CCM YAPITA KATA YA LANGILO RUVUMA bila kupingwa!

CCM YAPITA KATA YA LANGILO RUVUMA bila kupingwa!

Mimi nasubiri kauli ya viongozi wa chedema kwanza kwa nini kata hiyo hawakuweka mgombea from their statement nitachangia na kujenga hoja mimi simuamini Nape, ni vuvuzela tu hilo!!

Mkuu, Tumaini Makene ameshatolea ufafanuzi, angalia Post #64

OMBI KWA WENYE JUKWAA: Kama inawezekana, mtu aki-quote post ya mtu, quotation ioneshe original ni Post No. ngapi na iko page namba ngapi of course pia na owner wa post kama ilivyo sasa. Hii itasaidia ku-jump easily to the original post badala kuanza kwenda page-by-page kuitafuta.

If possible pia, anaye-quote asiweze kwa namna yoyote kuifanyia editing original post (specifically kubadili text) labda formatting kama color, bold, underline, au italics ili kuweza kuweka reference to specific areas of interest.

For action: Invisible, Maxence Melo, Buchanan, et. al. (whoever may help).
 
Last edited by a moderator:
Kwanza hajasema wameshinda kwa kura ngapi na zile pesa za kuhonga wametoa ngapi? maana darasanai kama uko mtu mmoja hata ukipata maksi 20 ya miamoja bado wewe unaonekana umeongoza. Ni ujinga mtu kufurahia umeshinda wakati timu pinzani haikuja uwanjani na ninachokiamini mimi chadema huwa hawakurupuki huwa wako strategically na ndo maana inawasumbua sana ccm na serikali yake. mmeimaliza cuf lkn chadema hamtoweza sana sana mtaikubali subirini moto wa 2015
 
Nape unashangaa nini? CHADEMA ni chama cha kikanda, nguvu na raslimali inapelekwa Arusha; mwenye macho haambiwi tazama

Nashangaa unashangaa ya CHADEMA! Hata TANU ilianzia na kujikita Dar es salaam.!

Kwani Nape si anajua kwamba kwa jinsi wanavyo tumia taasisi za serikali kukandamiza demokrasia ya kweli, pana kosekana "UWANJA ULIO SAWA" ili kila chama kuonyesha umahiri wake wa kunadi sera za kumletea mTanganyika maendeleo?

Si umeona kule Bumbuli Kwetui kwa Makamba? Ile ya kumuendea na askari/ Mkuu wa wilaya, kiongozi aliye chaguliwa na watu kumlazimisha ajiuzulu ndio kujisifia huko? Namshangaa Nape. Kama anaiona CHADEMA haina lolote na kesi za kupika kwa viongozi wa CHADEMA ni za nini?

Kwa nini POLICCM wapo busy kuhangaika na CHADEMA kwa maagizo yao?

Kwa nini RCs na DCs ni Makada wa CCM kinyume na majukumu waliyo pewa kikatiba?

Hata MBUYU ULIANZA KAMA MCHICHA.
 
Nchi ya Langilo?

Ndio mana niliwakebehi kwenu kuchukua nchi si kukomaa na Ikulu? kwani kuchukua kata ya Longilo au kata zingine kwenu ni kuchukua nchi? Kuchukua nchi ni kukomaa na Ikulu bhana
 
Wakuu

Kwanza tunashukuru sana kuwa Msemaji wa CCM, amethibtisha mwenyewe hofu inayotokana na kutokuwa na uhakika wa ushindi kila wanapokutana na CHADEMA katika uchaguzi wowote, eneo lolote, mjini na vijijini.

Kilichotokea ni mtindo wa CCM ambao bila shaka yoyote utafikishwa mwisho muda si mrefu, kwa kasi ya mabadiliko na uasi mkubwa dhidi ya CCM unavyozidi kuongezeka.

Wamemtisha aliyekuwa mgombea wa CHADEMA hadi ameshindwa kurudisha fomu. Kwa sababu tu baba yake na mgombea huyo ni mwanachama wa CCM. Ni staili ile ile ambayo CCM chini ya au kwa maelekezo ya Makamba wametisha wagombea na hata viongozi halali wa wananchi wanaotokana na CHADEMA huko Lushoto.

