Cheche Mtungi
JF-Expert Member
- Nov 14, 2010
- 2,619
- 776
Ben Saanane njoo umjibu huyu gamba Nape Nnauye
Last edited by a moderator:
Hapa si kumbeza Nape ,swali ni kwa nn hatuna mgombea kwenye hiyo kata,hatuwezi kuendelea kujifariji kwa uzembe wa namna hii na baadae tuanze kutafuta sababu,ikumbukwe chama kimepuuzia matokeo ya awali (kushindwa) kwa wanachama wetu kwenye uchaguzi wa mabaraza ya katiba,kwa mtu yeyote mkweli na anayefikiria kwa kina uchaguzi ule ulikuwa kipimo cha uchaguzi wa serikali za mitaa 2014 na tulichovuna ndicho hicho tutakachovuna hapo mwakani iwapo juhudi za makusudi hazitachukuliwa.Rai yangu Chadema ihimize uchaguzi wa ndani ya chama watu wenye moyo wa kufanya kazi wapatikane na tuachane na hawa wanaofanya kazi kwa mazoea.J2 njema.
Hivyo vyama vingine havijajinasibu kuchukua nchi 2015; anyways naona jamaa hawana haja na kata wao watakomaa tu na Ikulu mbona hata hiyo nayo ni poa sana kwani kwenye kata kuna ulaji ganiChadema, Chadema, Chadema... Nape we ni muenezi wa CCM.. Why should all your speeches start with Chadema? Kuna vyama vingine 18 ambavyo vilikuwa na mandate ya kuweka mgombea huko... Lakini asubuhi yote hii umekurupuka kitandani kuja kuandika kuhusu CDM. Kweli wamekushika pabaya...
Kuna hali ya kuridhika na kujiaminisha kuwa shughuli ya ukombozi tayari imetimia na kusahau kuwa kilichowadia ni saa ya ukombozi! Bado kuna milima na mabonde nani atakuwa tayari kwenda jela baada ya kuachia madaraka kirahisi hivyo? Nani atakubali kufilisiwa na kuishi kwenye umasikini anaousoma kwenye vitabu na kuangalia kwenye film? Ukweli ni kwamba akina Ridhiwan na Lowasa wapo tayari kutoa kila walichonacho na kuanza upya lakini wakiwa ndani ya mikono salama ya Chama cha Mapinduzi.Dr Slaa anajua vyema haya yote wasiwasi wangu ni hizi kurugenzi zinazomzunguka.Naunga mkono hoja huu ni upuzi usio kubalika waje hapa waseme kwanini hawajasimamisha mtu. Unless watuambie mgombea amenunuliwa na kuna hila hapo tutawaelewa na hata hiyo haitoshi kwani kwa vyovyote hila zina julikana sasa inakuwaje hawajajiandaa kwa hizi hila?
Nampenda huyu Nepi ninayo kwa sababu amekijenga sana chama chetu CDM hivi mnadhan bila ya kuropoka ropoka huyu bui bui cc kama cc cdm tungekua wapi 4now? Yaan anakijenga chama chetu vere weli halafu anabomoa kwao akhsante permpas
Mkuu acha kuropoka ujinga hapa JF.Hapa si kumbeza Nape ,swali ni kwa nn hatuna mgombea kwenye hiyo kata,hatuwezi kuendelea kujifariji kwa uzembe wa namna hii na baadae tuanze kutafuta sababu,ikumbukwe chama kimepuuzia matokeo ya awali (kushindwa) kwa wanachama wetu kwenye uchaguzi wa mabaraza ya katiba,kwa mtu yeyote mkweli na anayefikiria kwa kina uchaguzi ule ulikuwa kipimo cha uchaguzi wa serikali za mitaa 2014 na tulichovuna ndicho hicho tutakachovuna hapo mwakani iwapo juhudi za makusudi hazitachukuliwa.Rai yangu Chadema ihimize uchaguzi wa ndani ya chama watu wenye moyo wa kufanya kazi wapatikane na tuachane na hawa wanaofanya kazi kwa mazoea.J2 njema.
Mkuu acha kuropoka ujinga hapa JF.
Kwanini unataka kuchanganya maji taka na maji safi kwenye chombo kimoja?
