Uchaguzi 2020 CHADEMA na ACT-Wazalendo wajitoa katika uchaguzi wa Diwani kata ya Igumbilo-Iringa. Mgombea wa CCM apita bila kupingwa

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
3,376
2,000
CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) na ACT-Wazalendo, vimejitoa katika uchaguzi wa udiwani kata ya Igumbilo, Manispaa ya Iringa uliopangwa kufanyika Desemba 8, mwaka huu.

Kata hiyo haikufanya uchaguzi katika uchaguzi mkuu uliofanyika nchini Oktoba 28, baada ya kifo cha mgombea wa CCM kutokea Oktoba 16, hivyo kusababisha Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) kuuahirisha.

Kutokana na kujitoa huko, Msimamizi wa Uchaguzi wa Jimbo la Iringa Mjini, Hamid Njovu, jana alimtangaza Boniface Kilave kuwa mshindi wa udiwani wa kata hiyo baada ya kupita bila kupingwa.

Novemba 13, NEC kupitia Kaimu Mkurugenzi wa Uchaguzi, Gerald Mwanilwa, alitangaza kufanyika kwa uchaguzi mdogo kwenye kata tatu ikiwamo hiyo.

Kata nyingine ni Nyahanga iliyoko Halmashauri ya Mji wa Kahama mkoani Shinyanga na Kibosho Kati, kwenye Halmashauri ya Wilaya ya Moshi, mkoa ni Kilimanjaro.

Katika kata hiyo ya Igumbilo, wagombea ambao ni Wilbert Kilave (CHADEMA) na Mahamad Rassa (ACT- Wazalendo), walitangaza kujiondoa katika kinyang’anyiro hicho.

Njovu alisema wagombea hao waliwasilisha barua zao za kujitoa kugombea zikiambatanishwa na viapo vyao vya tamko la kujitoa vilivyotolewa mbele ya hakimu juzi.

Alisema barua hizo za kujiondoa zilizingatia kifungu cha 50 cha sheria ya uchaguzi wa serikali za mitaa, sura ya 292 ya mwaka 2015 na kanuni zake.
Alisema diwani mteule atapatiwa hati ya kuchaguliwa kwenye nafasi hiyo ifikapo Desemba 8, ambayo ni siku iliyopangwa kufanyika uchaguzi huo.

IPPMedia
 

Dam55

JF-Expert Member
Oct 8, 2015
4,666
2,000
Halafu wataleta Kura za kwenye mabegi kutoa ushahidi kuwa wameibiwa Kura kwenye huo uchaguzi mdogo huku wakiwa wamejitoa haito shangaza kabisa.

Wanajua wakishiriki kwenye huo uchaguzi mdogo kisha wakashindwa itadhihirisha kuwa watanzania wamewakataa hata kwenye Kule wanakodai kuporwa ushindi.

Maigizo bado yanaendelea hapo.
 

FUSO

JF-Expert Member
Nov 19, 2010
21,655
2,000
Msimamo wa Prof. Lipumba ulikuwa sahihi mno kwamba mfumo wa uchaguzi nchi hii ni wa hovyo kupata kutokea...hivyo chama chake hatashiriki uchaguzi uchaguzi wowote ule utakaondaliwa na Tume hii ya Uchaguzi... nafikiri ndiyo ilivyo misimamo ya CDM na ACT wazalendo pia.

Lakini cha ajabu Prof kama kawaida yake.... Mzee wa NAFSI IMENISUTAA... tayari kashakula matapishi yake - kasema uchaguzi ulikuwa huru na haki...na uchaguzi huu chama chake kitakwenda kushiriki.

Kurudi kwenye mada, kushiriki uchaguzi wowote ule unaoandalikwa na tume hii ya uchaguzi itakuwa ni sawa na kula matapishi yako, cha msingi kuokoa fedha na raslimali watu basi Tume iwe inawatangaza wagombea wa CCM kwamba wamepita bila kupigwa.
 

brazaj

JF-Expert Member
Jul 26, 2016
6,690
2,000
CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) na ACT-Wazalendo, vimejitoa katika uchaguzi wa udiwani kata ya Igumbilo, Manispaa ya Iringa uliopangwa kufanyika Desemba 8, mwaka huu...

Kwanini wachanganyiwe magunzi? Tochi haitawaka!
 

denooJ

JF-Expert Member
Mar 31, 2020
3,833
2,000
Wamefanya vizuri, na zile kata nyingine zilizobaki nako wakapite bila kupingwa.

Yale maigizo yao ya kitoto hakuna mtu anataka kuyaona tena.
 

tindo

JF-Expert Member
Sep 28, 2011
38,246
2,000
Halafu wataleta Kura za kwenye mabegi kutoa ushahidi kuwa wameibiwa Kura kwenye huo uchaguzi mdogo huku wakiwa wamejitoa haito shangaza kabisa.

Wanajua wakishiriki kwenye huo uchaguzi mdogo kisha wakashindwa itadhihirisha kuwa watanzania wamewakataa hata kwenye Kule wanakodai kuporwa ushindi.
Maigizo bado yanaendelea hapo.

Ule haukuwa uchaguzi, bali maonyesho ya ujinga wa mtu mweusi kwenye box la kura.
 

mwengeso

JF-Expert Member
Nov 27, 2014
7,909
2,000
Wamefanya la maana kwani nchi hii sasa hakuna uchaguzi bali kuna uchafuzi.
Mkuu Salary Slip wewe pamojana wenzio humu JF, mshauri M/kiti wa chama avunje chama au ajiuzuru ili nanyi mpate kuwa HURU kifikra. Naamini mnaumia sana rohoni kutetea kitu mnachojua kwa uhakika kuwa ni uwongo
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom