ni ukweli usiopingika na ulio wazi kabisa kwamba, chadema ndio ukawa, hawa wengine ni bendera fuata upepo tu. kama alivyosema jaji warioba kuwa tangantika imevaa koti la muungano, chadema nayo imevaa koti la ukawa...

maamuzi na nafasi muhimu za ukawa zimechukuliwa na viongozi wa chadema, hawa wenzangu na mie, wanazugwa tu ili nao wajione ni sehemu ya ukawa kumbe watu wana mambo yao nyuma ya pazia....hebu fikiria, mwenyekiti wa ukawa bungeni ni freeman mbowe, mwenyekiti wa ukawa nje ni dr W. Slaa..kwanini mwenyekiti mmoja asitoke chama kingine? Na unafahamu fika kuwa hakuna jambo linaweza kuamuliwa au kufanyika bila mwenyekiti kuamua au kukubali...
Hapa ndio ukweli mchungu unapoonekana kwamba chadema imevaa koti la ukawa...hutaki unaacha.

Source: wachambuzi makini wa mambo ya kisiasa nchini.
 
ccm matope matupu...si ni nyinyi mnaobisha kwamba tanganyika haikuvaa koti la muungano??!? vichwa vya uvccm vimejaa....nyau
 
Huu ni ukweli usiopingika na ulio wazi kabisa kwamba, chadema ndio ukawa, hawa wengine ni bendera fuata upepo tu. kama alivyosema jaji warioba kuwa tangantika imevaa koti la muungano, chadema nayo imevaa koti la ukawa...

maamuzi na nafasi muhimu za ukawa zimechukuliwa na viongozi wa chadema, hawa wenzangu na mie, wanazugwa tu ili nao wajione ni sehemu ya ukawa kumbe watu wana mambo yao nyuma ya pazia....hebu fikiria, mwenyekiti wa ukawa bungeni ni freeman mbowe, mwenyekiti wa ukawa nje ni dr W. Slaa..kwanini mwenyekiti mmoja asitoke chama kingine? Na unafahamu fika kuwa hakuna jambo linaweza kuamuliwa au kufanyika bila mwenyekiti kuamua au kukubali...
Hapa ndio ukweli mchungu unapoonekana kwamba chadema imevaa koti la ukawa...hutaki unaacha.

Source: wachambuzi makini wa mambo ya kisiasa nchini.

Amakweli mnawashwa tena sana tu, na bado
 
ImageUploadedByJamiiForums1399793350.180869.jpg
 
Huu ni ukweli usiopingika na ulio wazi kabisa kwamba, chadema ndio ukawa, hawa wengine ni bendera fuata upepo tu. kama alivyosema jaji warioba kuwa tangantika imevaa koti la muungano, chadema nayo imevaa koti la ukawa...

maamuzi na nafasi muhimu za ukawa zimechukuliwa na viongozi wa chadema, hawa wenzangu na mie, wanazugwa tu ili nao wajione ni sehemu ya ukawa kumbe watu wana mambo yao nyuma ya pazia....hebu fikiria, mwenyekiti wa ukawa bungeni ni freeman mbowe, mwenyekiti wa ukawa nje ni dr W. Slaa..kwanini mwenyekiti mmoja asitoke chama kingine? Na unafahamu fika kuwa hakuna jambo linaweza kuamuliwa au kufanyika bila mwenyekiti kuamua au kukubali...
Hapa ndio ukweli mchungu unapoonekana kwamba chadema imevaa koti la ukawa...hutaki unaacha.

Source: wachambuzi makini wa mambo ya kisiasa nchini.

Ni kweli.
 
Back
Top Bottom