CECAFA Kagame Cup 2012 - Live updates

CECAFA Kagame Cup 2012 - Live updates

Tutapunguza mawili tu

Five-goal-Simba-rout-Yanga.jpg

Hili bango lenu very soon litakuwa outdated hence history,mimi nawaombea mvuke leo kwa Azam ili kuongeza possibility ya kukutana fainali au kwenye kutafuta mshindi wa 3 ili na mimi nijipatie Avator...MUNGU awaepushe kina Bahanuzi,Kiiza na wachezaji wote wa Yanga na majeruhi ili tuje tuwafunge mdomo
 
Vita 1 Atletico 0 dk ya 6

Hii inaashiria kuwa Simba watakutana tena na AS Vita Club napo patakuwa patashika nguo kuchanika! Bila shaka AS Vita hawatakubali kuondoshwa mashindanoni. Haya yakitimia na huku APR wakivunja uteja kwa Yanga bila shaka watani watakutana saa 8 mchana siku ya fainali kama ilivyotokea kipindi kileee!

Je Yanga wataweka ngumu kuingia uwanjani dhidi ya Simba tena? Bila shaka wataingia kwa kishindo, je watakubali kufungwa tena na Simba hasa ukizingatia mabao waliyofungwa katika mechi ya mwisho? Hapana shaka hawatakubali ujinga huo uendelee hasa ukizingatia hali ya Mnyama ilivyo. Huu utakuwa ni muda wa kumchinja Mnyama japo haliwi katika kipindi hiki cha mwezi Mtukufu wa Ramadhan. Angekuwa analiwa angepelekwa Jangwani na wazee wangepata supu ya futari. La haula, li mnyama lenyewe haliliwi!
 
Hii inaashiria kuwa Simba watakutana tena na AS Vita Club napo patakuwa patashika nguo kuchanika! Bila shaka AS Vita hawatakubali kuondoshwa mashindanoni. Haya yakitimia na huku APR wakivunja uteja kwa Yanga bila shaka watani watakutana saa 8 mchana siku ya fainali kama ilivyotekea kipindi kileee!

Je Yanga wataweka ngumu kuingia uwanjani dhidi ya Simba tena? Bila shaka wataingia kwa kishindo, je watakubali kufungwa tena na Simba hasa ukizingatia mabao waliyofungwa katika mechi ya mwisho? Hapana shaka hawatakubali ujinga huo uendelee hasa ukizingatia hali ya Mnyama ilivyo. Huu utakuwa ni muda wa kumchinja Mnyama japo haliwi katika kipindi hiki cha mwezi Mtukufu wa Ramadhan. Angekuwa analiwa angepelekwa Jangwani na wazee wangepata supu ya futari. La haula, li mnyama lenyewe haliliwi!

Sisi tunawataka hata kwenye kutafuta mshindi wa 3 potelea mbali-liwalo na liwe,Simba sasa hivi dhorfulhali...niliwaambia hapa mapema tu kuwa mafanikio yao ya mwaka jana yalipatikana kwa jitihada za Okwi na Marehemu Mafisango(RIP) wakanibishia sana,sasa hv Kocha wao analia
 
Mkuu nimedhihirisha uoga wako wa kutotaka kukutana na sisi kwenye Kagame hii,mnataka mkiwa mnaendelea kuchangia hapa JF muendelee kutumi ile avator ya score board ya 5 - 0,unajua tukikutana ile itakuwa outdated....usijali lkn hata ukivuka kesho kwa maswaiba zenu utakuwa bado una kimbembe cha kukutana na Atletico au AS Vita na ule ndo utakuwa mwisho wenu rasmi,kwahiyo punguza dua mbaya kwetu kwa kiwango chenu cha sasa hv hakuna matarajio ya kukutana na sisi.
Mkuu mimi sikuogopa kukutana na nyie, lakini kiukweli nilitaka Mafunzo washinde kwanza kuimarisha Muungano, pili kuwapunguza kuongea sana baada ya kucheza kandanda safi na APR mkaona kama ndo mmemaliza.

Sisi kama tutapita leo timu ninayoihofia ni AS VITA, lakini sio Atletico kuelekea nusu fainali, ndo niko Taifa sahivi nawacheki si wazuri sana, kama watashinda na sisi tukashinda matumaini ya kufikika fainali ni zaidi ya asilimia 60, lakini kwa Wacongo ni 50 kwa 50.
 
Sisi tunawataka hata kwenye kutafuta mshindi wa 3 potelea mbali-liwalo na liwe,Simba sasa hivi dhorfulhali...niliwaambia hapa mapema tu kuwa mafanikio yao ya mwaka jana yalipatikana kwa jitihada za Okwi na Marehemu Mafisango(RIP) wakanibishia sana,sasa hv Kocha wao analia

kutofanikiwa kwenu mwaka jana kulitokana na jitihada za Canavaro. Niyonzima, Nurdin na Rashidi Gumbo siyoeee!!!!,
 
iwe Vita club au Atretico yeyote itakayo kutana Simba nusufainali kama Simba itafanikiwa kuvuka basi jue kaliwa.
 