Kwa taarifa za uhakika tulizonazo ni kwamba CHADEMA na mgombea wake, wanakubalika sana katika kata ya Langido, CCM wakamfuata baba yake ambaye ni mwanachama wao, wakamwambia iwapo atamruhusu mtoto wake aendelee kugombea kisha ashinde uchaguzi huo, watamfungulia kesi ambayo hatatoka. Walisema watamhusisha na vurugu fulani zilizotokea hivi karibuni ambapo wananchi walipinga uchakachuaji uliofanyika kwenye uchaguzi wa mabaraza ya katiba.

Wakaenda mbali kuiambia familia nzima haitakuwa salama. Hivyo wajiandae kwa umaskini, kwa yale watakayofanyiwa.

Ni mambo yale yale yaliyofanyika pia kule Ruaha, ambako Kanali Kinana baada ya kuulizwa swali kuhusu tuhuma za tembo, yeye na msafara wake wakavunja mkutano haraka na kukimbia, wakiwatuhumu wanakijiji kuwa wametumwa na CHADEMA.
Matokeo yake CCM wametumia nguvu kubwa, ikiwemo kumbambikia kesi aliyekuwa mgombea kijiji hicho kwa tiketi ya CHADEMA na hadi sasa yuko gerezani.

Wananchi walipomjazia fomu na kuirejesha kwa msimamizi wa uchaguzi, CCM wakaogopa aibu ya kushindwa na mtu aliye gerezani (kama ilivyotokea Tarime), wakaelekeza isikubaliwe. Hadi leo wananchi wamemkataa mtu wa CCM aliyepitishwa kwa mabavu bila kupingwa.

Ofisi ya Katibu Mkuu, kupitia Kurugenzi ya Kampeni na Uchaguzi, imeshatoa maelekezo kwa hatua za haraka kuchukuliwa.

Ni kata hiyo moja pekee kati ya 26, ambako hadi sasa CHADEMA haina mgombea.

Makene

0688 595831/ 0752 691569

Maelezo yako hayatoshi mkuu mlipaswa kujua hizi move zote za CCM kumtisha mgombea wetu au mkampa nguvu na support au mkamtoa na kuweka kamanda mwingine mwenye moyo aliye tayari kufungwa au hata kufa kwa ajili ya chama! haya yalipaswa kufanyika kabla ya dead line ya kurudisha fomu!! Hilo ni kosa kubwa sana la kiuongozi lazima uongozi ukiri umekosea,. ona sasa Nape anaanza matambo!!
 
Katika hali inayodhihirisha kuwa Chadema wana kufa kwa kasi ya ajabu, wamefikia mahali pa kushindwa kuwa na mgombea wa Udiwani kata ya Langido mkoani Ruvuma kiasi cha kuifanya CCM ipite bila kupingwa na hivyo kuanza na kata moja tayari kati ya kata 26 zinazofanya uchaguzi mdogo.

kama watani hata kusimamisha mgombea tu kwenu inakuwa tabu tena wa kata kweli mko serious kutaka kuaminiwa kukabidhiwa nchi? Hili limenifanya nikumbuke maeneo kibao mwaka 2010 ambayo majimbo na kata hamkusimamisha agombea au mliwatelekeza pale mliposimamisha! Na sasa nasikia nguvu kubwa mnapeleka Arusha!!!!! Mwenye akili na atafisiri hili!

Itawachukua muda kidogo kukomaa!

mbona unaisemea chadema?,wenzenu wa Cuf vipi?. Utakufa kwa presha
 
katibu mwenezi unaanzisha uzi kuhusu ishu ndogo namna hii.

wewe ndo unakufa kwa kasi ya ajabu.
 
Asante sana kwa taarifa japokuwa imechelewa kidogo kwa sisi wapenzi wa Chadema humu mtandaoni. Lakini kuna mambo kadhaa ya kuuliza na kushauri.
1/Katika hili kuna namna yoyote kisheria kureverse situation?

2/Kwanini CHADEMA ikaligundua hili baada ya muda wa mwisho wa kurudisha form na sio kabla?

