Wakuu
Kwanza tunashukuru sana kuwa Msemaji wa CCM, amethibtisha mwenyewe hofu inayotokana na kutokuwa na uhakika wa ushindi kila wanapokutana na CHADEMA katika uchaguzi wowote, eneo lolote, mjini na vijijini.
Kilichotokea ni mtindo wa CCM ambao bila shaka yoyote utafikishwa mwisho muda si mrefu, kwa kasi ya mabadiliko na uasi mkubwa dhidi ya CCM unavyozidi kuongezeka.
Wamemtisha aliyekuwa mgombea wa CHADEMA hadi ameshindwa kurudisha fomu. Kwa sababu tu baba yake na mgombea huyo ni mwanachama wa CCM. Ni staili ile ile ambayo CCM chini ya au kwa maelekezo ya Makamba wametisha wagombea na hata viongozi halali wa wananchi wanaotokana na CHADEMA huko Lushoto.
Kwa taarifa za uhakika tulizonazo ni kwamba CHADEMA na mgombea wake, wanakubalika sana katika kata ya Langido, CCM wakamfuata baba yake ambaye ni mwanachama wao, wakamwambia iwapo atamruhusu mtoto wake aendelee kugombea kisha ashinde uchaguzi huo, watamfungulia kesi ambayo hatatoka. Walisema watamhusisha na vurugu fulani zilizotokea hivi karibuni ambapo wananchi walipinga uchakachuaji uliofanyika kwenye uchaguzi wa mabaraza ya katiba.
Wakaenda mbali kuiambia familia nzima haitakuwa salama. Hivyo wajiandae kwa umaskini, kwa yale watakayofanyiwa.
Ni mambo yale yale yaliyofanyika pia kule Ruaha, ambako Kanali Kinana baada ya kuulizwa swali kuhusu tuhuma za tembo, yeye na msafara wake wakavunja mkutano haraka na kukimbia, wakiwatuhumu wanakijiji kuwa wametumwa na CHADEMA.
Matokeo yake CCM wametumia nguvu kubwa, ikiwemo kumbambikia kesi aliyekuwa mgombea kijiji hicho kwa tiketi ya CHADEMA na hadi sasa yuko gerezani.
Wananchi walipomjazia fomu na kuirejesha kwa msimamizi wa uchaguzi, CCM wakaogopa aibu ya kushindwa na mtu aliye gerezani (kama ilivyotokea Tarime), wakaelekeza isikubaliwe. Hadi leo wananchi wamemkataa mtu wa CCM aliyepitishwa kwa mabavu bila kupingwa.
Ofisi ya Katibu Mkuu, kupitia Kurugenzi ya Kampeni na Uchaguzi, imeshatoa maelekezo kwa hatua za haraka kuchukuliwa.
Ni kata hiyo moja pekee kati ya 26, ambako hadi sasa CHADEMA haina mgombea.
Makene
0688 595831/ 0752 691569