CECAFA Kagame Cup 2012 - Live updates

CECAFA Kagame Cup 2012 - Live updates

matokeo si ya kujivunia kwa wanayanga mafunzo kawatoa jasho
 
hongera watani tunawasubiri fainali kama mtavuka nusu
 
Mafunzo wamefanya tu kuwapisha Yanga ili Msonye asijihudhuru na si kwamba wamefungwa.
 
Hongereni watani, ila Mafunzo nao wameniudhi ina maana hawana Kaseja wao kama vile Yanga wasivyokuwa na Boban wao.
 
maneno ya makoye yametimia haya sasa je APR watakubali kuendeleza uteja kwa yanga...
 
Mashabiki wa Yanga naona wananyong'onyea, hapa ujue zote ni timu za Jamhuri ya Muungano, ingawa timu ya visiwani imeingia kama individual country exclusive kwa Muungano.

Mkuu, hadi sasa kuna mpasuko mkubwa ndani ya muungano, usiuongeze hapa tafadhali. Wapenzi wa Yanga wanaipenda Yanga si kwa sababu ni ya Bara, inapendwa kwa sababu ni Yanga, hata leo kuna Wazanzibar walikuwa upande wa Yanga.

Angalia kesho Azam atakavyopata sapoti ya wana Jangwani eti amuue Mnayama, suala ambalo halipendezi.

Mimi ni Yanga, hakuna timu naichukia kama Azam, nawaomba wana Yanga wenzangu kesho tuwe upande wa Mnyama hawa dogo wadharirike kadri iwezekanavyo. Azam ndiyo adui namba 1 wa Yanga, hawa ndiyo walitunyima ubingwa wa Bara, hawa hawa ndiyo walisababisha wachezaji wetu kibao kufungiwa, hawa hawa walipochukua kombe la mapinduzi wakaanza kuwabeza Yanga na Simba; jamani Simba siyo adui wa Yanga ni mtani tu tena tangu zamani.

Wakimtoa Mnyama wataanza, ooh! bado Yanga huku tutakuwa tumewapa sapoti. Chonde chonde jamani, tuwatose Azam, kama Yanga atashindwa kuchukua ubingwa heri Bingwa awe Simba kuliko Azam.

KESHO IWE NI SIKU YA KISASI, AZAM WATOKE KWENYE MASHINDANO HAYA KWANZA HAWANA JIPYA, NI WAZUSHI TU.
 
wasiwasi wangu ni kwa Rashid Gumbo, vipi Nizar Alfan ni majerui???

PrN I salute U,leo ulikuwa unaongea vitu vya msingi sana hiki ni kimojawapo,nilipomuona Gumbo nilikata tamaa kabisa ya upande wa kulia na ndo kilichotokea,hadi anatoka mimi sikuona amefanya nn?...
 
Natabili tena: mpira utakao chezwa kesho na Simba zidi ya Azam nyote mtashangaa: utakuwa na ufundi wa hali ya juu sana.
 
Mkuu, hadi sasa kuna mpasuko mkubwa ndani ya muungano, usiuongeze hapa tafadhali. Wapenzi wa Yanga wanaipenda Yanga si kwa sababu ni ya Bara, inapendwa kwa sababu ni Yanga, hata leo kuna Wazanzibar walikuwa upande wa Yanga.

Angalia kesho Azam atakavyopata sapoti ya wana Jangwani eti amuue Mnayama, suala ambalo halipendezi.

Mimi ni Yanga, hakuna timu naichukia kama Azam, nawaomba wana Yanga wenzangu kesho tuwe upande wa Mnyama hawa dogo wadharirike kadri iwezekanavyo. Azam ndiyo adui namba 1 wa Yanga, hawa ndiyo walitunyima ubingwa wa Bara, hawa hawa ndiyo walisababisha wachezaji wetu kibao kufungiwa, hawa hawa walipochukua kombe la mapinduzi wakaanza kuwabeza Yanga na Simba; jamani Simba siyo adui wa Yanga ni mtani tu tena tangu zamani.

Wakimtoa Mnyama wataanza, ooh! bado Yanga huku tutakuwa tumewapa sapoti. Chonde chonde jamani, tuwatose Azam, kama Yanga atashindwa kuchukua ubingwa heri Bingwa awe Simba kuliko Azam.

KESHO IWE NI SIKU YA KISASI, AZAM WATOKE KWENYE MASHINDANO HAYA KWANZA HAWANA JIPYA, NI WAZUSHI TU.

Pamoja sana Mkuu,binafsi naichukia sana hii team inayoitwa Azam na.....ila nako kui'support Simba inataka moyo,anyway nitajaribu, ngoja kesho ifike...inshallah MUNGU ajalie uhai
 
Back
Top Bottom