Mikoa mitatu kutofanya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa, CCM yapita bila kupingwa kwenye kila Kitongoji na Mtaa

Suley2019

JF-Expert Member
Oct 7, 2019
1,811
4,533
Wizara ya Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi) imesema mikoa mitatu haitafanya uchaguzi wa serikali za mitaa kwa kuwa wagombea kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) wamepita bila kupingwa.

Naibu Waziri wa wizara hiyo, Mwita Waitara amesema leo jijini Dar es Salaam kuwa, kati ya halmashauri za wilaya 184 nchini, 90 hazifanyi uchaguzi huo Novemba 24 mwaka huu kwa kuwa wagombea wamepita bila kupingwa.

“Katika mikoa 26 ya hapa bara, kwa taarifa ambazo tumeshapokea mpaka leo asubuhi mikoa mitatu inaonekana kwamba wagombea wa Chama Cha Mapinduzi wamepita bila kupingwa kwa hiyo kuanzia siku ya uteuzi wao ni viongozi halali na wasimamizi wameshawateua, hakuna haja ya kampeni katika eneo hilo” ameyasema hayo wakati anazungumza kwenye kipindi cha Asubuhi Hii kinachorushwa na kituo cha redio cha TBC Taifa cha Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC).

Wakati akizungumza na Habarileo leo mchana Waitara ameitaja mikoa ambayo haitafanya uchaguzi kabisa kuwa ni Katavi, Tanga, na Ruvuma.

“Mahalali ambako mgombea alikuwa peke yake na amepita bila kupingwa kazi ya msimamizi ni kumtangaza na baada ya hapo atasubiri baada ya tarehe 24 ataapishwa na ataanza majukumu yake kwa hiyo hakuna habari ya kampeni lakini mikoa 23 itakuwa na mchakato wa uchaguzi”amesema Waitara.

Kwa mujibu wa kiongozi huyo hata katika mikoa hiyo 23 uchaguzi utafanyika kwenye baadhi ya maeneo.

Amesema, kuna vitongoji 64,000 lakini 3,432 tu vitafanya uchaguzi na kuna mitaa zaidi ya 4,000 lakini mchakato wa uchaguzi utakuwa kwenye mitaa 188 tu. Waitara amesema, Tanzania bara kuna vijiji 12,000 lakini mchakato wa uchaguzi utakuwa kwenye vijiji 1,000.

Amevituhumu baadhi ya vyama kuwa vimewatisha wanachama wao wakilazimisha wajitoe kwa kuwatishia kuwafukuza uanachama.

Amesema Serikali haiingili michakato ndani ya vyama, na kwamba, vyama havitoi maagizo kwa Serikali bali kwa wanachama wake.

Waitara amesema, kwa mujibu wa kanuni anayestahili kujitoa ni mgombea na si chama cha siasa, na kwamba, vyama hivyo vilipewa kanuni hizo Aprili mwaka huu jijini Dodoma hivyo ama hawataki kuzisoma au havisemi ukweli.

“Katika mikoa hii mitatu ambayo haifanyi uchaguzi kabisa, naposema mkoa ninamaanisha kwamba yaani hakuna mahali popote uchaguzi utafanyika isipokuwa mgombea wa Chama Cha Mapinduzi wamepita bila kupingwa maana yake hakuna kitongoji wala mtaa wala kijiji ambacho watakuwa na uchaguzi maana yake hawa wameandika barua wagombea wenyewe”amesema.


Chanzo: Habarileo
 
Copy & past!!! Utasemaje mikoa 3 wakati vyama nchi nzima vimejitoa? Wanataka kuhalalisha uchafu unaoitwa kampeni wakati vyama vingine vilishajitoa!
 
Kwa kweli najuta kujiandikisha.Kwa hali hiii sijui kama kutakuwa na uchaguzi 2020.

Watu mna Moyo,
Sikuthubutu kujiandikisha, mara yangu ya kwanza na mwisho ni 2015 baada ya kuona Kuna uwezekano wa mabadiliko,nikaunga tela.

Sasa imetosha, hao wanaotaka sana kututawala wacha watawale.
 
Suley2019,

Kwanini mnapenda kuhalalisha matumizi mabaya ya pesa za umma, vyama vimejitoa kwanini msiwaapishe watu wenu bila UCHAFUZI WA PESA ZA UMMA mambo yakaisha!!?
 
Mbowe, Lissu na Zitto kwenye form zao za kuwania Ubunge watakosea mambo kadhaa ikiwemo Umri, Jinsi na kushindwa kuandika kwa usahihi Makazi yao


‘...Wanaonikashifu wataumbuka baada ya 2015...’
 
Nyaisonga na pengo wanayajua hayo. Kwamba waumini wao wamenyimwa haki ya kuchagua wawakilishi wawatakao?
 
Mkuu sijutii kujiandikisha kwani nimetekeleza wajibu wangu, na wao walipaswa kutekeleza wajibu wao.
na 2020 nitafanya hivyo, najivunia kuwa mpiga kura.
Wewe upo sawa ila chama tawala walipanga kuuvuruga uchaguzi huu mapema na wanawadanganya wananchi kuwamba kuna uchaguzi.Hili linaleta kero na karaha kwa kutupotezea muda na raslimali kuandikisha watu kuwa wapiga kura ilhali wakiwa wameshatengeneza mazingira ya kupita bila kupingwa.

Wabadili sheria tupige hata kura ya ndiyo au hapana tuone kama hawa waliopita bila kupingwa wanakubalika na wananchi wote?Vinginevyo huu ni udanganyifu na ufisadi wa mali ya umma.We wasted alot of tax payers money for comedian actions.
 
Back
Top Bottom