Na hawataamini kuvuka huku kwa tabu ndo kumeishia hapohapo kwa mafunzo from now ni "clean win" ndani ya dk 90 mpaka tunachukua Kombe
Mkuu Yanga bado timu dhaifu tu, hebu niambie akiumia Niyonzima na Kiiza replacement ni nani? First eleven yenu ni nzuri sawa lakini msipopata magoli ya mapema na mkafanya sub ndo kwisha habari yenu, Tegete anakimbia kimbia tu utafikiri tajiri wa kiarabu anamiliki visima vya mafuta.
 
kutofanikiwa kwenu mwaka jana kulitokana na jitihada za Canavaro. Niyonzima, Nurdin na Rashidi Gumbo siyoeee!!!!,

Nakubali kabisa kuwa walichangia kwa namna moja au nyingine kutofanikiwa kwetu kwa msimu uliopita,kinachonishangaza ni jinsi washabiki msivyotaka kulikubali hili kuwa bila Okwi na Marehemu basi Kocha lazima ataonekana hajui,Rage na yeye kasoro zake zitaanza kuonekana waziwazi kwa ufupi team itaboronga na migogoro itaibuka kama kawaida,take my words PrN
 
Sisi tunawataka hata kwenye kutafuta mshindi wa 3 potelea mbali-liwalo na liwe,Simba sasa hivi dhorfulhali...niliwaambia hapa mapema tu kuwa mafanikio yao ya mwaka jana yalipatikana kwa jitihada za Okwi na Marehemu Mafisango(RIP) wakanibishia sana,sasa hv Kocha wao analia
Acha uongo wako wewe, sisi tumetoka kuchukua kombe bila ya hao uliowataja.
 
Mkuu Yanga bado timu dhaifu tu, hebu niambie akiumia Niyonzima na Kiiza replacement ni nani? First eleven yenu ni nzuri sawa lakini msipopata magoli ya mapema na mkafanya sub ndo kwisha habari yenu, Tegete anakimbia kimbia tu utafikiri tajiri wa kiarabu anamiliki visima vya mafuta.

Kiongozi,hujaijua Yanga ya sasa hivi wewe embu angalia hii list:-

1. Berko/Barthez
2. Juma Abdul/Godfrey Taita
3. Oscar Joshua/David Luhende
4. Canavaro/Ladislaus Mbogo
5. Kelvin Yondani/Chuji anaweza ku'cover hapa
6. Chuji akicheza mahala pake/Kijiko
7. Nizar/Rashid Gumbo/Shamte Ally
8. Febregus/kuna mtoto anaitwa Domayo...huyu ni noma
9. Kiiza/Tegete
10. Bahanuzi/kuna Dogo anaitwa Simon Msuva...huyu ni balaa
11. Mwasyika/Idrissa Rashid

Nafikiri nimejibu swali lako kiufasaha,yaani hao waliokuwa bold ndo 1st eleven ambayo duru za ndani kabisa zimetonya Milovan hataki kabisa kukutana nayo ksbb anajua hana wachezaji wa kuwazuia na hao wengine ndo sub ambazo na zenyewe moto yaani kama ugali moto-mboga moto,bado kuna kina Meddy Kagere wakifanikiwa kusajiliwa itakuwa HATARE siyo HATARI,hapo sijawagusia madogo wengine kama Omega Seme na Salum Telela....Kaka usichezee Yanga hii Kaka
 
Nakubali kabisa kuwa walichangia kwa namna moja au nyingine kutofanikiwa kwetu kwa msimu uliopita,kinachonishangaza ni jinsi washabiki msivyotaka kulikubali hili kuwa bila Okwi na Marehemu basi Kocha lazima ataonekana hajui,Rage na yeye kasoro zake zitaanza kuonekana waziwazi kwa ufupi team itaboronga na migogoro itaibuka kama kawaida,take my words PrN

Mkuu Anselm usihofu, sio lazima wakubali kwa maneno hapa jamvini; matokeo ya timu yao yanaonesha kukubali kuwa bila Okwi, Mafisango - Simba si lolote wala si chochote, utamwona Sunzu aliyekuwa scavenger wa mipira ya marehemu na Okwi sasa anaonekana kichekesho tu, anakosa hadi penati kichovu mno.

Angalia mfano huu, mtu unaposafiri kutoka Ubungo kwenda Kariakoo huku ukijua kuwa nauli ni Tsh. 300/= japo hujakubali kwa maneno, unapoingia ndani ya basi na kuanza safari ni wazi kuwa umekubali nauli hiyo hakuna punguzo wala nini, konda akifika mpe chake; ndivyo ilivyo kwa mashabiki wa Mnayama hata kama hawataki kukiri kwa maneno, matokeo ya timu yao yanakubali kwa vitendo umuhimu wa Okwi na Marehemu.
 
Yaaani yebo yebo mafanikio kidogo kelele nyingi hiki ndio mnachoweza
 
Acha uongo wako wewe, sisi tumetoka kuchukua kombe bila ya hao uliowataja.

Ha ha ha ha Mbavu zangu,hivi lile kombe la kuku na lenyewe mnalihesabu by the way usije kukuta Viongozi wenu wameingiza tayari kwenye kumbukumbu muhimu za Club?
 
Welcome back to the national stadium here in Dar es Salaam (SS9). Atletico 0-1 AS Vita.
 
Tupeni update jamani,dk ya ngapi na ngapingapi hapo Taifa,Masuke tupe taarifa
 
KOCHA Mkuu wa Simba SC, Milovan Cirkovic, ametangaza kikosi kitakachoshuka dimbani leo hii dhidi ya Azam katika Robo Fainali ya Kombe la Kagame ambapo wachezaji Uhuru Selemani na Jonas Mkude wataanza.

Kikosi hicho kinaundwa na Juma Kaseja, Haruna Shamte, Shomari Kapombe, Juma Nyoso, Lino Masombo, Jonas Mkude, Mussa Mudde, Mwinyi Kazimoto, Felix Sunzu, Haruna Moshi na Uhuru.

Benchi watakuwepo; Waziri Hamad, Obadia Mungusa, Kiggi Makassi, Salim Kinje, Kanu Mbiyavanga, Dani Mrwanda na Amri Kiemba.
 
Back
Top Bottom