Kila mtu mdadisi anajua Chaguzi za mabaraza ya Katiba zilikuwa ni Uchafu mtupu.
Hata kama wagombea wa CHADEMA wangekuwa ni Mitume wa Mungu na wapiga kura wengi wangekuwa ni Malaika wa Mungu, bado CHADEMA ingeshindwa tu. Na ingeshindwa sio kwa sababu ya wingi wa kura bali kutokana na kanuni na mfumo wa uendeshaji wa chaguzi zile zilipangwa makusudi kabisa kuifanikisha CCM.
*Turudi kwenye mada, Swali je ni kweli CHADEMA wameshindwa kusimamisha mgombea huko Ruvuma, na kama ni Kweli kuna sababu gani ya msingi kushindwa kufanya hivyo?
Viongozi na Wasemaji wa CHADEMA tunataka watupe majibu hapa hapa JF tena sasa.
Mkuu,bahati mbaya sana siuelewi vizuri ushiriki wako ktk siasa zetu ,lakini nikukumbushe tu jambo moja juu ya uchaguzi wa mabaraza ya katiba ni ulikuwa ukiwashirikisha wananchi wa mtaa/kitongoji husika,sahau juu ya uchakachuzi uliochukuwa nafasi yake kwenye ngazi ya kata,kwetu sisi ambao huwa tunapenda kufanya utafiti hata kwa vitu vidogo vinavyotuzunguka ni kuwa wagombea wetu wengi ngazi hiyo chini kabisa walishindwa na sababu kubwa ni sisi kama chama hatukuwa tumejipanga vema.Kuhusu mada husika majibu ya aina yoyote toka kwa viongozi wetu hayawezi kusaidia lolote kumbuka kitendo cha kutoweka mgombea ni sawa nakujihukumu kifungo cha miaka 5 so haindoi wahusika kuwajibika.Uliwahi kusikia kisa cha mfalme Daudi baada ya kujichukulia mke wa mtwana wake? Pamoja na kujuta kwa kuyararua mavazi yake ya kifalme na kuvaa marapurapu ya magunia huku akijipaka majivu mwili mzima na kutoa toba kwa muumba wake bado hakukwepa adhabu ya Mungu.Mkuu acha kuropoka ujinga hapa JF.
Kwanini unataka kuchanganya maji taka na maji safi kwenye chombo kimoja?
Kila mtu mdadisi anajua Chaguzi za mabaraza ya Katiba zilikuwa ni Uchafu mtupu.
Hata kama wagombea wa CHADEMA wangekuwa ni Mitume wa Mungu na wapiga kura wengi wangekuwa ni Malaika wa Mungu, bado CHADEMA ingeshindwa tu. Na ingeshindwa sio kwa sababu ya wingi wa kura bali kutokana na kanuni na mfumo wa uendeshaji wa chaguzi zile zilipangwa makusudi kabisa kuifanikisha CCM.
*Turudi kwenye mada, Swali je ni kweli CHADEMA wameshindwa kusimamisha mgombea huko Ruvuma, na kama ni Kweli kuna sababu gani ya msingi kushindwa kufanya hivyo?
Viongozi na Wasemaji wa CHADEMA tunataka watupe majibu hapa hapa JF tena sasa.
Ametoa tu taarifa na siyo kutangaza ushindi. Ni jukumu lake kufanya hivyo. BTW, hata atangaze nani, hali halisi haibadiliki! CCM ni washindi, na wataendelea kuwa hivyo daima!
Hoja mufilisi kabisa, yaani wewe unataka kumhubiri Mungu bila kumtaja shetani?!!!! Injili gani hiyo?
Katika hali inayodhihirisha Nape Nauye anaiogopa sana chadema nikutokufikiria kuwa Tanzania kunavyama vingine vya upinzani....mkuu NCCR hauijui? au CUF umeisahau? Vipi kuhusu TLP? Na kile chama chenye bendera nyingi kuliko idadi ya wanachama (ADC) haukitambui? au hivi vyote havijaweka wagombea? Kama havijaweka wagombea mbona hauvisemi?.....bwana mdogo Nape kitu kikubwa ambacho mwenyezi Mungu ametunyima binadamu nikutokuijua kesho yetu suala linalotufanya tuamini kwamba nchi hii itakuwa chini ya ccm milele....Naomba nikutakie jumapili njema!