3/Mwanachama akishateuliwa na CHADEMA anakuwa ni mgombea wa chama na sio binafsi, ni vipi hili mkaruhusu mtu binafsi akajiamulia kutorudisha fomu na chama kikakaa kimya?

4/Hila kama hizi zimeshatokea mara nyingi na zitaendelea kutokea sana mpaka kufikia 2015, CHADEMA imejiandaaje katika hili kuanzia nafasi ya Kijiji, kitongoji, kata, Ubunge na Urais?

5/Je CHADEMA haina utaratibu wowote wa kuwa na reserve ya watu wa kugombea kama itatokea aliyeteuliwa kalaghaiwa kabla ya muda wa mwisho wa kurudisha fomu?

6/Sasa CHADEMA imejiandaa vipi na wagombea watakaojitoa(Kwa kuwa wamehongwa au kutishwa na CCM) wakati yatari wameshapitishwa na tume ya Uchaguzi?

7/Chadema imejipanga vipi na hila kama za 'Chitambala 2009' za mgombea kuondolewa kwenye Uchaguzi kwa sababu tu kuna makosa ya kisheria kwenye form za kugombea?

mkuu kudos, maswali yako utafikiri ulikuwa kichwani kwangu!!
 
Nina wasiwasi na weledi wa aliyekupa nafasi uliyo nayo kichama Nape Nnauye. Nadhani hujui ethics za ukatibu uenezi wa chama kwani huwezi kuwa mwenezi wa CCM na CHADEMA at the same time!

Na kwanin CHADEMA tu while we have 18 other political parties?
 
Last edited by a moderator:
Tunashukuru sana kwa taarifa katibu mwenezi wetu msaidizi,sasa hii taarifa usisahau pia kuipitisha kwa bosi wako jj mnyika,kwa hatua zingine.pia mkumbushe msaidizi a katibu mkuu wa cdm ndugu kinana,mwambie mbona siku hizi hafanyi kazi zake vizuri mara baada ya kuperfom vizuri pale moro?
 
Kwanza natanguliza pole na mjukumu magumu ya ujenzi wa Taifa letu Kwa kutetea maslahi ya wananchi kwa MAKAMANDA CDM wote walipo TZ nzima!

Pili nitoe pongezi kwa harakati za kuelekea kunyakua viti vingi vya UDIWANI kutokana na chaguzi ndogo zitakazo fanyika th. 16/06/2013 Tanzania kupitia viti 26 wazi.

SWALI ni Je tuhuma za post ya Nape Nauye(ccm) ni sahihi ya kuwa huko Ruvuma ccm imepitwa bila kupingwa katika kata ya Langilo? na kama ndo hivyo ni kwa sababu gani?? Maana mtoa mada licha ya kuwa mpinzani wetu wa jadi japo amelala, amejitahidi kushawishi ya kwamba CDM bado hatujajipanua vya kutosha kiasi kwamba eti bado hatuna watu wa kugombea katika maeneo yayo!!!!!! Nalo kama ndilo tunafanya nini katika maeneo kama hayo ambako ccm inaonekana kuwa na mtaji mkubwa kwa sababu watu hajafikiwa kupewa elimu ya Uraia! kama ujuavyo ccm wao Elimu ya Uraia kwa wananchi ni MWIBA mkubwa!

Asante sana kwa ushirikiano wa kulikjomboa Taifa kutoka kwa wakoloni weusi tena wanadhubutu kujiita watanzania, bila ya kuwajali wenzao!!

Development is the function of Time, With TZ, 50yrs of independence is inversely proportional to development such that;

Devilopment = [K/Time] where K is constant.
 
NIMEPATA MESSAGE HII:

"Nimeona post na nape jf kilichotokea huku Langiro ni hujuma zilizosimamiwa na mke wa katibu mkuu wa wizara ya ujenzi Dr ndunguru za kushinikiza kwa vitisho kutopokelewa kwa fomu za mgombea wetu na kimsingi itawagharimu jimbo 2015 maana huyo dr ndunguru anautaka ubunge wa mbinga mashariki hivyo kuna uhasama mkubwa kati yake na mbunge wa ss bwn kayombo....asilete propaganda za kitoto huku hawapo imara kihivyo....jpili njema Ben"
 
Watakuwa walipitiwa tuu kuweka mgombea au yawezekana fedha ni tatizo

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
Katika hali inayodhihirisha kuwa Chadema wana kufa kwa kasi ya ajabu, wamefikia mahali pa kushindwa kuwa na mgombea wa Udiwani kata ya Langido mkoani Ruvuma kiasi cha kuifanya CCM ipite bila kupingwa na hivyo kuanza na kata moja tayari kati ya kata 26 zinazofanya uchaguzi mdogo.

kama watani hata kusimamisha mgombea tu kwenu inakuwa tabu tena wa kata kweli mko serious kutaka kuaminiwa kukabidhiwa nchi? Hili limenifanya nikumbuke maeneo kibao mwaka 2010 ambayo majimbo na kata hamkusimamisha agombea au mliwatelekeza pale mliposimamisha! Na sasa nasikia nguvu kubwa mnapeleka Arusha!!!!! Mwenye akili na atafisiri hili!

Itawachukua muda kidogo kukomaa!

kwa hiyo kata hiyo ndo kipimo chako cha kifo cha CDM.... Analysis yako haiko realistic... Nakushauri Nape na wana-CCM wengine, msiwe mnaweka wagombea kila eneo, angalieni na eneo. Kwa mfano, jimbo la Moshi kwa Ndesamburo, msiwe mnajihangaisha kusimamisha mgombea....
 
Katika hali inayodhihirisha kuwa Chadema wana kufa kwa kasi ya ajabu, wamefikia mahali pa kushindwa kuwa na mgombea wa Udiwani kata ya Langido mkoani Ruvuma kiasi cha kuifanya CCM ipite bila kupingwa na hivyo kuanza na kata moja tayari kati ya kata 26 zinazofanya uchaguzi mdogo.

kama watani hata kusimamisha mgombea tu kwenu inakuwa tabu tena wa kata kweli mko serious kutaka kuaminiwa kukabidhiwa nchi? Hili limenifanya nikumbuke maeneo kibao mwaka 2010 ambayo majimbo na kata hamkusimamisha agombea au mliwatelekeza pale mliposimamisha! Na sasa nasikia nguvu kubwa mnapeleka Arusha!!!!! Mwenye akili na atafisiri hili!

Itawachukua muda kidogo kukomaa!

Kama kata haijatangazwa halafu inatangazwa siku moja kabla unategemea nn. Hata ivyo una bahati sana kukujibu
 
Tunashukuru sana kwa taarifa katibu mwenezi wetu msaidizi,sasa hii taarifa usisahau pia kuipitisha kwa bosi wako jj mnyika,kwa hatua zingine.pia mkumbushe msaidizi a katibu mkuu wa cdm ndugu kinana,mwambie mbona siku hizi hafanyi kazi zake vizuri mara baada ya kuperfom vizuri pale moro?

Kama chama kimechukua hatua gani baada ya kuona hizo hujuma. Ben lazzima tukubali kuwa hapa viongozi wetu wameteleza. Mm sikubaliani na sababu alizo toa TUMAINI.
 
Last edited by a moderator:
Hata Cuf mbona wapo lakini kama kweli chadema hilo kosa kubwa viongozi wa hayo maeneo waeleze
Huwezi kutegemea kuongoza nchi huku unashindwa kusimamisha wagombea kwenye uchaguzi
 
NIMEPATA MESSAGE HII:

"Nimeona post na nape jf kilichotokea huku Langiro ni hujuma zilizosimamiwa na mke wa katibu mkuu wa wizara ya ujenzi Dr ndunguru za kushinikiza kwa vitisho kutopokelewa kwa fomu za mgombea wetu na kimsingi itawagharimu jimbo 2015 maana huyo dr ndunguru anautaka ubunge wa mbinga mashariki hivyo kuna uhasama mkubwa kati yake na mbunge wa ss bwn kayombo....asilete propaganda za kitoto huku hawapo imara kihivyo....jpili njema Ben"
Mbaazi ikikauka husingizia jua....hizi ni sarakasi tulizozizoea
 
Back
Top Bottom